Jaji Mgeta: Niliumizwa na Waziri Mkuu kuchana Hukumu ya kesi niliyotoa kuwa kashindwa

Jaji Mgeta: Niliumizwa na Waziri Mkuu kuchana Hukumu ya kesi niliyotoa kuwa kashindwa

Huyu maza amshukuru mwendazake kumzawadia Ubunge, ila akitaka kuaibika arudi tena kichwa kichwa, mbeleko this time haipo.
 
Itasaidia Nini kwa sasa? Alitakiwa asema jambo hilo wakati uleule angeonekana jasiri na mwenye msimamo madhubuti kuliko kusema sasa.

Alionyesha udhaifu mkubwa sana kwa kutokuchukua hatua kipindi kile akabaki na maumivu Hadi Leo!!

Anawafumdisha nidhamu ya uoga, kwamba ukifanyiwa jambo baya usiseme usubirie Hadi siku ya kustaafu ndipo uelezee kama stori!
Ulitegemea achukue hatua gani yeye kama jaji?
Jaji akishatoa hukumu kinachofuata ni mamlaka zingine kuchukua hatua
 
Ulitegemea achukue hatua gani yeye kama jaji?
Jaji akishatoa hukumu kinachofuata ni mamlaka zingine kuchukua hatua
Apeleke unafiki wake huko.
Amestaafu kwa fedheha, ni bora angekaa kimya kama alivyo fanya mwanzoni kuliko kuonyesha udhaifu wake hadharani.coward!!!
 
Apeleke unafiki wake huko.
Amestaafu kwa fedheha, ni bora angekaa kimya kama alivyo fanya mwanzoni kuliko kuonyesha udhaifu wake hadharani.coward!!!
Ulitaka aseme wakati wa Magufuli halafu unajuwa kingefuata nini? Angeweza kutekwa, angeweza kufunguliwa kesi ya utakatishaji fedha au angeweza hata kuuliwa.

Naunga mkono msimamo wa Jaji Mgeta
 
Ulitaka aseme wakati wa Magufuli halafu unajuwa kingefuata nini? Angeweza kutekwa, angeweza kufunguliwa kesi ya utakatishaji fedha au angeweza hata kuuliwa.

Naunga mkono msimamo wa Jaji Mgeta

Jaji wa aina hii inaonekana hata hukumu zake hazikuwa za Haki, mashaka matupu kama kweli alikuwa anatoa hukumu za haki!!!
 
Itasaidia Nini kwa sasa? Alitakiwa asema jambo hilo wakati uleule angeonekana jasiri na mwenye msimamo madhubuti kuliko kusema sasa.

Alionyesha udhaifu mkubwa sana kwa kutokuchukua hatua kipindi kile akabaki na maumivu Hadi Leo!!

Anawafumdisha nidhamu ya uoga, kwamba ukifanyiwa jambo baya usiseme usubirie Hadi siku ya kustaafu ndipo uelezee kama stori!
Ukituliza akili kidogo utaona mantiki ya aliyoyasema jaji, lakini najua wewe ni kichwa maji huwezi elewa chochote.

Mfumo wa uendeshaji serikali uliopo sasa ndio unaoruhusu hali hiyo iwepo. Katiba haisimamii hayo unayoyaeleza wewe hapa.

Kama huoni kwamba ni taratibu hizo hizo zinazovuruga kila kitu kwa sasa, na kumfanya kila mtu kuwa kama mnafiki vile hata bila kutaka, sababu ni hiyo hiyo ya kuwa na udhaifu katika Katiba.

Huyu Jaji angekaza shingo kama unavyojigamba hapa, wakati huu asingekuwa amefika popote. Leo hii asingepata hata nafasi ya kukumbusha uovu/ubovu tulionao katika mfumo wetu wa uendeshaji nchi.

Kwa bahati nzuri, pamoja na ubovu huo, serikali iliweza kuona upungufu wake, na kwa bahati nzur pia na Jaji naye kawa hakupoteza nafasi yake kwa kukurupuka kama unavyoshauri wewe hapa.

Dawa sahihi ni kuukomesha mfumo huo mbaya, ili uruhusu kila mtu kufanya kazi huru bila kuogopa yatakayomtokea.
 
Miaka 65!!!
nadhani wengi wao hawatambui hata umri wao wa kuzaliwa, ukiwatizama kwa sura zao wengi Wana umri mkubwa!!!

Nawashauri wangeomba kustaafu kwa hiari ili wapate muda wa kufanya kazi zao za kifamilia.

Miaka 55, 60, 65 ni umri mkubwa sana , ni vyema wakastaafu wakiwa na miaka 50.
Hivi wewe una umri gani maana unaongea kama umepata ganzi ya ubongo hivi, aliyekuambia familia inataka ikae na Baba ama Mama masaa 24 bila ya kufanya kazi ni nani?

Wastaafu wengi wanapokuwa nje ya utumishi hujihisi upweke na wengine wasio na shughuli za kufanya hufariki kabisa.
 
Sa Kama Kiongozi kadharau mahakama na hakuna kitu kafanywa wanataka wana nchi tupate wapi Imani na mahakama?
Tanzania Mahakama haijawahi kuwa Huru,Nchi huo aliyehuru ni mwanasiasa, anatunga sheria na bado anaamua namna ya kutumia hiyo sheria.
 
Kaingiliwa uhuru wake badala ya kuchukua hatua wakati ule kuonyesha kuchukuzwa na jambo Hilo badala yake anakuja kutueleza Leo hii anapo staafu!!!!
Huu ni uoga na unafiki ambao haupaswi kuigwa.

Unafiki mtupu
Sheria inasemaje kwa mfano Raia wa kawaida akichana hiyo karatasi ya hukumu iliyotolewa dhidi yake ?
 
Naomba kutofautiana na wewe..

Kwa maoni yangu naona ni vyema kwanza ingejulikana kama ni kweli kuna huyo kigogo( Waziri mkuu) alichana hukumu ya mahakama? au jaji amejitungia stori?

Jambo la pili tujiulize,kama ni kweli alichana hiyo hukumu,ni jambo sahihi kwa kiongozi yoyote wa serikali kuchana hukumu kama hizo?

Jambo la tatu ni tujiulize,kuchana hiyo hukumu,kiongozi huyo aliidharau Mahakama kama mhimili au alimdharau Jaji husika? ( Maana tunaona aliyeumia ni jaji binafsi na wala siyo mahakama)

Kama hayo yote hapo juu ni kweli,je viongozi uliowaorodhesha hapo juu ukiwa na hofu kuwa iko siku nao watatuhumiwa, je wanayo haki ya kuchana hukumu iliyotolewa na viongozi wa mhimili mwingine?

La mwisho ni kuwa,maoni yako japo nayaheshimu, bali yamejaa ukale wa kuwatukuza viongozi uliowaita wa juu hata kama wakifanya makosa ya wazi,watu wakae kimya tu
Kabisa
 
Itasaidia Nini kwa sasa? Alitakiwa asema jambo hilo wakati uleule angeonekana jasiri na mwenye msimamo madhubuti kuliko kusema sasa.

Alionyesha udhaifu mkubwa sana kwa kutokuchukua hatua kipindi kile akabaki na maumivu Hadi Leo!!

Anawafumdisha nidhamu ya uoga, kwamba ukifanyiwa jambo baya usiseme usubirie Hadi siku ya kustaafu ndipo uelezee kama stori!
yaani munavyojifanya wajuaji mpaka munachosha.

Hivi nyinyi huwa hamufanyi analysis ya nchi za kiafrika zinavyotawala hata mukatoa comments hizo?
 
Back
Top Bottom