Nimefuatilia mkutano wa ACT Live unaorushwa na ITV.
Tundu Lissu kapewa nafasi ya kuongea, kaongea kirefu, kisha akaanza kuzungumzia hali ya nchi ndani ya miaka mitano iliyopita, na nia na sababu ya kuiondoa CCM madarakani.
ITV wakamzimia sauti.
Sasa najiuliza kama ITV inafanya kazi kwa maslahi ya CCM si ni bora mngejiunga kwa Humphrey polepole naye alikuwa Live?
Hizi tabia za kipuuzi za vyombo vya habari nchini kufanya Censoring, wapinzani pindi wakiwa Live zinaudhi, na zinakatisha tamaa, na zinaonyesha kuwa hivi vyombo vya habari havijwezi
Nimeona siku hizi ndo mchezo wa TV za online na hii ITV, yaani wapinzani wakianza kupoint out mapungufu ya serikali hii mnawazimia Sauti
Hivi ITV na heshima zenu zote mmekuwa low kiasi hiki?
Wananchi wanakereka kwa upumbavu kama huu
Kama hamtaki kurusha Live matukio ya wapinzani basi acheni.
Leo ITV wamemzimia Sauti Tundu Lissu takribani dakika tano nzima.
Haya mambo ya ajabu sana
Mtoa hoja ujue kuwa mtoa habari (lissu) na msambaza habari ( itv n.k) wote wana wajibu wa kuzingatia miiko, sheria na haki za wengine.
Bila ya hivyo iwapo mzungumzaji atatoa matamshi yanayothibitika kuwa ni ya kashfa, uchochezi, uhaini au uvunjifu wa amani katika jamii, chombo hicho cha utangazaji kitakuwa hatiani kwa uvunjifu wa maadili na sheria kikifikishwa mahakamani, sanjari na aliyetamka maneno hayo.
Kwa kuchelea madhila hayo, ndio maana vyombo vya utangazaji vinachukua maamuzi magumu ya kujidhibiti vyenyewe vinapohisi dalili za kutolewa matamshi kinyume na sheria, maadili, na weledi, vikifahamu kuwa vipandishwa kizimbani hata mtoa habari hatakuwa msaada kwao. Mwanahalisi TV nayo ilijilipua vivyo hivyo.