Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Unahisi USA hana ballistic missiles!!
Ndio hana tupe Ushahidi lini katumia??

Mm nasema hana kwa Ushahidi huu
Wa matendo yake!!

Kama USA yupo kwenye iyo program ya Makombora Kama ya Iranian mbona anafukuzwa na nchi kadhaa hasitumie BASE za nchi zao kama Spain Italy UK nk???

Kama yeye anao uwezo huo kwanini sasa anatafuta Base kwa wengine!!!

kwani Iranian si yupo kwake na mbona tunaona MOTO wake nchi kibao 💥💥💥💥💥 kiasi sasa Dunia nzima tunalipia Ujenzi wa Iranian.!!
.
Kwamaana USA kashindwa kulejesha Dunia vile imekuwa mpaka katafuta Ceasefire lkn lango limefungwa🔒✍️
 
🤣🤣🤣
 
Wewe mlokole mwenzangu unatuibisha sana humu wote tunaonekana hatuna akili Bali mihemko. Ndio wakatoliki wanatudharau mana wako objective sio mihemko kama mlokole wewe.
😄
Yote kwa yote Iron dome na mifumo ya arrows ipongezwe imefanya kazi kubwa na hakuna pingamizi hadi sasa hakuna mifumo bora ya ulinzi kupita hii duniani🤞
🤣🤣 Empty set
 
😄😄😄 Kosa vyote lakini sio Akili , Kuna watu wanapinga kabisa hilo
 
Mnamkumbuka raisi wa Iran Ibrahim rais aliyeitishia Israel na akafa kifo cha utata na hadi sasa haijulikani ilikuwaje

Wewe tu ndio ujui lkn sisi wengine tumeona kwenye Al Jazeera kulikuwa na Ukungu mkali sana ndio Sababu!!!
Itakumbukwa % 90 za ajali zote za ndege Duniani zinatokana na Ukungu kufunika milima✍️

sasa ile ndege imepitia chanzo kikuu cha Ajali yani Ukungu na ndege imekutwa milimani lkn wewe unataka kutwambia ni Mossad️ 🚮

lkn Walokole kwa Propaganda za kusifia Zayuni uku wameshiba Migebuka utowaweza utasikia ni Mossad Aleluyaaaaaaaa 💩🫡🫡
 
Hiyo ni selective reasoning
Israel na US ndio walianzisha huu mgogoro/operations/vita

Lengo lilikuwa
1. Regime change, kwa kuondoa au kuangusha Islamic republic na kuweka puppet government ya mtu wanayemtaka wao, either Shah au moderates katika hao waliokuwa hapo awali
2. Kupunguza nuclear capability ya Iran ambayo walishasema kuwa wameimaliza kwenye 12 day war ya June 2025

Iran walichosema wao watalipiza kisasi
Hawakusema ya kuwa wataua viongozi wa Israel au US. Na hata kama lengo ni hilo hawakuweka time frame ya kwamba by this date tutakuwa tumekamilisha hilo tofauti na US waliosema ndani ya mara Siku 3, mara Week 1, Week 4-6 na siku mpaka zimetimia siku 40 wanashift goal posts na hawajafanikisha lengo hilo
Badala yake licha ya kufanya assassinations za viongozi wa Iran nchi imeendelea kusimama na kuwa na solidarity zaidi kuliko hapo awali in contrast na western media propaganda kwamba wananchi hawaipendi serikali yao wakiamini kuwa wataiasi serikali kama wao walivyokuwa wakiamini na huku wakichochea na kuaminisha watu kuwa serikali ya Iran imeua waandamanaji 30k mara 40k ndani ya wiki 1 jambo ambalo logically haliwezekani kwa dunia ya sasa
Na hili niliwahi kukuuliza kama Israel imeua wapalestina 70k pale Gaza kwa ndege vita, drones, mabomu, vifaru, kuangusha majengo na ndani ya miaka 2 kila aina ya silaha indiscriminately inawezekana vipi kuua watu 40k ndani ya wiki moja kwa risasi za askari wa kutuliza fujo tu mitaani?

