ITIFAKI: Ni nani Mkubwa kati ya Waziri Mkuu na Spika wa Bunge?

Hao wanaokesha kwa waganga wakilala kwenye majeneza na makaburi ndio wamjue Mwenyezi Mungu!!??

Tanzania (especially WanaCCM), mtu anakuwa kiongozi si kwa Mwenyezi Mungu kupenda, bali ni kwa uwezo, jitihada na nguvu zao wenyewe.

Akili kubwa zinaongelea maendeleo,
Akili za kawaida zinaongelea matukio,
Akili mbovu (kama zako) zinaongelea watu.

Bila Mwenyezi mungu wasingepata nyadhifa hizo, kama unabisha kawaulize.
 
Attachments

  • 5811616-cda2df17014df6e326b1227a0e29153.mp4
    2.6 MB
Ushakoroga maji na mafuta hapa!

Waziri mkuu ni nambari 3 hapa TZ, hakuna cha mihimili wala protokali.

Kichama, waziri mkuu ndio mwenyekiti wa wabunge wote wa chama, speaker akiwa mmojawapo.

Kama swali lingekuwa limelenga worldwide, pengine kuna nchi jibu lingekuwa tofauti!
Huyo waziri mkuu wako hata katika muhimili wake tu wa 'executive ' bado ni wa tatu kiprotokali.

Ukija kitaifa Rais, Spika na Jaji Mkuu wote wapo juu kiprotokali kwa waziri mkuu.

Shughuli ya kitaifa ikiwa inahusu muhimili wa utawala waziri mkuu atatajwa wa kwanza, watafuata mpaka mawaziri wa kawaida kisha ndiyo ifuatie mihimili mingine.

Vilevile kama shughuli ya kitaifa inahusu Bunge basi ataanza kutajwa spika, naibu spika na wabunge wote kisha ndiyo itafuata mihimili mingine.

Halikadhalika, kama shughuli ya kitaifa inahusu Mahakama basi ataanza kutajwa Jaji Mkuu, Majaji wa rufani, Jaji Kiongozi wa Mahakama kuu, Mtendaji Mkuu wa Mahakama kisha itafuatia mihimili mingine.

Kwahiyo nani kutajwa wa kwanza hii inatokana na shughuli yenyewe inahusiana na muhimili upi.
 
Inatusaidia nini sisi wakulima wa mbaazi?
 
Ushakoroga maji na mafuta hapa!

Waziri mkuu ni nambari 3 hapa TZ, hakuna cha mihimili wala protokali.

Kichama, waziri mkuu ndio mwenyekiti wa wabunge wote wa chama, speaker akiwa mmojawapo.

Kama swali lingekuwa limelenga worldwide, pengine kuna nchi jibu lingekuwa tofauti!
Hapana, waziri mkuu ni namba nne hapa nchini.
 
Ttzo watu weng tulisoma tulikua tunalizarau somo la civics na tuliamini ni somo rahisi na lisilo na umihimu
 
Iko hivi, kuna Nchi (taifa), Serikali, Bunge na Mahakama.
Serikali, Bunge na Mahakama vipo ndani ya nchi, kwa hiyo hapa utagundua mkubwa wao ambaye hata raia wote wanatakiwa kuwa wazalendo kwake na kumpigania kwa jasho na damu katika hali yoyote ile ni nchi (taifa), Rais ni mkuu wa nchi na serikali pia, Spika ni mkuu wa Bunge na Jaji mkuu ni mkuu wa Mahakama, kwa mjibu wa mtoa mada anaulizia itifaki ya nchi lakini watu wametaja mihimili, unapozungumzia itifaki ya nchi hapo habari ya mihimili haipo ndo maana makamu wa rais ni mkuu kwa spika wakati yeye sio mkuu wa mhimili wowote, na spika kiitifaki ni mkuu wa jaji mkuu wakati wote ni wakuu wa mihimili.
Itifaki ya Tanzania iko hivi:-
1. Rais wa JMT
2. Makamu wa Rais wa JMT
3. Rais wa SMZ
4. Waziri mkuu wa JMT
5. Makamu wa kwanza wa SMZ
6. Makamu wa pili wa SMZ
7. Spika wa bunge la JMT
8. Jaji mkuu wa JMT
9. Spika wa baraza la wawakilishi Z'bar
10. Jaji mkuu Zanzibar

