Israel yafaulu kumuua waziri wa uchumi wa HAMAS

Israel yafaulu kumuua waziri wa uchumi wa HAMAS

Hallo Israel ni hatari lile Taifa. Hapo ujue amezingirwa kila kona na sio hao tu Lebanon na Parestina,hapo ujue kuna korea kask kuna Iran pia. Lakini anapiga Lebanon huku anachakaza Hamas. Ni hii kweli itakuwa vita vya muda mrefu. Hawa kenge wamechokoza nyuki. Watapigwa wachakae. Wakawaulize Misri vile vita vya siku 6 viliwafanyeje
Kina faiza watakuambia myahudi kashashindwa
 
Hii isitupe kiwewe kwamba kuna sehemu iliyokuwa imechukuliwa na Israeli imekombolewa. Tujikumbushe mwaka 1973 Waarabu waliposhambulia Israeli kwa kustukiza siku ya sikukuu ya Kiyahudi ya Yom Kippur. Misri ilishambulia upande wa Sinai na Syria ikashambulia wakati huohuo upande wa Golan Heights. Katika siku tatu Waarabu walikomboa sehemu kadhaa za ardhi yao zilizokuwa zikikaliwa na Israeli. Israeli ilichukua wiki mbili kujipanga na kujibu mapigo hayo ya kustukiza. Ndani ya wiki mbili wakaziteka upya sehemu zilizokuwa zimekombolewa na wakaenda mbali zaidi na kuteka sehemu mpya nyingine. Furaha ya Waarabu ilidumu chini ya wiki tatu wakaja wakapata kilio kikubwa zaidi. Waarabu hawakuweza kufanya cho chote mpaka Misri ilipokuja kurudishiwa kwa amani sehemu ya Sinai kutokana na mazungumzo ya Camp David kati ya Rais Jimmy Carter wa Marekani, Rais Anwar Sadat wa Misri na Waziri Mkuu Menachem Begin wa Israeli. Masharti ya kurudishiwa Sinai yalikuwa pamoja na Misri kuitambua Israeli kama nchi halali na kuanzisha uhusiano wa kibalozi. Makubaliano hayo yalifanyika Oktoba 1978, miaka mitano baada ya vita vya Yom Kippur vya Oktoba 1973. Sinai aliyorudishiwa Misri ilikuwa kwenye meza ya mazungumzo na si kwa ukombozi wa mtutu wa bunduki.
Hali kadhalika hivi sasa. Tusibweteke kwa mafanikio hayo ya kustukiza ya Oktoba 2023. Hatujui kilio kinachoweza kufuata. Aidha, sijui mwezi Oktoba unaashiria nini kati ya Israeli na Waarabu kwani vitu vingi vinatokea mwezi huo.
Waarabu wanavizia sherehe ya wayahudi ndio wanzishe ugaidi wao. Na km wanataka vita watoe taarifa sio kuvizia
 
Huyu kazi yake ilikua kupanga mipango yote ya matumizi ya fedha, yaani zipi zitumike kwenye ugaidi upi na wapi. Poleni kwa msiba wenzetu wa huku uswahilini mnaowaita wale ndugu.

Israel bado haijaanza kulipiza kisasi.

=========

Israel kills Hamas Economy Minister

PHOTO: GETTY IMAGES

Rear Admiral Daniel Hagari, spokesman for the Israel Defence Forces (IDF), has announced that the Israeli army has killed Jawad Abu Shamala, Hamas' Minister of Economy.

"Tonight [on the night of 9-10 October – ed.], an IDF aircraft killed Jawad Abu Shamala, the Minister of Economy of the Hamas terrorist organisation.

He was in charge of the organisation's finances and allocated funds to finance and manage terrorism inside and outside the Gaza Strip."

Hagari also stated that "one of the senior members of the political bureau of the Hamas terrorist organisation, who served as the head of the organisation's national relations department," had been killed as well.

pravda.com.ua
Wa-Tz tukumbuke haya yanayotokea Gaza ni marejeo ya madhambi ya utawala wa makaburu huko Afr. Kusini. Nchi za Magharibi ziliunga mkono ubaguzi na ukandamizaji wa Weusi kama wanavyounga mkono Israel sasa hivi katika ukatili wao kwa Wa-Palestina.
Ukweli ni kuwa mzungu anamchukia Mwafrika kuliko hata Muisrel anavyo mchukia ndugu yake (rejea Abraham/Ibrahim) Mpalestina.
Sichukii Waisrael, lakini Wa-Palestina Wana HAKI ya kuwa na TAIFA lao HURU.
Ebu jikumbushe George Flloyd alivyouwawa na Wazungu kule Marekani.
 