Trump kama umemfuatilia anakiri kuwa walichochea maandamano kwa kuwapa silaha kwa kupitia Kurds ambao walimgeuka na anakiri pia Iranians are smart, brave and good fighters

Unahoji kuhusu kutotimiza ahadi ya Iran kulipa kisasi na kuona wameshindwa lakini humu unahoji pia kwanini Iran wanataka kuifuta Israel na hawajafanya hivyo ila ni justification ya Israel kuanzisha vita/mauaji kwa raia wa Iran

Je ni sahihi kwa Israel kupiga vyuo, mashule, research centres, kuua scientists na professors na kubomoa civillian infrastructures na ulitaka Iran afanye hivyo ili aonekane kalipa kisasi kesho wamuite UN kuwa anakiuka sheria za kimataifa?
Si alipiga missiles zenye cluster heads Israel akalalamika UN wakati wao hizo silaha wamezitumia sana Gaza na Lebanon?
Ulikuwa unaleta updates hapa milipuko mikubwa sana hujui silaha walizokuwa wakitumia na kufanya carpet bombing?
Unafahamu pia restraint ya Iran imechangiwa zaidi na nini au kufuata international laws na hasa Geneva conventions na alikuwa akitoa onyo kuwa atapiga maeneo yapi akiguswa na anatoa na early warning ili raia na wasiohusika wasidhurike

Israel ili kumuua Ayatolla Khamenei waliua watu zaidi ya 50, wakaua watoto 160, kumuua Ali Larijani waliua watu 200 kwenye apartment block aliokuwepo, Nasrallah wa Hezbollah waliua watu zaidi ya 100 halafu wanaitwa collateral damage
Hata juzi hapo Lebanon wameshambulia maeneo 100 na kuua watu zaidi ya 100 na kujeruhi wengi zaidi
Hapo kuna proportionality au restraint?
Wapi zile precision strikes za assassinations ili kupunguza mauaji yasiyo ya lazima?

Kutangaza jihad ni rallying cry kupata support, haimaanishi kushika silaha
Hata kupinga upotoshi kama huu wa kwako ni jihad
Kumuua Khamenei ni kama kuua kiongozi wa dini hasa kwa Shia Muslims ambao walimfuata kwa imani ya juu kama Imam au kiongozi mkuu ndio maana mpaka TZ kina Mo Dewji walikuwa kwenye maombolezo, ukipita Dar pale mitaa ya kati utashuhudia
Kuna waShia wengi duniani na huwezi kujua kitu gani kitafuata, either kwa sleeper cells kufanya mashambulizi au kuhujumu assets za US kama walivyofanya, kwa muda na convenience ya kwao

Kwa kuanzia kisasi, Iran alianza kupiga base na embassy za US hapo Gulf. Kuharibu base au embassy ya US is no mean feat, hakuna kitu kikubwa kama hicho. Ulizia mtu aliyeingia pale Drive In kwenye US embassy Dar akuambie ulinzi wake. Ilipopigwa ile ya zamani na ile ya Nairobi mwaka 1998 reaction ya US inajulikana. Ile embassy ya US Baghdad ndio ilikuwa largest ever pale MENA na ile ya Riyadh pia na assets za CIA humo ndani, zote zimepigwa
Hakuweza kufika mainland US lakini kupiga tu hizo embassy umeingia kwenye territory ya nchi husika na kama unafahamu hostage crisis ya kutekwa kwa ubalozi wa US Tehran 1980 ilisababisha Secretary of State kujiuzulu na Rais Jimmy Carter kupoteza uchaguzi na hata miaka ya karibuni hapo Libya kitendo cha balozi wa US kuuawa ubalozini kilisababisha Hillary Clinton kupoteza significant support kwenye uchaguzi wa Urais 2016

Battle wise US na Israel wanaweza kuwa na advantage mpaka sasa na hasara kila nchi inacho cha kupoteza
Licha ya media blackout taarifa zinatoka sasa hivi zinaonesha US wameharibikiwa latest military equipment, Israel haijawahi kupigwa kama hivi tangu iundwe hapo 1948 na Iran wameharibikiwa public na military infrastructure lakini US strategically wamepoteza influence na support ya NATO, kila kiongozi anawakomalia baada ya kupata guts za waIran, Gulf states ambazo wameona hizo base haziwasaidii na shift ya opinions kutoka kwa raia ambao mwanzoni walisupport lakini mwisho wa siku wameona hasara yake
US amepoteza generals wake licha hawakupigwa lakini wameondolewa jeshini kwa hiyo military experience and knowledge yao is as good as dead, hakuna wa kuwasikiliza tena labda kwenye media au akija kiongozi mwengine

