Israel yajibu mashambulizi dhidi ya Iran. Yashambulia Iran, Syria na Iraq

Kuna kila dalili WWW3 inakwenda kuanza rasmi........na mwisho wa Israel unakaribia........kumbuka Amerika ameshasema yeye anakaa kando......
America sio Taifa lakuaminika, alisema ata kaa kando kujibu shambulio la Iran ila Iran akiyafukua tena atapeleka meli zake na kutumia military base zake Syria na Jordan kuintafia missile za Iran zisifike Israel
 
Wacha weeeh!
Yaani mishipa ya shingo imekusimama na misuli ya mikono imekaza unatype ukiamini kabisa hiki unachokiandika?
 
Asilimia kubwa ya wanasayansi waliopo USA ni waisrael na ndio wanaowatetea ndugu zao kwa kutumia technolojia wanazozitengenezea usa πŸ‡ΊπŸ‡Έ
 
Kaka watu wanataka mabadiliko na maisha mapya.
Maisha ya hofu sio mazuri mkuu.
Ndio maana Yair Lapid alipokua kiongozi wa mpito kipindi Netanyahu anakabiliwa na kesi za rushwa,Israel na Palestina waliishi vizuri kwa amani maana Yair sera zake zilikua za ujirani mwema kiasi kuna mpaka wayahudi waliwekeza Gaza mkuu.
Hata ilipotokea shambulio oktoba 7 wayahudi waliowekeza Gaza iliwauma sana na ndio maana wanaandamana Netanyahu atoke madarakani maana sera zake za upanuzi wa Israel zinagharimu maisha na amani ya Israel.
 
Asilimia kubwa ya wanasayansi waliopo USA ni waisrael na ndio wanaowatetea ndugu zao kwa kutumia technolojia wanazozitengenezea usa πŸ‡ΊπŸ‡Έ
Kuna wahindi na wachina kwa wingi wanaofikia idadi ya hao waisrael katika sekta ya sayansi usisahau hilo.
 
Ngoja tusubili. Saudia analindwa na Marekani na ana base pale.
Saudia hawezi ruhusu anga lake litumike kumshambulia Iran atakama US ana Military base pale Saudia, kitendo cha kuruhusi basi Iran itajibu ndani mwa Saudia pia.
 
Bei ya mafuta kwenye soko la dunia yamepanda Kwa asilimia 4% sipati picha kama vita itachukua Miezi 6 Hali ya uchumi huku Africa itakuaje
 
Win to win situation... Ndo kitu kilichotokea hapo ila Israel akizidi zaidi ya hapo Marekani atakua kando kusoma mchezo
Tit for tat ndio neno hapo
Kama amepiga Isfahan wanapotengenezes silaha za maangamizi na hakuna majeruhi basi na Iran atatuma ujumbe kwenye sehemu za Israel anapotengenezea silaha Ramat HaSharon

Ni kurushiana vijembe tu
 
Dunia nzima imeripuka na taarifa na dhana kuwa Israel imejibu mapigo ya Iran.Wengine wakaenda mbali na kusema Israel imepiga Iraq,Syria na hiyo Iran.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran wakionesha picha za moja kwa moja ni kwamba hakuna kibaya kilichotokea na shughuli zinaendelea kama kawaida.

Hata hivyo wamesema mifumo ya kiulinzi iliwashwa na kupiga vitu vilivyodhaniwa ni vibaya juu ya anga la Isfaham.

Wachunguzi wa mambo ya nyuklia wamethibitisha kuwa vituo vya nyuklia vya Iran viko salama na vinaendelea na kazi zake kama kawaida.

Tangazo la kufungua anga kwa ndege za abiria za ndani tayari limeshatolewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…