NOTE: Marais wastaafu wa JMT, Makamu wa Rais Wastaafu wa JMT na Marais wastaafu wa SMZ kiitifaki ni wakubwa kuliko namba 5 ambaye ni makamu wa kwanza wa SMZ na wote waliopo chini yake hapo yaani 5-10.
 
1. Rais Tanzania
2. Makamu wa Rais wa Tanzania
3. Rais wa Zanzibar
4. Wazari mkuu wa Tanzania
Mkuu, baraza la mawaziri linaweza kuongozwa na raisi wa SMZ kama PM yupo?
  • Kama ndio, huoni kuna shida mahali?
  • Kwenye kurithi uraisi wa JMT, raisi wa SMZ anatoeaje? Katiba ya JMT inamtambua raisi wa SMZ kama mmojawapo wa warithi?

PM wa JMT hapaswi kuwa juu ya raisi wa Tanganyika(kama ingekuwepo) na SMZ?
 
Hapana hawezi, unapozungumzia baraza la mawaziri unazungumzia serikali ya JMT, ambapo viongozi wake wakuu ni Rais, VP na PM. Serikali ya JMT ni mhimili ndani ya nchi kati ya mihimili mitatu, kikao cha baraza la mawaziri serikalini ni sawa na kikao cha bunge katika mhimili wa bunge, ambapo kila mhimili una itifaki yake. Muhimu kumbuka hapa inazungumziwa itifaki ya nchi, ebu jiulize kwa nini spika ni kiongozi mkubwa sana nchini kuliko hata waziri wa afya haingii kwenye cabinet lakini waziri wa tamisemi anaingia?! jibu ni spika sio sehemu ya mhimili wa serikali na baraza la mawaziri ndo serikari yenyewe sasa, ndo maana linatunga sera ndo zinawasilishwa katika mhimili wa bunge.
Rais wa Zanzibar sio sehemu ya viongozi wa serikali ya JMT ingawa anaingia ndani ya Cabinet, kwa kuwa sio kiongozi wa serikali ya JMT ndo maana hawezi kuongoza vikao hivyo, kwa sasa hata kama PM hayupo ataongoza Biteko ila sio yeye. Kwa katiba hii ya sasa, hapo awali rais wa Zanzibar ndo alikuwa makamu wa kwanza wa rais wa JMT, alikuwa anaingia kwenye cabinet kama makamu wa rais sijui kwa sasa anaingia kama nani.
Kwenye kurithi urais Rais wa SMZ hayupo kabisa, kumbuka itifaki ya viongozi nchini ni tofauti kabisa na orodha ya mpangilio wa kurithi kiti cha urais na ni tofauti kabisa na orodha ya rais akisafiri!. Rais na Makamu wakisafiri nchi itakuwa mikononi mwa PM, na MP asipokuwepo atateuliwa waziri yeyote kuongoza hadi pale kati ya rais, VP au PM akirejea.
 
Umesema vyema mkuu! Kwa muktadha huo, SMZ haipaswi kujimbafa sio?

Ilivyo na inavyopaswa kuwa ni vitu viwili tofauti!
  • Itifaki, protokali, mihimili, dola n.k ni vichaka tu vya kutimiza adhma yao ya kukwapua vizuri...SMZ ijitegemee 100%, Tanganyika IFUFUKE...kisha tuulizwe kama tunataka kuungana au lah!
  • No, wasituulize kwakuwa wataiba kura...tutoe talaka 3, tukimrudia iwe kwa utaratibu mwingine unaoleweka!
 
Back
Top Bottom