Iran wameshaanza kurekebisha kwao kutokana na tozo ya Hormuz ambapo kabla ya vita walikuwa hawapati hata riyal 1 na sasa mpaka US analipia kwa Yuan (siyo dollar) kupitisha meli zake
Huduma ya reli imerejea na inafuatia taarifa ya kurekebisha nyumba karibia zote zilizoharibiwa ambapo trainee na experienced engineers wamefanya kazi kwa kushirikiana na Jeshi.
Iran wanairejesha nchi yao kwenye normal life ndani ya masaa tu. Lile daraja walopiga kabla halijaisha linasndeles na matengenezo. Tehran ulokuwa ukiiripotia kupata milipuko mikubwa sana watu wanaendelea na maisha yao licha ya kiapo cha Trump kurudisha stone age wakati Tel Aviv bado inapokea missiles za Hezbollah

Regime change ni rahisi kutokea US kwa sasa baada ya US Congress kutaka kuita impeachment ya Trump wakati Iran Supreme Leader ni Khamenei mdogo, na IRGC ni kama nyoka waliojivua gamba
Mossad wameiambia Knesset kuwa utawala wa sasa wa Iran ni more extreme na hardline kuliko waliokufa, wamegundua too late kwa hasara kubwa kuwa Khamenei alikuwa na restraint kubwa kivita kuliko hao gangsters wapya wa IRGC
Israel kelele zimeanza kutaka PM aondoke, Jumapili anarudi mahakamani kwenye kesi zake za ufisadi na rushwa

Nuclear enrichement inaendelea na sasa Iran wameapa hakuna wa kuwazuia na wanajitoa IAEA ili wasisumbuliwe. US walifanya surprise attack kutaka kuiba uranium kwa kisingizio cha kwenda kumuokoa pilot lakini aibu ilowakuta hawasemi wakati hapo awali June 2025 Trump alisema waliharibu kila kitu na Iran hana uwezo huo tena lakini wameendelea kupiga hapo Natanz na Isfahan ili kutaka kuifikia mitambo ya nuclear ya Iran walioshindwa kuiharibu licha ya kelele nyingi za kujisifu

Leo hii huko Islamabad, Pakistan negotiations za ceasefire zinafanyika, licha ya reports kuwa Iran hawajatuma mwakilishi, ikishindikana maana yake vita itaendelea

Hapa kilicho baki ni kuomba common sense itawale vita iishe kabisa, watu waheshimiane na kuachana na ubabe usiokuwa na faida na kuleta athari kubwa duniani
 
Mkuu haya maelezo ungeyajengea kwenye mpangilio mzuri wa paragraph zilizopangika vizuri ingependeza zaidi. Ni mateso kusoma haya maelezo yako ambayo pia yanajirudia na yaliyojaa hadaa na uongo
 
Hii comment yako inasikitisha inaonyesha wewe ni mtu usiyekua na uwezo wa kuelewa mambo. Nimekuonea huruma
 
Ukiwa unaandika punguza hasira maana hazisaidii chochote kwenye haya maandishi. Ni sawa na kupiga ngumi ukutani utaumia mwenyewe

Pili jifunze kuacha space kila baada ya paragraph ili kumsaidia anayesoma asome kwa uzuri.

Mwisho, nimeshindwa kujua ulichokusudia nielewe ni kipi.umejaza malalamiko badala ya facts
 
Mkuu haya maelezo ungeyajengea kwenye mpangilio mzuri wa paragraph zilizopangika vizuri ingependeza zaidi. Ni mateso kusoma haya maelezo yako ambayo pia yanajirudia na yaliyojaa hadaa na uongo
Pole kwa kuweza kujua kuwa yamejirudia na kujaa uongo na hadaa bila kusoma

Pole kwa mateso ya kukosa kuleta hadaa na uongo wa “milipuko mikubwa sana”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…