Uchaguzi 2020 Itokee Lissu akashinda Urais, akakupa nafasi ya kutoa pendekezo, ni kitu gani alichofanya Magufuli utamwomba akiondoe mara moja?

Ggr mwisho dodoma. Reli ya kati inatosha sana mwanza na kigoma
 
Bodi ya mikopo wafanye marekebisho.

Fao la kujitoa.

Uhuru wa kujieleza

Marekebisho kwenye bima ya afya maana sa ivi dawa nyingi zimeondolewa
Kama mambo yenyewe ndo haya tutampa lissu ukatibu tawala...Sasa happy maendeleo ya watu yako wapi na vitu vikwapi...nkajua akija atabomoa madaraja yoote...ah ah lissu bana mwengine atakwambia aongeze mshahara ah ah
 
Katiba mpya ambayo utawala wa jiwe umeutupilia mbali
 
Swali lako liko biased. Ungeuliza ni nn kifanyike sio ni nn kitolewe. Swali la kitoto sana. Swali lako limeelemea upanfe mmoja. Nchi ni yetu wote so kiongozi yeyote ana mazuri na mabaya yake. So wananchi inatakiwa tuchambue mazuri tu kutoka kila pande na kujenga nchi.
 
Serikali iache kufanya biashara ambayo ilikuwa inafanywa na walala hoi, angalia GPSA inavyoshndana na wafanyabiashara wadogo kabsa kuuza peni na ream za karatasi katka taasisi za serikali.
 
Nadhani tulikaa sana kwenye hatua ya kutambaa. Ili tuanze kusimama tulihitaji hiyo "one man show " kidogo. Hii minyororo ya vikao kamati n.k. huchelewesha mambo na kupunguza fedha ambazo zingefanya mambo ya manufaa kwa raia wote.
 
Kamuulize kwanza Zitto, kwa nini alikuwa anashadadia hili suala.
 
bahati mbaya hatoshinda sasa.
 
bahati mbaya hatoshinda sasa.
Kufungua line za simu zilizofungiwa na makampuni ya simu mpaka NIDA watoe vitambulisho vya taifa kwa kila mtanzania. Kurejesha nyumba za serikali na za mashirika ya uma zilizouzwa. Yeye raisi atangaze hadharani kwamba haungi mkono mashoga .
 
Kufuta ukabila na ubaguzi wote wa kivyama
 

umesahau, lazima pia waliochoma moto ofisi za chadema washuhulikiwe
- zile bil 8 pia za mbowe zirudishwe kwenye mzunguko
- wale wabunge waliofukuzwa kisa walienda bungeni wakati wa corona wapewe haki yao maana hawakufanya kosa lolote
- matusi yanayorushiwa kwa polisi, polisi wapewe haki ya kuwaadhibu wanaowatukana ni binadam pia
 
Nadhani tulikaa sana kwenye hatua ya kutambaa. Ili tuanze kusimama tulihitaji hiyo "one man show " kidogo. Hii minyororo ya vikao kamati n.k. huchelewesha mambo na kupunguza fedha ambazo zingefanya mambo ya manufaa kwa raia wote.
Nakubaliana na wewe 100%. Tatizo langu kubwa na Magufuli ni kuonea wapinzani na ukosefu wa haki za binadamu kutia ndani uonevu wa polisi na ku-endorse Wsiojulikana. UKkondoa haya he is a very aggressive leader for development. Wasiojulikana amesitisha, labda kwa pressure ya USA, kwa hiyo akiwa reasonable kwa upinzani basi ni kiongozi mzalendo sana.
 
Nini kitolewe na nini kifanyike vinashabihiana. KUna watu wanamchukia Magufuli kutokana na aliyotenda, ndio maana kuna element ya nini kikomeshwe. Kama kila aliyotenda yanakubalika, kwa nini wamchukie?
 
mradi wa bwawa la umeme austopishe kwanza, amflisi magufuli na kumfunga HAPO MOYO WANGU UTAKUWA N.A. MATUMAINI TENA
Tatizo la huu mradi ni nini hadi usimamishwe?

Mie ningedhani ungesema uendelee ila sio kwa kukamua hela za ndani kupitia kodi, faini za barabarani, fedha za mifuko ya hifadhi, kubana mafungu ya maendeleo ya serikali za miji nk. Maradi kama mradi hauna tatizo, bali ni namna ya utekelezaji wake
 
Usijisumbue hawezi kushinda kamwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…