Uchaguzi 2020 Jaji Kaijage: Baada ya uhakiki, sasa tuna jumla ya wapiga kura 29,188,347. Vyombo vya Habari vitende haki kwa vyama vyote

Uchaguzi 2020 Jaji Kaijage: Baada ya uhakiki, sasa tuna jumla ya wapiga kura 29,188,347. Vyombo vya Habari vitende haki kwa vyama vyote

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ( NEC) mh Jaji Kaijage amesema baada ya kuhakiki daftari na kuondoa majina yanayojirudia sasa wamebakia wapiga kura 29,188,347

Source East africa radio

My take; Kumbe nyomi ya Tundu Lisu si chochote si lolote.

Maendeleo hayana vyama!

======

Daftari la wapiga kura lina wapigakura milioni 29

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa mstaafu, Semistocles Kaijage, amesema daftari la wapiga kura lina wapigakura milioni 29,188,347.

MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC), JAJI WA RUFAA MSTAAFU, SEMISTOCLES KAIJAGE.
Amesema hayo leo katika kikao baina ya NEC na vyama vya siasa nchini.

Amesema bajeti inayotarajiwa kutumika katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu ni Sh. Bilioni 331.7.

Amesema kutakuwa na vituo 80,155 vya kupigia kura na kila kimoja kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500.

Jaji wa Rufaa mstaafu Kaijage amesema jumla ya asasi za kiraia 97 zenye nia ya kuwa watazamaji wa uchaguzi ndizo zimekidhi vigezo na tayari zimepewa taarifa na zinasubiri kupewa vibali wakati ukifika.

Amesema kwa upande wa watazamaji wa uchaguzi wa Kimataifa mwaliko umetolewa na mchakato wa kupokea maombi unaendelea."Wakati ukifika tutawajulisha idadi ya waombaji hao," amesema.

Kuhusu malalamiko ya baadhi ya watendaji wa uchaguzi kutokuwapo ofisini wakati wa uteuzi wa wagombea, Kaijage amesema kitendo hicho ni kinyume cha maadili na kwa namna yoyote hakikubaliki.

" Tume tayari imekutana na wasimamizi wote wa uchaguzi upande wa Tanzania Bara Julai24, jijini Dodoma na msisitizo uliotokewa wazingatie maadili ya Uchaguzi na maelekezo yanayotolewa na NEC,"

Amesema tayari wasimamizi wa uchaguzi wamekwisha kuteuliwa na wanaendelea na mafunzo ambayo yatakamilika Jumatatu.

Pia amevitaka vyama kuwasisitizia wagombea wahakikishe wanajaza fomu kwa usahihi ili kuepuka dosari zinazoweza kuwafanya kushindwa kushindwa kuteuliwa.

Amesema wagombea wana haki ya kisheria ya kuweka pingamizi dhidi ya mgombea mwenzake na kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msajili wa Vyama vya Siasa ni miongoni mwa waliopewa haki hiyo.

Mkurugenzi wa NEC, Dk. Wilson Charles, amesema katika kampeni za uchaguzi wagombea wanatakiwa kutumia lugha ya Kiswahili tu na kama eneo husika hawajui pawepo mkalimani.

Pia amesema haitaruhusiwa kampeni kwenye nyumba za ibada au kutumia viongozi wa dini kuwafanyia kampeni.

Kaijage.jpg
 
Kipindi cha uchaguzi, vyombo vya habari vinatakiwa kuwa makini sana ili kuepusha ( 640 X 640 ).jpg


Hata hivyo hakusema kama vile ambavyo vitakaidi agizo lake vitachukuliwa hatua gani , na wala haifahamiki kama anayo mamlaka ya kushughulikia vyombo vya habari vitakavyotoa habari za upendeleo , maana tayari hapa kibindoni ninayo orodha ya vyombo vya habari vinavyopendelea mgombea mmoja na kutelekeza wengine
 
Hiyo ni data ya kupika yenye nia ovu. Tutajua tu mwisho wa huo mchezo.
Ni kawaida yenu, mnataka daftari la kutoka mbinguni, nyie hololo.Maana kila kitu kwenu hakifai, hata hiyo tume huru mnayoitaka ikiletwa mtaikataa haiko huru.Number hizo za jaji kaijage zimetoka jipimeni ubavu, wapiga kelele
 
Nijuavyo Mimi ni kuwa wengi hawakujitokeza kujiandikisha sababu ya figisu za chaguzi za marudio na S/M. Sasa sijajua hii 29M inatoka wako,isijekuwa kuna kiasi kikubwa cha hii namba itaongezwa kwenye kura za mgombea urais chama tawala ili ionekane kapata kura nyingi na kufikisha adhma ya 90% ya kura.

Anyway,sisi tutadeal na primary votes za kutoka vituoni,huko ndo namba huwa haidanganyi.
 
Kwenye red, kwani wote watajitokeza kupiga kura?

Kwenye blue, kama maendeleo hayana vyama, kwa nini hatuna mgombea binafsi?
 
Katika hao wapiga kura waliojiqndikisha
Milion 27 ni kwa Magu
Milio 2 kwa Lisu
Zilizobaki ni kwa Membe na wengineo
Umewapunja sana bwashee.fanya hivi.
Kura za Lowasa wape hizo mil 6.
Alafu mili 3 watagawana vyama vingine na kura zitakazo aribika humoumo.

Kura mil 20/zilizobaki toa mil 1,hawa mil 1 hawatopiga kura kwa sababu tofauti.
Kura mil 19,000 za Magufuli a.k.a Chuma.
 
Back
Top Bottom