Israeli - Imekuwa Taifa lenye nguvu kubwa sawasawa na jinsi Mungu alivyoahidi

Hawa jamaa hawamkubali Yesu na Mama yake wanawapa tuhuma nzito , na wanatuhumiwa kuhusika na kumfanyia hujuma Yesu na watu zake , sasa nashangaa Wagalatia mnakuwa chawa wa Hawa jamaa wakati wanampinga Yesu wanamuona kama Tapeli.
Mungu akisema "ndiyo" hageukigeuki kama kinyonga na kusema "hapana"
Tunachofurahia hapo sio hujuma walizofanya, tunafurahia kutimia kwa ahadi za Mungu, jambo linalodhihirisha kwamba Biblia ni kitabu cha kweli, sio hadithi.

Hata hivyo ipo ahadi nyingine ya Mungu ya kuwakomboa Israeli. Na wao siku inakuja watamwamini Yesu.
 
Ulaya miaka ya nyuma walikuwa wanaitwa Jesus killers , Waroma baada ya Kuukubali ukiristo walioanza kuwachukia na kuwatesa ndio maana kabla ya first crusader war kwenda kuikonboa Jerusalem Jeshi la msalaba lilienda kuwauwa Jews kulipa machungu kabla ya kuingia mzigoni.
Aisee 🤔
 
Watu wameduwaa! Watu wamebaki midomo wazi kwa jinsi wanavyoona Taifa la Israeli likiinuliwa na kuwa na nguvu kubwa. Nawaonea huruma wanaoamini uongo wa Ibilisi eti Biblia ni maneno ya watu. Biblia ingekuwa ni maneno tu ya watu, basi ahadi alizozitoa Mungu kwa Israeli zisingetimia kwa usahihi wa ajabu kama tunavyoshuhudia leo. Mungu aliahidi mambo makubwa kwa taifa la Israeli, na licha ya vikwazo na mapingamizi mengi, historia imethibitisha wazi jinsi ahadi hizo zilivyotimia.

Baadhi ya ahadi za Mungu kwa Israeli zilizotimia:
  1. "Nitawatawanya katika mataifa na baadaye nitawarudisha" (Ezekieli 36:24)
    Israeli walitawanywa duniani kote baada ya uharibifu wa Yerusalemu mnamo mwaka 70 BK. Lakini Mungu aliahidi kuwakusanya tena, na mnamo mwaka 1948, taifa la Israeli lilirejeshwa rasmi. Jambo hili sio la kawaida kwa taifa lililotawanyika kwa maelfu ya miaka.

  2. "Nitakufanya taifa kubwa" (Mwanzo 12:2)
    Mungu alimwahidi Ibrahimu kwamba atambariki na kumfanya kuwa taifa kubwa. Leo Israeli ni taifa lenye nguvu, na lenye ushawishi mkubwa ulimwenguni.

  3. "Nchi ya Israeli itastawi" (Ezekieli 36:34-35)
    Mungu kwa kumtumia Nabii wa kweli Ezekieli, alitabiri kwamba nchi hiyo iliyokuwa kame na jangwa itastawi na kuwa na rutuba. Leo, Israeli inaongoza kwa uvumbuzi wa teknolojia ya kilimo na umwagiliaji, na imegeuza jangwa kuwa bustani yenye mazao tele.
Naku-challenge wewe unayedai Biblia ni maneno ya watu, tunga na wewe ahadi fulani. Chagua nchi moja Afrika uitamkie ahadi hiyo. Tamka jambo ambalo halipo kabisa katika nchi hiyo, useme kwamba litakuwepo baada ya miaka 10 ijayo. Andika tamko lako hilo kwenye kitabu halafu uone jinsi utakavyoaibika baada ya miaka hiyo 10 kupita, kwakuwa hayatatimia utakayotamka!
Wapumbavu ni wengi sana
 
Wapumbavu ni wengi sana
Wapumbavu ni wale wanaosema eti Mungu hayupo. Sio sisi.
Zaburi 14:1 (SUV):
"Mpumbavu amesema moyoni mwake, Hakuna Mungu; Wametenda mabaya, wametenda matendo ya kuchukiza; Hakuna atendaye mema."
 
Wachumba TU Kwa hamas hao, 16,000 wamekaangwa na hamas je wangezichapa na taifa kama Yemen? Hali ingekuawaje
 
Mimi sishabikii vita. Najiuliza tu hao Hamas hawaoni kwamba Mungu anawapigania Israeli? Si waweke silaha chini? Gaza ilikuwa inapendeza sana, sasa yamebaki magofu. Oh, Mungu awafunulie wasome hata Torati waone ahadi za Mungu kwa Israeli
 
Dini ni upofu
Mimi sizungumzii Dini hapa. Nazungumzia jinsi ahadi za Mungu zilivyotimia kwa Israeli kuonyesha kwamba Biblia sio maneno ya watu. Kwani wewe huoni jinsi Israeli ilivyobarikiwa? Hujaona hizo takwimu za GDP? Unless kama wewe mwenyewe ndo macho yamepofuka
 
Watu wameduwaa! Watu wamebaki midomo wazi kwa jinsi wanavyoona Taifa la Israeli likiinuliwa na kuwa na nguvu kubwa. Nawaonea huruma wanaoamini uongo wa Ibilisi eti Biblia ni maneno ya watu. Biblia ingekuwa ni maneno tu ya watu, basi ahadi alizozitoa Mungu kwa Israeli zisingetimia kwa usahihi wa ajabu kama tunavyoshuhudia leo. Mungu aliahidi mambo makubwa kwa taifa la Israeli, na licha ya vikwazo na mapingamizi mengi, historia imethibitisha wazi jinsi ahadi hizo zilivyotimia.

