Israel yajibu mashambulizi dhidi ya Iran. Yashambulia Iran, Syria na Iraq

Israel yajibu mashambulizi dhidi ya Iran. Yashambulia Iran, Syria na Iraq

Kuna kila dalili WWW3 inakwenda kuanza rasmi........na mwisho wa Israel unakaribia........kumbuka Amerika ameshasema yeye anakaa kando......
America sio Taifa lakuaminika, alisema ata kaa kando kujibu shambulio la Iran ila Iran akiyafukua tena atapeleka meli zake na kutumia military base zake Syria na Jordan kuintafia missile za Iran zisifike Israel
 
Hizo nchi za kiarabu ndo zizue WW III? Vita ya dunia ilikuwa inakadiriwa ingetokea baina ya Russia dhidi ya Ukraine sio hao Iran na Israel, kwa hesabu nyepesi tu, Israel atakuwa na upande wa washirika wenye nguvu sana sababu hata nchi nyingi za kiarabu hazifurahishwi na vitendo vya Iran.

Piga hesabu zako vyema, nambie mshirika gani wa maana atasimama upande wa Iran? Russia ambaye anavuja jasho huko Ukraine? China? Hayupo. Upande wa Israel huko hakushikiki ana watu wengi sana nyuma yake.
Wacha weeeh!
Yaani mishipa ya shingo imekusimama na misuli ya mikono imekaza unatype ukiamini kabisa hiki unachokiandika?
 
Marekani wanahangaishwa sana na mtoto wao wa kambo.........

Ningependa mdau mwenye uelewa mpana wa siasa na uchumi wa kimataifa atudadavulie kuwa Marekani anafaidika nini na Israel mpaka kuingia hasara na kuhatarisha usalama wa taifa lake kiasi hicho
Asilimia kubwa ya wanasayansi waliopo USA ni waisrael na ndio wanaowatetea ndugu zao kwa kutumia technolojia wanazozitengenezea usa 🇺🇸
 
Labda Tu nikuambie.......vita ndio vinamuweka Israel huko tangu alipotangaza taifa lake.......kumekuwepo na majaribio kadhaa ya kuiondoa Israel upande huo lakini imeshindikana.......kwa lugha nyepesi Israel anakaa hapo kwa ngu u za kijeshi na msaada wa mataifa they nguvu duniani.......

Hivyo vita anapigania kila leo na bado anaendelea kuishi....... threat pekee Kwa Israel kwenye ukanda huo ni Iran pekee
Kaka watu wanataka mabadiliko na maisha mapya.
Maisha ya hofu sio mazuri mkuu.
Ndio maana Yair Lapid alipokua kiongozi wa mpito kipindi Netanyahu anakabiliwa na kesi za rushwa,Israel na Palestina waliishi vizuri kwa amani maana Yair sera zake zilikua za ujirani mwema kiasi kuna mpaka wayahudi waliwekeza Gaza mkuu.
Hata ilipotokea shambulio oktoba 7 wayahudi waliowekeza Gaza iliwauma sana na ndio maana wanaandamana Netanyahu atoke madarakani maana sera zake za upanuzi wa Israel zinagharimu maisha na amani ya Israel.
 
Ngoja tusubili. Saudia analindwa na Marekani na ana base pale.
Saudia hawezi ruhusu anga lake litumike kumshambulia Iran atakama US ana Military base pale Saudia, kitendo cha kuruhusi basi Iran itajibu ndani mwa Saudia pia.
 
Bei ya mafuta kwenye soko la dunia yamepanda Kwa asilimia 4% sipati picha kama vita itachukua Miezi 6 Hali ya uchumi huku Africa itakuaje
 
Win to win situation... Ndo kitu kilichotokea hapo ila Israel akizidi zaidi ya hapo Marekani atakua kando kusoma mchezo
Tit for tat ndio neno hapo
Kama amepiga Isfahan wanapotengenezes silaha za maangamizi na hakuna majeruhi basi na Iran atatuma ujumbe kwenye sehemu za Israel anapotengenezea silaha Ramat HaSharon

Ni kurushiana vijembe tu
 
Dunia nzima imeripuka na taarifa na dhana kuwa Israel imejibu mapigo ya Iran.Wengine wakaenda mbali na kusema Israel imepiga Iraq,Syria na hiyo Iran.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran wakionesha picha za moja kwa moja ni kwamba hakuna kibaya kilichotokea na shughuli zinaendelea kama kawaida.

Hata hivyo wamesema mifumo ya kiulinzi iliwashwa na kupiga vitu vilivyodhaniwa ni vibaya juu ya anga la Isfaham.

Wachunguzi wa mambo ya nyuklia wamethibitisha kuwa vituo vya nyuklia vya Iran viko salama na vinaendelea na kazi zake kama kawaida.

Tangazo la kufungua anga kwa ndege za abiria za ndani tayari limeshatolewa
 
Back
Top Bottom