Israel ni nchi ya Wayahudi - Netanyahu

Israel ni nchi ya Wayahudi - Netanyahu

Ni kweli yuko sawa.
Hivi ili kuepusha haya maafa kila siku kwa nini tu sisi Tanzania tukawagawia Israel mikoa ya nyanda za juu kusini minne waje wahamie huku waanzishe makazi ya kudumu huko? Kule wawaachie waparestina.

Kwanza linchi lenyewe likubwa hata uendeshaji limetushinda. Miaka zaidi ya 50 sasa ni kama bora hata kipindi cha ukoloni kulikuwa na umeme wa kutosha kila palipo na watu. Umasikini ndio kabisa umetamalaki. Hatuna hata dila,tupo tu,hatujui hata tunajikwamuaje na huu Umasikini na haya matatizo ya kila siku.

Kuna faida ya kuwa karibu nao. Watatupa challenge sana kimarndeleo.
(Natania tu japo ndio ukweli).
 
Mandela alimtosa Nyerere? Wacha wewe. Mandela kalamba Nobel, kamaliza apartheid, heshima yake duniani Haina mfano nk, huyo mjinga na mpuuzi kuliko wewe?!

Itakuwa buza ya wapi ndugu?
kitu gan kilibadilika ndan ya SA baada ya Mandela kupewa nchi?
 
Wayahudi wapi unao ongelea. Hawa waliopo sasa wametoka nchi za Ulaya kuanzia miaka 75 iliyopita!. Wengi ni waabudu wa dini ya kiyahudi lakini sio kabisa wale waliokuwepo miaka hiyo!. Kuna watu wengi wanaitwa wayahudi kwasababu tu ya kuabudu dini na sio lazima wale jamii hii naona wengi wanajichanganya. Ukifuatilia DNA wayahudi wa miaka 2000 iliyopita wengi wapo North Africa, East Africa na wengine walibaki sehemu ile. Hawa wanao ongoza wengi wametoka German na Poland
hahaaa akili zako bana haziko sawa
 
Acha hizo ndugu. Mtadanganyana hizo huko huko. Mandela alikuwa jembe. Wewe na fake ID kumvaa huyo hujihurumii?
Mandela hajawahi kuwa jembe.
Alisifiwa zaidi na wanyonyaji wa Afrika ikiwamo makaburu.
Sababu alifuata matakwa ya makaburu.
Sifa walizompa ilikuwa ni kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa
 
Kila mdu akipadai kwao miaka 4000 iligopita patakalika kweli Duniani
Wengi kwao hawapajui. maana hakuna hata kitu kimoja cha kihistoria walichoacha babu zao.
Tofauti na wayahudi wanahistoria na eneo lao na ushahidi wanao.
 
Kumbe waarabu wahamiaji ndio walijipachika jina la wapalestina na kudai hiyo ardhi ni yao kumbe waisrael wakomae kabisa hao wapalestina warudi kwenye mataifa ya kiarabu maanake ndiko walikotoka.
 
Yote tisa, nothing justifies kinachoendelea mauaji ya watoto wadogo na kama jana wamepiga hospitali na kuua watu 500
Wameuana wenyewe, kombora lililorushwa na magaidi ya Islamic Jihad.
 
"Wayahudi wameishi katika ardhi ya Israel, ambayo sasa ni nchi ya Israel, kwa takriban miaka 3,500. Tumetawaliwa na Warumi, tumetawaliwa na Wa-Byzantini, wametufanyia mambo mabaya, lakini hawakutufukuza, tofauti na vile watu wanavyofikiria. Upotevu wa ardhi yetu ulitokea wakati wa uvamizi wa Kiarabu katika karne ya saba.

Wa-Arabu waliingia kutoka Arabia na kufanya kitu ambacho hakijawahi kutokea kabla, si Warumi, Wa-Byzantini, si Wagiriki kabla yao, wala Alexanda the great, hakuna aliyewahi kufanya hivyo. Walianza kuchukua ardhi ya mkulima Myahudi. Walileta makoloni ya kijeshi ambayo yalichukua ardhi. Kadri muda ulivyopita, Wayahudi wakawa wachache katika ardhi yetu. Kwa hivyo, ni chini ya uvamizi wa Kiarabu ambapo Wayahudi walipoteza ardhi yao.

Wa-Arabu walikuwa wakoloni, Wayahudi walikuwa wenyeji. Hii ndivyo ilivyokuwa kwenye historia. Wayahudi walipokonywa ardhi yao. Tuliachwa tukitawanyika katika pembe za dunia, tukiteseka kwa sababu hatukuwa na nchi yetu, lakini hatukutoweka na kamwe hatukukata tamaa ya kurudi katika ardhi yetu ya kiasili.

Wa-Arabu, ambao walitawala ardhi, hawakuwahi kuifanya kuwa yao. Ilikuwa ardhi isiyo na watu. Katika karne ya 19, wazo la kurudi Yerusalemu likawa ukweli, na kwa sehemu kubwa, ilikuwa kutokana na msaada wa Wakristo Wakizayuni.

Kwa wazo la kurudi, Wayahudi waliendelea kurudi katika ardhi ya Israel katika karne ya 19. Matokeo ya kurudi huku ni kwamba tukaanza kujenga mashamba, viwanda, na maeneo ya ajira. Wa-Arabu, ambao walikuwa wamehamia katika karne zilizotangulia, sasa wanajiita Wapalestina. Waliibua upya historia na kusema wamekuwepo kwa karne nyingi.

Hawana haki ya kuwa hapa. Ardhi hii ni yetu. Imekuwa yetu kwa miaka 3,500. Ikiwa unachukua nyumba ya mtu, kuwafurusha na kuwapokonya, na hawakukataa madai yao, na wanasema ni madai yetu, na wewe unaiacha kama eneo lisilo na watu.

Na familia na uzao wa watu waliotimuliwa wanarudi, wanajenga nyumba, huna haki ya kuwakataza kuwa hapa. Tunawaambia, mnaweza kuishi hapa, sisi pia tunaweza kuishi hapa, lakini ardhi hii ni yetu, ni nchi yetu.

Na sababu hii ya mzozo inaendelea ni kwa sababu Wapalestina, wanaowakilisha wakoloni wa Kiarabu, uvamizi wa Kiarabu, katika Mashariki ya Kati na maeneo mengine, wanadai kuwa hatuna haki ya kuwa na nchi ya Kiyahudi. Lakini tunayo haki. Kama kuna watu wenye haki ya kuwa na nchi, kama kuna watu ambao hawajawahi kukataa ndoto yao ya kurudi katika nchi yao ya kiasili, basi Wayahudi wanamiliki ardhi hii. Ardhi hii ni ya Wayahudi.

Wapalestina wana uhuru wa kuishi hapa karibu nasi, miongoni mwetu, lakini hawana haki ya kudai kuvunjwa kwa nchi ya Kiyahudi. Hiyo si haki. Hiyo ni dhuluma." Alisema Benjamin Netanyahu alipohojiwa na chombo kimoja cha Habari.
Stori ya upande mmja,tupeni stori ya Wapalestina maana hiyo ya Netanyahu ni ya kujitetea.

Mwenye stori ya upande wa pili nae aiweke ili tulinganishe.

Tujue Mpalestina akitoka wapi maana isijekuwa wakati wa tawala zote hizo za kale na Wapalestina walikuwepo na kutawaliwa pia au isijekuwa ni ugomvi wa watu wa familia Moja.

Kusema Wayahudi walifurushwa na Wapalestina/Waarabu inaleta ukakasi.
 
Back
Top Bottom