Baadhi ya ahadi za Mungu kwa Israeli zilizotimia:
  1. "Nitawatawanya katika mataifa na baadaye nitawarudisha" (Ezekieli 36:24)
    Israeli walitawanywa duniani kote baada ya uharibifu wa Yerusalemu mnamo mwaka 70 BK. Lakini Mungu aliahidi kuwakusanya tena, na mnamo mwaka 1948, taifa la Israeli lilirejeshwa rasmi. Jambo hili sio la kawaida kwa taifa lililotawanyika kwa maelfu ya miaka.

  2. "Nitakufanya taifa kubwa" (Mwanzo 12:2)
    Mungu alimwahidi Ibrahimu kwamba atambariki na kumfanya kuwa taifa kubwa. Leo Israeli ni taifa lenye nguvu, na lenye ushawishi mkubwa ulimwenguni.

  3. "Nchi ya Israeli itastawi" (Ezekieli 36:34-35)
    Mungu kwa kumtumia Nabii wa kweli Ezekieli, alitabiri kwamba nchi hiyo iliyokuwa kame na jangwa itastawi na kuwa na rutuba. Leo, Israeli inaongoza kwa uvumbuzi wa teknolojia ya kilimo na umwagiliaji, na imegeuza jangwa kuwa bustani yenye mazao tele.
Naku-challenge wewe unayedai Biblia ni maneno ya watu, tunga na wewe ahadi fulani. Chagua nchi moja Afrika uitamkie ahadi hiyo. Tamka jambo ambalo halipo kabisa katika nchi hiyo, useme kwamba litakuwepo baada ya miaka 10 ijayo. Andika tamko lako hilo kwenye kitabu halafu uone jinsi utakavyoaibika baada ya miaka hiyo 10 kupita, kwakuwa hayatatimia utakayotamka!
BIla USA , Israel ni sawa na Congo DRC ndugu yangu.
 
Mimi sizungumzii Dini hapa. Nazungumzia jinsi ahadi za Mungu zilivyotimia kwa Israeli kuonyesha kwamba Biblia sio maneno ya watu. Kwani wewe huoni jinsi Israeli ilivyobarikiwa? Hujaona hizo takwimu za GDP? Unless kama wewe mwenyewe ndo macho yamepofuka
Inasikitisha sana.
 
Si unge-google tu kwanza jamani?
Haya much know nimekusaidia ku-google:

Kulingana na takwimu za hivi karibuni, Pato la Taifa la Israeli (GDP) lilifikia dola za Kimarekani bilioni 513.61 mwaka 2023.

Linganisha sasa GDP ya Israeli na ya nchi hizi:
Norway: GDP ya takriban dola bilioni 482 mwaka 2023.
Austria: GDP ya takriban dola bilioni 480 mwaka 2023.
Nigeria: GDP ya takriban dola bilioni 477 mwaka 2023.
Ireland: GDP ya takriban dola bilioni 476 mwaka 2023.
United Arab Emirates: GDP ya takriban dola bilioni 474 mwaka 2023.

Takwimu zinaonyesha kuwa Israeli inashikilia nafasi ya 27 kati ya nchi 196 katika orodha ya GDP duniani. Hapo tu hujaona kuwa Mungu yuko upande wa Israeli. Nchi yenye eneo dogo tu lakini GDP kubwa namna hiyo.

Source:
Benki ya Dunia (World Bank)
Trading Economics
Country Economy
Global FirePower
Huffington Post
Sasa si sawa na Nigeria tu tena Kwa data za mwaka huu kapitwa mbali sana tena bado inapewa misaada kibao imagine kila badget ya marekani Israel inapewa zaidi ya trillion 20 za kibongo na bado misaada ya dharula na mambo mengine bado na France UK German na Italy
 
Mimi sizungumzii Dini hapa. Nazungumzia jinsi ahadi za Mungu zilivyotimia kwa Israeli kuonyesha kwamba Biblia sio maneno ya watu. Kwani wewe huoni jinsi Israeli ilivyobarikiwa? Hujaona hizo takwimu za GDP? Unless kama wewe mwenyewe ndo macho yamepofuka
Israel nguvu zote ni za USA..subiri USA aache kuwafadhili ndio utajua Israel ni Taifa linalopiganiwa na Mungu au Shetani.
 
Wapumbavu ni wale wanaosema eti Mungu hayupo. Sio sisi.
Zaburi 14:1 (SUV):
"Mpumbavu amesema moyoni mwake, Hakuna Mungu; Wametenda mabaya, wametenda matendo ya kuchukiza; Hakuna atendaye mema."
Umekosea kuna makundi ma 3
Makundi mawili ya wanao sema Mungu yupo na moja linalosema hakuna mungu .

Sasa kati ya hayo makundi mawili ya wanao sema Mungu yupo moja wapo ndiyo la wapumbavu walio kubuuu kuliko hata wale wasemao hakuna Mungu...na ndiyo maana duniani watu wanao ongoza kwa kufanya mambo ya kipumbavu na kipuuzi na kishenzi ni hao hao wanao sema Mungu yupo ...sababu ni ilo kundi mojawapo ya hayo mawili ya wasemao Mungu yupo .
 
Ee Israeli hakika umebarikiwa na Mungu.
Hii Israel???
Screenshot_20230515-172320.png
 
Makundi mawili ya wanao sema Mungu yupo na moja linalosema hakuna mungu .
Weka source ya kuaminika inayotetea hoja yako hiyo. Mimi nimenukuu source inayoaminika iliyotamka Israeli itabarikiwa na sasa tunaona inabarikiwa. Wewe source yako ya hayo makundi matatu ni ipi.
 
Back
Top Bottom