Israeli - Imekuwa Taifa lenye nguvu kubwa sawasawa na jinsi Mungu alivyoahidi

Israeli - Imekuwa Taifa lenye nguvu kubwa sawasawa na jinsi Mungu alivyoahidi

T
Mimi sishabikii vita. Najiuliza tu hao Hamas hawaoni kwamba Mungu anawapigania Israeli? Si waweke silaha chini? Gaza ilikuwa inapendeza sana, sasa yamebaki magofu. Oh, Mungu awafunulie wasome hata Torati waone ahadi za Mungu kwa Israeli
Torati tunayo Kwenye Quran
 
Watu wameduwaa! Watu wamebaki midomo wazi kwa jinsi wanavyoona Taifa la Israeli likiinuliwa na kuwa na nguvu kubwa. Nawaonea huruma wanaoamini uongo wa Ibilisi eti Biblia ni maneno ya watu. Biblia ingekuwa ni maneno tu ya watu, basi ahadi alizozitoa Mungu kwa Israeli zisingetimia kwa usahihi wa ajabu kama tunavyoshuhudia leo. Mungu aliahidi mambo makubwa kwa taifa la Israeli, na licha ya vikwazo na mapingamizi mengi, historia imethibitisha wazi jinsi ahadi hizo zilivyotimia.

Baadhi ya ahadi za Mungu kwa Israeli zilizotimia:
  1. "Nitawatawanya katika mataifa na baadaye nitawarudisha" (Ezekieli 36:24)
    Israeli walitawanywa duniani kote baada ya uharibifu wa Yerusalemu mnamo mwaka 70 BK. Lakini Mungu aliahidi kuwakusanya tena, na mnamo mwaka 1948, taifa la Israeli lilirejeshwa rasmi. Jambo hili sio la kawaida kwa taifa lililotawanyika kwa maelfu ya miaka.

  2. "Nitakufanya taifa kubwa" (Mwanzo 12:2)
    Mungu alimwahidi Ibrahimu kwamba atambariki na kumfanya kuwa taifa kubwa. Leo Israeli ni taifa lenye nguvu, na lenye ushawishi mkubwa ulimwenguni.

  3. "Nchi ya Israeli itastawi" (Ezekieli 36:34-35)
    Mungu kwa kumtumia Nabii wa kweli Ezekieli, alitabiri kwamba nchi hiyo iliyokuwa kame na jangwa itastawi na kuwa na rutuba. Leo, Israeli inaongoza kwa uvumbuzi wa teknolojia ya kilimo na umwagiliaji, na imegeuza jangwa kuwa bustani yenye mazao tele.
Naku-challenge wewe unayedai Biblia ni maneno ya watu, tunga na wewe ahadi fulani. Chagua nchi moja Afrika uitamkie ahadi hiyo. Tamka jambo ambalo halipo kabisa katika nchi hiyo, useme kwamba litakuwepo baada ya miaka 10 ijayo. Andika tamko lako hilo kwenye kitabu halafu uone jinsi utakavyoaibika baada ya miaka hiyo 10 kupita, kwakuwa hayatatimia utakayotamka!
Israel is the EU and NATO Military base in the middle East meant to closely monitor Arabs and the Islamic countries all across the region.

Unlike African, Arab countries are economically strong enough to cause chaos in this interwoven world if they are to be left unchecked.

Bila wazungu kuwapo middle east, Iraq, Iran, Syria na hata Saudi Arabia, zote zingekuwa na silaha za maangamizi kama Nuclear.
 
Israel nguvu zote ni za USA..subiri USA aache kuwafadhili ndio utajua Israel ni Taifa linalopiganiwa na Mungu au Shetani.
Kwani Daudi alivyomshinda Goliati kwa jiwe tu, Trump alikuwepo kumsaidia?
Musa alipoipasua bahari ya Sham, majeshi ya Farao yakaangamia, alikuwepo Obama kumsaidia.
Soma Biblia, mkuu, acha kudanganywa. Marekani wanaijua Biblia. Wanaijua ahadi ya Mungu. Mungu alisema anayelibariki Taifa la Israeli atabarikiwa. Anayelilaani atalaaniwa, ndio sababu wako upande wa Israeli.
 
Weka source ya kuaminika inayotetea hoja yako hiyo. Mimi nimenukuu source inayoaminika iliyotamka Israeli itabarikiwa na sasa tunaona inabarikiwa. Wewe source yako ya hayo makundi matatu ni ipi.
Source ya kuaminika ni kutumia akili tu ...hivi ukitumia akili anaye sema hakuna Mungu na anayesema Mungu yupo ila anamfuata zumaridi na kiboko ya wachawi ni yupi mpumbavu zaidi (tumia logic) kuhusu ushahidi wa biblia yesu anasema bora kuwa moto au baridi kuliko uvuguvugu ...maana yake kama unakubali kubali kwelikweli katika haki yote na kama unakataa kataa kweli siyo kuwa mnafiki wa kidini au mshabiki wa dini ...asilimia karibu yote ya wanao sema Mungu yupo ni wanafiki na mashabiki wa dini tu... kweli haipo pamoja nao (yaani wapo mbali na kweli mioyoni mwao wana mkubali mungu midomoni tu ila matendo yao ni kinyume )
 
Ukitaka kujua dini ni mojawapo ya magonjwa ya akili mabaya sana, basi soma alichoandika mleta mada na wanaocomment.

Siku ikiwa kinyume chake atatafuta tena kimstari kingine ndani ya kitabu hichohicho ili akidhi matakwa yake
 
Wakristo wa bongo wanavyoishabikia Israel wewe usiyejua unaweza dhani Taifa la Israel ni la kikristo yaani linamkubali Kristo.

