MImi binafsi kuna mambo ambayo sikubaliani kabisa na Raisi Magufuli, na mengi yamejikita katika style yake ya uongozi ya one man show ya yeye kuwa mihimili yote mitatu ya uongozii, ukiukwaji wa utawala wa sheria nchini, uvunjaji katiba wa makusudi, upendeleo na undugu katika nafasi za uongozi, ukiukwaji haki za binadamu na chuki dhidi ya upinzani na yeyote ambae anamkosoa au kutokubaliana nae hata ndani ya chama chake CCM. Lakini sijaona watu wakiongelea sana mambo haya. Nilitarajia haya ndio yatakuwa mambo Makuu ambayo yatawafanya watu watake kumchagua Lissu kumbadili Magufuli.
Sasa kama watu hawaoni haya mambo kuwa ni tatizo basi Raisi Magufuli sio tatizo kiasi hicho hapa Tanzania. KUmchagua Lissu ili aondoe Chato nadhani ni extreme sana. Suala la pato la kujitoa lina mantiki. Zaidi ya hapo sijaona bado mambo ya msingi.