Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Watu wameduwaa! Watu wamebaki midomo wazi kwa jinsi wanavyoona Taifa la Israeli likiinuliwa na kuwa na nguvu kubwa. Nawaonea huruma wanaoamini uongo wa Ibilisi eti Biblia ni maneno ya watu. Biblia ingekuwa ni maneno tu ya watu, basi ahadi alizozitoa Mungu kwa Israeli zisingetimia kwa usahihi wa ajabu kama tunavyoshuhudia leo. Mungu aliahidi mambo makubwa kwa taifa la Israeli, na licha ya vikwazo na mapingamizi mengi, historia imethibitisha wazi jinsi ahadi hizo zilivyotimia.
Baadhi ya ahadi za Mungu kwa Israeli zilizotimia:
Baadhi ya ahadi za Mungu kwa Israeli zilizotimia:
- "Nitawatawanya katika mataifa na baadaye nitawarudisha" (Ezekieli 36:24)
Israeli walitawanywa duniani kote baada ya uharibifu wa Yerusalemu mnamo mwaka 70 BK. Lakini Mungu aliahidi kuwakusanya tena, na mnamo mwaka 1948, taifa la Israeli lilirejeshwa rasmi. Jambo hili sio la kawaida kwa taifa lililotawanyika kwa maelfu ya miaka.
- "Nitakufanya taifa kubwa" (Mwanzo 12:2)
Mungu alimwahidi Ibrahimu kwamba atambariki na kumfanya kuwa taifa kubwa. Leo Israeli ni taifa lenye nguvu, na lenye ushawishi mkubwa ulimwenguni.
- "Nchi ya Israeli itastawi" (Ezekieli 36:34-35)
Mungu kwa kumtumia Nabii wa kweli Ezekieli, alitabiri kwamba nchi hiyo iliyokuwa kame na jangwa itastawi na kuwa na rutuba. Leo, Israeli inaongoza kwa uvumbuzi wa teknolojia ya kilimo na umwagiliaji, na imegeuza jangwa kuwa bustani yenye mazao tele.