ITV siyo sahihi kutoa sauti ya Hotuba ya Tundu Lissu katika Mkutano wa ACT-Wazalendo

ITV siyo sahihi kutoa sauti ya Hotuba ya Tundu Lissu katika Mkutano wa ACT-Wazalendo

Duh! Labda wakafungulie account Nje ya nchi ambapo hiyo sheria haifanyi kazi. Kisha waendelee kushare link na subscribers.
Mpaka kufika hatua ya kufanya hivyo Basi tukubali tumerudi zama za masokwe!! Na huyo aliyesababisha ataitwa malaika mkuu
 
Nimefuatilia mkutano wa ACT Live unaorushwa na ITV.

Tundu Lissu kapewa nafasi ya kuongea, kaongea kirefu, kisha akaanza kuzungumzia hali ya nchi ndani ya miaka mitano iliyopita, na nia na sababu ya kuiondoa CCM madarakani. ITV wakamzimia sauti.

Sasa najiuliza kama ITV inafanya kazi kwa maslahi ya CCM si ni bora mngejiunga kwa Humphrey Polepole naye alikuwa Live?

Hizi tabia za kipuuzi za vyombo vya habari nchini kufanya Censoring, wapinzani pindi wakiwa Live zinaudhi, na zinakatisha tamaa, na zinaonyesha kuwa hivi vyombo vya habari havijwezi.

Nimeona siku hizi ndo mchezo wa TV za online na hii ITV, yaani wapinzani wakianza kupoint out mapungufu ya serikali hii mnawazimia Sauti.

Hivi ITV na heshima zenu zote mmekuwa low kiasi hiki?

Wananchi wanakereka kwa upumbavu kama huu

Kama hamtaki kurusha Live matukio ya wapinzani basi acheni.

Leo ITV wamemzimia Sauti Tundu Lissu takriban dakika tano nzima.

Haya mambo ya ajabu sana
Kwenye Redio One walichomoa betri alipoanza kuongea.
 
Mtoa hoja ujue kuwa mtoa habari (lissu) na msambaza habari ( itv n.k) wote wana wajibu wa kuzingatia miiko, sheria na haki za wengine.

Bila ya hivyo iwapo mzungumzaji atatoa matamshi yanayothibitika kuwa ni ya kashfa, uchochezi, uhaini au uvunjifu wa amani katika jamii, chombo hicho cha utangazaji kitakuwa hatiani kwa uvunjifu wa maadili na sheria kikifikishwa mahakamani, sanjari na aliyetamka maneno hayo.

Kwa kuchelea madhila hayo, ndio maana vyombo vya utangazaji vinachukua maamuzi magumu ya kujidhibiti vyenyewe vinapohisi dalili za kutolewa matamshi kinyume na sheria, maadili, na weledi, vikifahamu kuwa vipandishwa kizimbani hata mtoa habari hatakuwa msaada kwao. Mwanahalisi TV nayo ilijilipua vivyo hivyo.
Hayo ni matokeo ya kuwepo kwa sheria mbovu zinazohusu vyombo vya habari.
 
Nadhani ulisikiliza Wenje tunakoelekea na kuwasusia pis
 
Acha Ujinga kwahiyo unataka kutuaminisha kuwa tatizo Hilo limejitokeza leo tangu ITV ianze kufanya kazi.

Kama supersport TVs huwa zinakata signal mechi inaendelea na bado tunaamini Ni matatizo ya kiufundi sembuse kwa Wana siasa uchwara Hawa wa kiafrika.
 
Anza kujiandalia nauli ya kuikimbia nchi kwani baada ya October watanzania kumchagua mh Lissu, itabidi ukimbilie Burundi kwenu.
Nani anataka kufokewa namna hiyo.

Yaani device yako halafu mtu anakufokea, si unazima tu.

Ndio maana tunasema Lisu sio presidential material, abakie kuwa mwanaharakati tu.
 
Tangu Mzee Reggy aondoke ITV imekuwa sio supper brand tena labda sasa ni supper vitoko..
Sasa hivi kuna watangazaji kama wawili hivi nadhani wameahidiwa kupewa uteuzi mmoja ni mwanamama na mwingine ni dume.

Hao wanakera sana na mmoja wao leo yupo kwenye mkutano wa ACT
 
Anza kujiandalia nauli ya kuikimbia nchi kwani baada ya October watanzania kumchagua mh Lissu, itabidi ukimbilie Burundi kwenu.
Viongozi karibu wote wa Chadema huwa wanaongea kwa jazba Sana.

Halafu mnajazana ujinga kuwa ndio akili kubwa.
 
Back
Top Bottom