Jaji Warioba: Miaka yote watu wanaelewa kujaza fomu, lakini 2020 ghafla hawajui. Siasa inataka kuingia kwenye Dini

Naunga mkono hoja ya mh.Jaji Warioba kuwa :-

1)Tukomeshe tabia za wanasiasa kutoa salamu za kisiasa/kuomba kura wakiwa katika mahali patakatifu katika nyumba za ibada....tabia hii imefurutu ADA hata kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani.....

2)Tabia ya kwenda misibani huku tukiwa na sare za vyama vyetu si AFYA KWA JAMII

#Siempre JMT🙏
#Nchi Kwanza 🙏
 
Kwanini hawakuenda mahakamani?

Kubaki unalialia umeonewa wakati hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga uchaguzi ni upuuzi na kupoteza muda.
Umerudi kule kule. Mahakamani gani,inayoweza kuamua haki?. Hii hii ya Tz?
 
Mahakama mwaka 2020 ilishikwa akili na "You know who"
Sio hiyo ya mwaka 2020. Mahakama za Tz serikali ikitia mkono tu tayari imetepeta. Hakuna wenye msimamo kule. Mahakama utazikuta kenya,zina uwezo wa kupingana na serikali kabisa. Wana uwezo kufuta uchaguzi. Wana maamuzi ya kumkamata al-Bashir wa Sudan il-hali serikali haitaki
 
Kwanini hawakuenda mahakamani?

Kubaki unalialia umeonewa wakati hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga uchaguzi ni upuuzi na kupoteza muda.

..MAHAKAMA hiihii ambayo imekuwa ikitumika na Ccm kuwafunga wapinzani kwa KESI ZA MICHONGO?
 
Warioba ana level ya kuwa baba wa taifa
 
Huyo Kinana hayo ameona hayakuwepo 2020 tu?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
Kipindi Cha Kinana CCM waliiba kura ila kwa aligorithm yaani Gap iwe 60-40% kuanzia Kata hadi Urais. Ila kwa JPM aisee hakuna Cha formula yeye alizoa kila kitu kuanzia vijiji hadi Urais 84%+

Yaani mpaka Pemba eti CCM ilishinda majimbo karibu yote!! Seriously?
 
Ila lizee lilikuwa na Roho mbaya sana, Limetesa na hata kuwauwa vijana wa watu waliokuwa TISS kwa kushukiwa tu walikuwa wanampinga
Alikuwa anaogopa kivuli chake mwenyewe, huwa wanasema mara nyingi mtu/kiumbe anayefoka sana na kujitutumua mbele ya kadamnasi mara nyingi huwa hajiamini na ni muoga namba moja! Ref. Nyoka Koboko, ni nyoka anayeongoza kwa uoga na ndiyo maana ishu ndogo tu anaattack, huwa hana kufikiri mara 2, hajui hata kutunza sumu yake kwa matumizi muhimu ya baadaye (Kusaka chakula)
 
Uchaguzi mkuu 2015 Kinana alikuwa katibu mkuu ccm. Demokrasia na haki vilikuwepo wakati huo?!
Kipindi Cha Kinana CCM waliiba kura ila kwa aligorithm yaani Gap iwe 60-40% kuanzia Kata hadi Urais. Ila kwa JPM aisee hakuna Cha formula yeye alizoa kila kitu kuanzia vijiji hadi Urais 90%+

Yaani mpaka Pemba eti CCM ilishinda majimbo karibu yote!! Seriously?

Then demokrasia haiishii tu kwenye uchaguzi, hata ushiriki wa wapinzani kwenye vyombo vya wawakilishi, free media, na uhuru wa maoni ikiwemo vyama vingi kufanya mikutano n.k, and more than other 11 principles of democracy walau hata 9 zilikuwepo. Ila kwa JPM hakukuwepo hata moja so unapo compare factor in Kila kitu sio chaguzi pekee.
 
Hahaha, jamaa alitia fora Chief, CDM kupata mbunge 1 nchi nzima!! Ule wizi utakuwa ulisimamiwa na wahuni akina Bashite/Musiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…