Israel yajibu mashambulizi dhidi ya Iran. Yashambulia Iran, Syria na Iraq

Israel yajibu mashambulizi dhidi ya Iran. Yashambulia Iran, Syria na Iraq

Mkuu, baada ya ngano kuadimika sisi huku siku hizi tulisha sahau kama ngano ni hadimu au laah, siku hizi matumizi ya unga wa ngano yameshakuwa replaced na unga wa mihogo. Kuanzia chapati, mikate, maandazi tunatumia unga wa mihogo tu.
Hivyo kama issue ni uadimu wa bidhaa zitokazo pale, basi jua tayari dunia ina altenative na huenda hata hiyo vita inachochewa ila hiyo altenative product iingizwe sokoni.
Lakini pia kumbuka mataifa mengi ya Africa bajeti zao zimeegemea kwenye msaada ya wakubwa......ambao muda wana hangaishwa na vita huko mashariki ya kati na lazima vipaumbele vyao zielekezwe huko..... unadhani tutasalimika kwenye hili
 
Jamani mmeshindwa kutuletea hata kasehemu tu ka shambulizi tujionee kwa macho? Mbona kule israeli tulioneshwa vitu Live live?? Au ndo mambo ya America " save the face" 🤣
Iran bado wanaishi karne ya 17, kupiga picha au kuchukua video mpaka upate kibali cha Ayatollah, ni tofauti na Israel.
 
Mkuu hebu nidadavulie kidogo nyuma ya maneno yako kuna maelezo gani ya kufanya dunia iamini hivyo......ukizingatia Iran na wenyewe wamepiga hatua kubwa kiuchumi na kiteknolojia
Iran ana mikwara mingi lakini hana ubavu wa kuendesha vita kubwa, nzito na muda mrefu kwa sababu hizi.
1. Ana matatizo makubwa mnoo ya kisiasa ndani ya taifa lake.
2. Hana uungwaji mkono kutoka taifa lolote kubwa lenye nguvu ya kijeshi.
3. Waarabu wanaomzunguka mpaka sasa wameshindwa kumuunga mkono.
4. Israel ina uungwaji mkono mkubwa kutoka mataifa makubwa ya kivita na wanaomzunguka.
 
Lakini pia kumbuka mataifa mengi ya Africa bajeti zao zimeegemea kwenye msaada ya wakubwa......ambao muda wana hangaishwa na vita huko mashariki ya kati na lazima vipaumbele vyao zielekezwe huko..... unadhani tutasalimika kwenye hili
Pesa nyingi zaidi za magharibi zinaenda kwenye vita vya Ukraine kwa sasa.
 
Kwa hiyo eslael hawakushambulia, then Iran wanataka ku counterattack, which is which? Kuna vitu inabidi utumie tu akili ya std two kudadavua
Kwan kwenye hizo taarifa kuna sehem imesemekana iran kasema Israel hajashambulia.Em soma vizur kabla ya kutoa watu akili
 
Jamaa kapiga sehemu tatu kwa mpigo Iran, Iraq na Syria.
Kuna sehemu Israel amekiri kuhusika na shambulizi lolote? Wapo kimya hadi muda huu tofauti na Iran aliwapa taarifa ya kushambulia na baada ya kushambulia akaweka wazi kwamba ameshambulia.

Israel hajathibitisha chochote so far ameingiwa uoga hata wakutoka hadharani.

Hiyo ni milipuko tu imeripotiwa hakuna sehemu imetaja mashambulizi ya kombora ama vinginevyo.
 
Lakini pia kumbuka mataifa mengi ya Africa bajeti zao zimeegemea kwenye msaada ya wakubwa......ambao muda wana hangaishwa na vita huko mashariki ya kati na lazima vipaumbele vyao zielekezwe huko..... unadhani tutasalimika kwenye hili
Nchi kama Tanzania huwa hazijifunzi, so kusalimika ni ngumu, ila kama ingekuwa ni nchi inayojielewa na watu wenye vichwa ambao vichwani zina chaji, basi migogoro ya hivi ingekuwa ni fursa ya kuiimarisha nchi na kuipeleka kwenye kundi la nchi zilizoendelea.
Ila kwa sasa ni lazima ziathirike kuliko nchi zinazopigana.
 
Back
Top Bottom