Jaji Mutungi: Sijazuia mikutano ya ndani ya kisiasa ya vyama

Mbona halishauri Jeshi la POLICE wasitishe mazuio ambayo ni kinyume cha Sheria badala yake anawazuia wahanga wa vitendo hivyo ndiyo wajizuie kufanya shughuli halali za kisiasa zilizopo kisheria?Huyu ni Judge wa aina gani anayeshindwa kukemea uvunjifu wa Sheria aliyoapa kuilinda?
CCM imechoka na haina pumzi tena,tujiepushe nayo.A dying Horse...
 
Halafu eti ni jaji hawa watu TAL alishawasema sema sana hawa watu wakishapewa hivi vyeo kwisha kazi, akili yotee wanampa aliyewateua.
 
Hivi hawa viongozi wa serikali wakoje lakini...?

Kwanini hawawi specific wanapotoa taarifa kwa ajili ya kuwa consumed na umma...?

Hii nayo haijafanunua lolote. Imeongeza utata juu ya utata...

Eti taarifa hii inasema hakuzuia vyama kufanya vikao na mikutano ya ndani ila "wajizuie kwa sasa...."

Wajizuie kwa yapi kwa sasa na yapi kwa sasa yaendelee..??

Taarifa haifafanui na haisemi lolote. Yaani utata juu ya utata, confusion juu ya confusion...!!
 
Hivi huyu mutungi ni jaji kweli au kuna mahali tumeruka step moja
 

Anatumika ku justify the end kama means
 

Maajabu ya Tanzania unaweka mkutano kujulisha watu kuwa utafanya mkutano lakini hujui mkutano huo utafanyika lini. Lakini utafanya mkutano mwingine ikijua siku maalumu ya huo mkutano😂👨👨
 
Sio tu hajazuia

Hata huo uwezo wa kuzuia HANAAAA.


Hivyo akae kwa kutulia
 
Acha kujidhalilisha wewe ngedere
 
Kuna
Ukitaka kuwa msajili unasomea nini wakuu????
 
Kilicho dhahiri ni kuwa tina jeshi la polisi ambalo ni kama genge la wahuni. Haliheshimu sheria, halitumii weledi wala halina maarifa zaidi ya maguvu. Ni jeshi la kigaidi.

Hili jeshi ni la kukemewa, kulainiwa na kuonywa. Unataka kikao na mhalifu cha nini? Mhalifu anachostahili ni kuadhibiwa, hastihili kukaa kwenye kikao.
 
Mutungi ni mhuni wa kawaida sana. Hana sifa za ujaji. Hajui hata anasema nini. Ni mtu wa kupuuzwa.
 
Jaji ambaye hana kumbukumbu hata ya matamshi yake mwenyewe, Jana tu kasema hakuna sintofahamu, leo anasema tuwe wavumilivu wakati jitihada zinafanyika kuwa na kikao kitakachoondoa sintofahamu iliyopo, duh!
 
Duh hiyo sahihi niya mwendo kasi.
 
Yaani anashauri vyama visitumie haki yao ya kikatiba kisa tu wahuni wachache wa polisi hawajui wajibu wao?
Polisi wana matatizo sana kwenye hii nchi. Wenzao wa JWTZ, JKT, Zima Moto, Mgambo, nk. Wametulia tu. Hawana shida na mtu. Ila siyo wao! Kutwa ni kutafuta tu kiki na kujitutumua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…