Kumbe Israel na ukristo ni Mashariki na magharibi. Bali wao hawamuamini Huyo kristo na wanamuona ni Tapeli tuu.

Israel ni katika nchi duniani ambazo ni mashuhuri kwa ushoga,, Napata ukakasi kuwa hili ni Taifa teule sijui Taifa lililobarikiwa,,, kivipi!!

Mungu awe pamoja na Mashoga??? Sasa kwanini aliwaangamiza watu wa sodoma na Gomora kisha awabariki waisrael hawa wa netanyau??

Kuna Namna Mtoa mada unaonekana Akili yako imekuwa overweighted na Mapenzi na Hisia.
 
Ukitaka kujua dini ni mojawapo ya magonjwa ya akili mabaya sana, basi soma alichoandika mleta mada na wanaocomment.

Siku ikiwa kinyume chake atatafuta tena kimstari kingine ndani ya kitabu hichohicho ili akidhi matakwa yake
Upo sahihi watu ni wapumbavu sana
 
mungu yupo ila anamfuata zumaridi na kiboko ya wachawi ni yupi mpumbavu zaidi
Hao sio wapumbavu. Maandiko yanasema fikra zao zimepofushwa na shetani.
 
Hao sio wapumbavu. Maandiko yanasema fikra zao zimepofushwa na shetani.
Hao ni zaidi ya wapumbavu ndiyo maana nikasema ni wapumbavu walio kubuu na maandiko yapo kuthibitisha ninacho sema ...wametajwa kwenye maandiko kuwa hao ni CHUKIZO LA UHALIBIFU LILILO SIMAMA PATAKATIFU ....na yesu alisema hukumu yao ni kubwa zaidi
 
Wakristo wa bongo wanavyoishabikia Israel wewe usiyejua unaweza dhani Taifa la Israel ni la kikristo yaani linamkubali Kristo.
Shida hamsomi Biblia mkajua kwanini Wakristo wanaibariki Israeli.
Ahadi hii ya Mungu kwa Israeli bado iko pale pale:

Mwanzo 12:3 ​

nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; ...
 
CHUKIZO LA UHALIBIFU LILILO SIMAMA PATAKATIFU ....na yesu alisema hukumu yao ni kubwa zaidi
Umetafsiri vibaya. Chukizo la uharibifu ni somo pana, linahitaji uzi wake
 
Shida hamsomi Biblia mkajua kwanini Wakristo wanaibariki Israeli.
Ahadi hii ya Mungu kwa Israeli bado iko pale pale:

Mwanzo 12:3 ​

nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; ...
Tuanze kwanza Neno Israel likitumika katika Biblia linakusudia nini??
 
Tuanze kwanza Neno Israel likitumika katika Biblia linakusudia nini??
Andika uzi wenye kichwa hicho utapata majibu. Tukianza kujadili hilo jina tutatoka nje ya mada.
 
Hawa jamaa hawamkubali Yesu na Mama yake wanawapa tuhuma nzito , na wanatuhumiwa kuhusika na kumfanyia hujuma Yesu na watu zake , sasa nashangaa Wagalatia mnakuwa chawa wa Hawa jamaa wakati wanampinga Yesu wanamuona kama Tapeli.
Aliyewatamkia baraka sio Yesu mzee, usichanganye mambo.
 
Andika uzi wenye kichwa hicho utapata majibu. Tukianza kujadili hilo jina tutatoka nje ya mada.
Uzi wa Nini??

Hatutoki njee ya mada kwa sababu wewe unazungumzia kubarikiwa Taifa la Israel sijui Kuteuliwa Sasa ndio inabidi utufahamishe Neno Israel likitumika katika Biblia linakuwa linamaanisha nini??

Ili tujue madai yako ni ya kweli au umeweka kitu sio sehemu yake.
 
Ukitaka kujua dini ni mojawapo ya magonjwa ya akili mabaya sana
Ungemuuliza kwanza Doctor yeyote usingeandika comment hiyo.
Magonjwa ya akili majina yake haya hapa. Niambie kama unaona jina "Dini" kwenye list hii:
  • Depression
  • Anxiety Disorders
  • Schizophrenia
  • Bipolar Disorder
  • Panic Disorder
  • Obsessive-Compulsive Disorder (OCD)
  • Post-Traumatic Stress Disorder (PTSD)
  • Anorexia, Bulimia, Binge Eating
  • Personality Disorders
  • Psychosis
  • Dementia (eg Alzheimer’s)
  • Attention-Deficit/Hyperactivity Disorder (ADHD)
 
Mimi ukubwa wa Israel siuoni zaidi naiona kama kambi kubwa ya jeshi ya kusimamia maslahi ya marekani pale middle east
Huo ndio uhalisia wa mambo. Hakuna Israel bila US. Siku US akiipa mgongo Israel hilo taifa litafutika kabisa
 
Uzi wa Nini??

Hatutoki njee ya mada kwa sababu wewe unazungumzia kubarikiwa Taifa la Israel sijui Kuteuliwa Sasa ndio inabidi utufahamishe Neno Israel likitumika katika Biblia linakuwa linamaanisha nini??

Ili tujue madai yako ni ya kweli au umeweka kitu sio sehemu yake.
Hujaelewa lengo la mada. Lengo ni kuonyesha kuwa Biblia sio maneno ya watu. Ni Neno la Mungu, ndio sababu ahadi walizoahidiwa Waisraeli zimetimia. Kwahiyo tujadili hapo zaidi. Tukianza kujadili jina Israeli yataibuka majina mengine kama Yakobo, Isaka na Ibrahimu. Mjadala utakuwa umeenda nje ya reli.
 
Back
Top Bottom