Israel yashambulia makao makuu ya viongozi wa Hamas nchini Qatar

Israel yashambulia makao makuu ya viongozi wa Hamas nchini Qatar

ukitaka kuishi vizuri na Israel ungana nae Tu kama anavyofanya Egypt
Waliwekeana mikataba Camp David miaka ya 70 ikasababisha Rais wa Egypt Anwar Sadat kuuwawa na Brotherhood. PM Yitzhak Rabin wa Israel nae aliuwawa na yahudi msimamo mkali kwa kusaini Oslo Accord ili kuleta amani na Palestina. Hao wa sasa Trump kawasainisha Abraham accord wawe na ushirikiano na Israel ila sio wote waliokubali
 
Greater Israel hiyo inaendelea

UN SG anashindwa kukemea na hao wenye nguvu ndio wanaamua wapi wapige kwa wakati gani, matokeo yake wanajiona hawaguswi na sheria
Mara ngapi Israel imekiuka maazimio ya UN Security Council lakini US inamkingia kifua
Kupiga magaidi hakuitaji maazimio ya UN. Hiyo Security council inakuwepo wapi Israel ikishambuliwa?
 
Israel waliishapanga kuwaua hao viongozi wa Hamas kwa muda mrefu ni mpango na US.

Walokifanya ni kuwakusanya wote mahala pamoja na kuwafanyia elimination.

Qatar pia waweza kuwa wahusika ingawa watapiga lugha ya kidiplomasia.

Ila Hamas top leadership wote wamekuwa eliminated isipokuwa kuna taarifa kwamba wapo baadhi ya viongozi ambao hawajaguswa.

Huo ni mpango uloratibiwa na Marekani na zimetumika ndege kadhaa pamoja na UAVs kuzuia uharibifu mkubwa ingawa wapo majeruhi wataopatikana.
Fake news, kiongozi gani amekufa?
 
Wacha iwe hivyo..
Ila inasemekana walikuwa wanakutana kujadili proposal ya cease fire...na inaonekana walikuwa wanaelekea kuikataa...
Ndio maana IDF wakaona hapahapa ndio pakusambaratisha top layer yote..
Kiongozi gani wa Hamas kafariki? Unadhani nao wajinga eeh wana intelijensia pia kutoka Iran, Russia n.k
 
Next stop ni Turkey maana Erdoğan anapiga mdomo sana acha nae afikiwe tutaona kweli ni mdomo tu au nae anaweza jitikisa kama Iran
Huyo mwepeesi sana tu, na washamlia data vizuri tu.
Gateway ya magaidi ni pale kwake kwenda Europe kote.
Atakimbizwa km Bashiru wa Misri.
Hiyo task ipo
 
Kumbe viongozi wapo nje ya nchi wanakula bata huku wananchi wao wakifa na njaa
 
Israel inalazimisha makubaliano ya kuacha vita au inakushambulia ukiwa popote.

Qatar sina imani nao sana huwa ni wanafiki kama UAE, sidhani kama hawakuwa na njia za kugundua au kuzuia jeshi la anga la Israel. Kitendo cha kutishia tu wangefanya IDF isite kushambulia maana of course ingeweza ila kidiplomasia ingeharibu.

Qatar wana Rafale, Eurofighter Typhoon na especially F-15 latest variant ambayo hata Israel imeagiza version yake. Air defence systems wanazo, sio wa kushambuliwa bila kuzungumza nao. Hapa watalalamika to save face.

Hii miaka miwili Israel inatafuta maadui kwa udi na uvumba. Sio serikali ya Iran, sio Hamas, Hezbollah, Houthi.
Netanyahu ameamua abebe lawama asafishe njia kwa atakayefuata ambaye atakuja na diplomasia kupoza upepo kusubiri maadui wajijenge upya kwa tabu.
Iran maadui wakubwa wa Israel na wenye teknojia kubwa ya kivita washindwe kuwazuia wayahudi...Qatar wanaweza kweli? Ukitaka ujue uwezo wa Israel kukufikia wafiche viongozi wa Hamas chumbani kwako.
 
ukitaka kuishi vizuri na Israel ungana nae Tu kama anavyofanya Egypt
Mkuu sio kuungana naye, yani Waarabu wawe wajinga ili mambo yaende, Misri ni mhanga kwa sababu anatumia gharama kubwa ya kulinda mpaka wa Gaza ili kutii masharti ya makubaliano yake na Israel.

Abraham Accord ni mpango wa Marekani wa kuleta mahusiano kati ya Israel na mataifa ya Kiarabu. Lakini haizuii Israel kufanya kinyume na maslahi yake ndio maana unaona Qatar imeshambuliwa na Qatar hawatajibu kitu wala kujitoa kwenye Abraham Accord. Ili Israel ikae na majirani zake wa Kiarabu ni lazima Israel iwe juu na Waarabu wawe chini. Hii ni dhairi kwa mfano Israel inaikalia Palestine na Syria (Golan heights) kimabavu, Lebanon inapigwa muda wowote wakijisikia, Ndege za Israel zinapita anga za mataifa ya Kiarabu (Lebanon, Jordan, Iraq, Syria , Yemen) bila tatizo kinyume chake waarabu wakatishe Israel uone moto wake. Kwa hiyo kuungana na Israel ni kusalimu amri kwa waarabu. Uhusiano huo unakosa maslahi na tija kwa mataifa yao
 
Iran ndiyo Cancer ya Amani ya middle east
 
Iran maadui wakubwa wa Israel na wenye teknojia kubwa ya kivita washindwe kuwazuia wayahudi...Qatar wanaweza kweli? Ukitaka ujue uwezo wa Israel kukufikia wafiche viongozi wa Hamas chumbani kwako.
Umenisoma ila hujanielewa.

Okay, niambie Iranian Airforce ina kitu gani cha kuidhibiti Qatari Airforce?
 
Qatar ni moja ya jamii zenye watu wajinga kifikra au watu wavivu kujifunza.

Qatar ilipopata hela nyingi sana iliamua kununua magari ya kifahari na kujenga majengo ya kifahari, akaacha kujiendeleza kielimu mwisho wake hawana watu wajuzi wala wenye hali ya kujenga jeshi lako.

Israel na Iran Ndio wapinzani hasa, hawa wote wamewekeza kwenye human capital na future ya vizazi 100
 
Hawa wayahudi wenu dawa yao ipo soon wao waendele tu. Sifurahishwi nakile kinacho wapata watoto wasio jua lolote, the day come when they ll be rubbed away the surface of earth, once ll hide back the stone, the stone ll say hey come here there is someone hide on back, stay aware and far to be safe

Fullstop, kwishaaa
 
Iran ndiyo Cancer ya Amani ya middle east
Pro Israel watasema hivyo kwa kuona Iran ni destabilizing factor na Pro Iran watasema Israel ni cancer kama foreigners imposed hapo na wakoloni. Kila mtu anataka kuwa mbabe hapo (power hegemony) Na hao wote ni wana back up na inluence ya US au Russia na China.
Iran kama Persia ilikuwa dola kubwa na ilipambana na dola za Ottoman na Uingereza kuendelea kuwepo. Upande mwengine nayo inapambana na nchi za Kiarabu za Kisunni (Shia expansionist influence) na kufadhili hayo makundi ya wanamgambo
Israel nayo ya kupambana kila siku na majirani zake ndiyo survival kwake
 
Back
Top Bottom