Solution ni tatu either waungane wawe nchi moja au wapalestina watawanywe kwenye nchi mbalimbali za kiarabu wakaanze upya maisha.
Yaani nchi ya Palestine isiwepo.
Waarabu waache ubinafsi wawachukue ndugu zao kuliko kuwaacha wauwawe wengi hawana hatia bali ni wahanga tu wa udhalimu.
Au waachwe wauwane atakaemmaliza mwenzio ndio apewe haki.
Wasomali hawakushaurika waliachwa wakauwana hadi wamechoka kuuwana wamepumzika.
Shetani ndie aletae vita ili kupata damu kwenye vita wanauhakika wa kupata lita nyingi sana za damu tofauti na ajali.
 
Wa-Tz tukumbuke haya yanayotokea Gaza ni marejeo ya madhambi ya utawala wa makaburu huko Afr. Kusini. Nchi za Magharibi ziliunga mkono ubaguzi na ukandamizaji wa Weusi kama wanavyounga mkono Israel sasa hivi katika ukatili wao kwa Wa-Palestina.
Ukweli ni kuwa mzungu anamchukia Mwafrika kuliko hata Muisrel anavyo mchukia ndugu yake (rejea Abraham/Ibrahim) Mpalestina.
Sichukii Waisrael, lakini Wa-Palestina Wana HAKI ya kuwa na TAIFA lao HURU.
Ebu jikumbushe George Flloyd alivyouwawa na Wazungu kule Marekani.
Kosa lao ni kuvuzia sherehe na kwenda kuuwa watu wasio na hatia wamelipiziwa wanaomba msaada
 
Nisikilize vizuri mkuu
Kama unaamini katika kisasi cha jino kwa jino basi mjadala huu una maana

Taifa la Israel lina Haki ya Kujilinda. Mimi na wengine tunaojua Historia tunaamini bila shaka kabisa kuwa waarabu wameikalia ardhi ya Israel isivyo haki lakini je kuua watoto kama HAMAS walivyofanya ndivyo kunaleta haueni?

Mtu mjinga ama mpumbavu asikulazimishe ukahama kutoka kwenye hekima na kufuata mkumbo wa upumbavu wake.

Tuikemee na kuilaani vita (aina yeyote), hata ya maneno bali tuwatafutie suluhu wanaogombana ili kustawisha amani na mshikamano.

Tanzania tuna utamaduni wa utani wa kikabila ambao unafanyika ktk misiba, sherehe na kadhalika. Chanzo cha utani huo ni kufunika machungu ya mauaji ya vita za kikabila zilizopelekea kugharimu maisha ya watu wengi. Waliamua kupatana na kugeuza uchungu kuwa utani.

Ukitumia akili kidogo utaona namna ambayo amani haijawahi kuwa chaguo baya

Sikuelewi kabisa, yaani mpaka sasa haueleweki, ina maana Israel walipaswa wafanye nini baada ya hayo makombora 4,000 ya HAMAS kuelekezwa Israel. Hebu weka nadharia pembeni utazame uhalsia.
 
Wa-Tz tukumbuke haya yanayotokea Gaza ni marejeo ya madhambi ya utawala wa makaburu huko Afr. Kusini. Nchi za Magharibi ziliunga mkono ubaguzi na ukandamizaji wa Weusi kama wanavyounga mkono Israel sasa hivi katika ukatili wao kwa Wa-Palestina.
Ukweli ni kuwa mzungu anamchukia Mwafrika kuliko hata Muisrel anavyo mchukia ndugu yake (rejea Abraham/Ibrahim) Mpalestina.
Sichukii Waisrael, lakini Wa-Palestina Wana HAKI ya kuwa na TAIFA lao HURU.
Ebu jikumbushe George Flloyd alivyouwawa na Wazungu kule Marekani.

Naomba upitie huu uzi hapa kisha unipe mrejesho, uusome bila ushabiki wowote ukiwa open minded Pongezi kwa Zakazakazi kuufafanua mgogoro wa Israel na Palestina kwa Facts, Ni muislam lakini kaweka dini kando kuelezea ukweli, someni alichoandika
 
Kawaida hiyo.

Myahudi kishachezea kichapo ambacho hajawahi kupokea maisha yake yote.

Hata wafanye nini, ushindi bado ni wa Palestina, kwa muda mchache sana wameweza kukishikilia tena kipande cha nchi yao mpaka leo hii. japo kidogo lakini wamekichukuwa tena.

