Kwa sifa ulizotaja nakubaliana USA ni super power.Hiyo kuwa na kambi za kijeshi Kila bara duniani? Ni hatari sana.
Na vipi kuhusu hawa wapinzani wa USA? Yaani BRICS! Je wanawezaje hawa kushindana na USA
Kwasasa wanaweza mkuu na ushahidi upo.
Japo wafanye kazi ya ziada maana BRICS inabebwa sana na China na Russia.
Tofauti na washirika wa USA wote wanajiweza na ni economic giants.
Ili kuwa superpower mkuu ni lazima uwe nguli katika sehemu kuu mbili,kwanza uchumi pili jeshi.
China ni second largest economy duniani nyuma ya USA. China inachangia zaidi ya 40% ya bidhaa za viwandani duniani,asilimia 60 iliyobako ndio dunia iliyosalia inachangia.
China ndio most industrialized nation duniani.
Benki kuu ya China ndio benki inayoongoza kukopesha duniani kuliko hata World bank na IMF.
Imekopesha nchi zaidi ya 138 na imesamehe nchi 40 madeni mazima mazima.
Kitu kama hiki benki kuu ya USA haiwezi hata kwa robo.
China ndio nchi yenye gold reserve kubwa duniani.
China ndio nchi yenye dollar reserve kubwa duniani kuliko USA yenyewe mwenye dollar.
Kwa haya maelezo utagundua kuwa hata kama USA akimuwekea mtu vikwazo basi China anaweza akamuinua kiuchumi.
Kijeshi China ina nguvu na imewahi kupapatuana na USA kwa proxy war na China kuibuka kidedea.Mathalan Korea war 1959. Mvutano wa Southern China sea na utekaji wa visiwa vya Phillipines. Huko kote USA alishindwa dhidi ya China.
Pia Urusi kwa jeshi ndio mbabe kwasasa,hili limejionesha hasa kwenye vita ya Ukraine.
Kwa kueleza maelezo haya nimelenga kukazia mkazo kwamba ndio BRICS wanaweza kushindana na USA and allies haswa China na Russia wakiendelea kuwa imara kijeshi na kiuchumi kama sasa.