Uchaguzi 2020 Itokee Lissu akashinda Urais, akakupa nafasi ya kutoa pendekezo, ni kitu gani alichofanya Magufuli utamwomba akiondoe mara moja?

Nini kitolewe na nini kifanyike vinashabihiana. KUna watu wanamchukia Magufuli kutokana na aliyotenda, ndio maana kuna element ya nini kikomeshwe. Kama kila aliyotenda yanakubalika, kwa nini wamchukie?
Kuhusu nn kifanyike. Sauti zetu ni ndogo sana hatuwezi kusikika. Tunaweza umiza vichwa hapa then hata maombi yetu yasisikike. Mi naona jamii forum ni sehemu ya kutolea hasira tu kwa mambo yaliyoko moyoni. Serikali yetu sidhani kama inaichukulia serious. Itachukulia serious endapo itaanza kuona impact.
 
Katiba mbovu,kuukuu ya kijima iliyo jaa viraka,jeshi la polisi la kikoloni lifumuliwe,mageuzi ya mfumo mzima wa elimu yetu toka wa kinadharia hadi wa kivitendo,wizara ya elimu iwekwe kikatiba ili wanasiasa wasiichezee,yapo mengi sana
Kama Katiba ni mbovu sio Magufuli alileta
 
Kama huna la kuongea zaidi ya ushabiki wa kipumbavu kaa kimya
 
Usikate tamaa. KUna jume zinaenyeza na kupita kupitia Jamii Forum. KUmbuka kwamba Jamii Forum na kina Maxello wanafuatwa kila wakati kutokana na mambo yanayopostiwa hadi wamelazimishwa kupitia thread kabla ya kuzipost. Ina maana kuna watu wanasoma ndio aana wanawasumbua JF
 
..Nitamshauri aachane na ujenzi wa gharama kubwa wa ikulu ya kifahari dodoma.

..badala yake fedha zilizotengwa zikasaidie miradi ya maendeleo maeneo mbalimbali ya mkoa wa dodoma.
 
Arudishe UHURU HAKI NA MAENDELEO YA WATU.
 
Twende nao taratibu Mkuu. Siku zote ndivyo inavyokuwa, kuna wa kuelewa na wa kutoelewa, hata jambo rahisi sana.
asilimia kibwa wamejibu tofauti na ulichouliza

ama kweli "You can't be wise and inlove at the sametime"
 
Aanze upya kufufua shirika la ndege. Sio kununua ndege na kupark. bali aanzishe mpango mkakati utakaoliwez sha shirika kufanya kazi kwa faida.
 
CHADEMA Ni SERIKALI? NAJUA CHADEMA NI CHAMA.KAMA WALIKUBALIANA ADHABU NI HIYO KWA WASALITI LAZIMA ITEKELEZWE, NI KAMA CCM WALIVYOMTOSA MBOBEZ MEMBE MAMBO YA VYAMA..
 
1. Afute mara moja sheria za kidikteta zinazoondoa uhuru wa maoni na uhuru wa vyombo vya habari

2. Wakurugenzi waliochaguliwa kwa sababu ya ukada wa CCM badala ya weledi, waondolewe mara moja

3. TISS iundwe upya na ifanye kazi yenye manufaa kwa Taifa badala ya kuteka na kupoteza watu wanaokosoa watawala

4. Waloteuliwa kwa sababu ya undugu, ukabila na ukanda badala ya merits, waondolewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria zote kandamizi zilizotungwa chini ya utawala wake
 
Magufuli anafanya vzr isipokuwa yako mambo kadhaa ya kurekebisha mfano :
(1) Makato kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu yabaki 8%.
(2) Mikopo ya halmashauri kwa wajasiriamali iongezwe ili kuchochea shughuli za uzalishaji mali.
(3)JKT wapewe fedha zaidi za kuanzisha viwanda vingi zaidi hasa ambavyo ni labour intensive kama vya nguo nk ili kuajiri vijana wengi zaidi.
(4) Mazingira ya ufanyaji biashara yaboreshwe zaidi ikiwa ni pamoja na kupunguza urasimu katika uombaji vibali/leseni.
(5)Kuchochea uhuru wa mawazo na hasa mijadala yenye tija ktk jamii juu ya demokrasia na maendeleo ya watu.
 
Hana lolote mtu wenu, subiri utarudi hapa 28/10/2020 kulialia.
Mkuu baada ya Magufuli kushinda jamii forums itakuwa tupu sana hao wote watatokomea gizani na mbelgiji Tundu Lisu
 
Naona unalialia tu. Unaeza ondoa kovu?
 
Afanye haraka kurudisha hospitali ya mloganzila MUHAS tupate university hospital nchini
 
zuio la bunge laive
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…