Leo alfajiri wamesukuma moto mwingine kutokea Lebanon.
Subiri moto.wa Israel atakaowasha

Israel ndilo taifa pekee duniani lenye uzoefu mkubwa wa vita kuliko taifa lolote duniani

Msije kulia lia humu Israel akianza kulipiza kisasi Na kisasi chake huwa kibaya mno.wamemchokonoa kitakachowakuta kila atakayesikia atasikia kuumwa ugonjwa wa pressure

Wameshaua huyo waziri na makomandoo wa hamas elfu moja mia tano

Wanaua high value targets ndiko huanzia

Sasa hivi mawaziri wa Palestina watakuwa kwenye mashimo ya vyoo wanaogopa kuuawa na Israel anytime.

Kwa kuua huyo waziri jeshi la Israel linawapelekea ujumbe serikali ya Palestina kuwa tutawaua wote tumeanza na huyu

Saa hii wengi wa mawaziri wa Palestina yawezekana kabisa watakuwa watakuwa wanetoka kwenye mashimo ya vyoo walomojificha wamekimbilia Iran baada ya huyo waziri kuuawa wakisubiri vita iishe
 
mnafurahia kupiga ngumi moja huku mnapigwa ngumi 20 , hiyo ni dalili ya ukilaza , raha ngumi uzipige muda wote sio kupigwa muda wote uku unashangilia ngumi uliyopiga jana
Tena moja ni kubwa sana, sisi hata robo ngumintunaidhangilia na ni ushindi mkubwa sana.

Ukimtandika myahudi ujuwe umeitandika NATO nzima, si madogo hayo.
 
Solution ni mbili either waungane wawe nchi moja au wapalestina watawanywe kwenye nchi mbalimbali za kiarabu wakaanze upya maisha.
Yaani nchi ya Palestine isiwepo.

Wapalestina na Waisraeli hawawezi kukaa kwenye nchi moja. Ni kama mafuta na maji.

Hii vita itapiganwa mpaka masihi atakaporudi.
 
Wapalestina na Waisraeli hawawezi kukaa kwenye nchi moja. Ni kama mafuta na maji.

Hii vita itapiganwa mpaka masihi atakaporudi.
Wapalestina wenyewe hawana shida sana tatizo wanatumiwa na nchi za kiarabu zisizowapenda Israel

Wanawatumia kama fimbo ya kupiga Israel na wakipata shida wakitaka kukimbia Palestina kwenda uhamishoni kwenye nchi za kiarabu huwakataa

Wapalestina wametekwa nyara na waaarabu waislamu wa nchi za kiarabu
Serikali yenyewe ya Palestina haina udhibiti kabisa na makundi ya wapiganaji wa Hamas

Serikali ya Palestina ni kiwete ina jeshi la serikali lakini vikosi vya wapiganaji vya magaidi wa Hamas ndio hujiamulia chochote wakati wowote wakiamua kuvamia Israel wanavamia hawahitaji kibali cha waziri mkuu wa serikali ya Palestina wala cha mkuu wa Jeshi wa serikali ya Palestina wanavamia

Serikali ya Palestina yaani haina meno kabisa mbele ya Hamas
 
Subiri moto.wa Israel atakaowasha

Israel ndilo taifa pekee duniani lenye uzoefu mkubwa wa vita kuliko taifa lolote duniani

Msije kulia lia humu Israel akianza kulipiza kisasi Na kisasi chake huwa kibaya mno.wamemchokonoa kitakachowakuta kila atakayesikia atasikia kuumwa ugonjwa wa pressure

Wameshaua huyo waziri na makomandoo wa hamas elfu moja mia tano

Wanaua high value targets ndiko huanzia

Sasa hivi mawaziri wa Palestina watakuwa kwenye mashimo ya vyoo wanaogopa kuuawa na Israel anytime.

Kwa kuua huyo waziri jeshi la Israel linawapelekea ujumbe serikali ya Palestina kuwa tutawaua wote tumeanza na huyu

Saa hii wengi wa mawaziri wa Palestina yawezekana kabisa watakuwa watakuwa wanetoka kwenye mashimo ya vyoo walomojificha wamekimbilia Iran baada ya huyo waziri kuuawa wakisubiri vita iishe
Huo mbona wapalestina wa sasa hivi wote wamezaliwa wanauona?

Wale uliokuwa unawaona wakiminywa, wakirusha mawe, sasa ndiyo wanarusha misail zao za kutengeza Tabata. Zilizoisimamisha dunia kwa siku nne.

Mambo yanaendelea huko, sikiliza kimbembe cha wiki ijayo.
 
Mazayuni wamejazana airport wanaikimbia nchi, cheza na misaili za tabata?
 
Wachague option zingine hizo
Option ni ya serikali ya majimbo ambako Palestina inakuwa jimbo huru ndani ya Palestina kama ilivyo Marekani, NK

Lakini Palestina hawataki wanataka lazima Palestina iwe nchi na ijitenge na Israel na Israel hawataki wanataka nchi iwe moja
 
Back
Top Bottom