Jakaya Kikwete aliwezaje kufanya mambo makubwa kwa wakati mmoja?

Jakaya Kikwete aliwezaje kufanya mambo makubwa kwa wakati mmoja?

Labda nikupe mfano mwingine.

Ummy Mwalimu alikuwa dhaifu ila huyu Gwajima ni takataka kabisaa.
Kila binadamu ni dhaifu .....that's y viongoz hufanya majukumu kwa muongozo wa katiba
 
KWA KIFUPI,WAKATI WA UTAWALA WA KIKWETE FEDHA NYINGI ZILIZOKUWA ZIINGIE KWENYE HAZINA YA SERIKALI,ZILIINGIA MIFUKONI MWA WATU BINAFSI NA TAASISI BINAFSI KUPITIA UFISADI WA VIONGOZI NA WAFANYABIADHARA WACHACHE WAKUBWA..Unanikumbusha enzi za EPA,IPTL,MEREMETA,ISUE YA UMEME ILIYOKATISHA UWAZIRI MKUU WA LOWASA n.k.Tender nyingi za Serikali zilichukuliwa na WAKUBWA na watoto wao na WAFANYABIAshara WAKUBWA ambao Ni marafiki zao,HUKU WAKILIPA KODI KIDOGO SERIKALINI.Wananchi tulikuwa tunaliShwa makombo TU KUPITIA KUFANYA vibarua kwenye maduka yao makubwa,na vibarua kwenye miradi yao ya ujenzi wa mahekalu yao.Tender nyingi za Barabara na madaraja vilijengwa CHINI ya viwango.Barabara zilizojengwa enzi hizo lami yake leo Ni mashimo tupu,madaraja yao Karibu yote yalishazombwa na mvua za kawaida TU za masika.Kupitia tender "fake na miradi fake" HAZINA YA TAIFA ILIKAUSHWA.Wananchi wenzangu tuvumilie kidogo,matunda ya juhudi za RAIS Magufuli mtayaona baadaye.Chakula ndo kipo Jikoni Kinapikwa,Subirini kitaiva.KWA KWELI,RAIS MAGUFULI MUNGU AMUJALIE AFYA NA MAISHA NAREFU NA MIAKA MINGINE YA YA KUITAWALA TANZANIA HADI ATAKAPOFIKISHA UMRI WA KAMA RAIS JOE BIDEN NA AU UMRI WA The Late Maalum Sharifu Hamadi,NDIPO AACHE URAIS.
Mkuu hapo
......umemaliza kila kitu
 
Kila binadamu ni dhaifu .....that's y viongoz hufanya majukumu kwa muongozo wa katiba
Magu siyo dhaifu ila ni takataka kabisaa. Utakosoa kipi uache kipi. Ndio maana wenye akili timamu wamebaki kuduwaa tu.

Kama nchi tungekuwa tuna safari ya kwenda Mwanza lakini JK akawa anaendesha ndivyo sivyo tungeweza kumkosoa namba ya uendeshaji wake ili arekebishe.

Ila huyu wa sasa badala ya kutupeleka Mwanza, yeye anatupeleka Zanzibar na hataki kukosololewa kuhusu hilo wala kuambiwa chochote. Kuna waliopotea hatujui walipo, kuna waliokufa, waliodhalilishwa na kuna walionyeshewa mvua ya risasi 32 mchana kweupee.
 
Huyu wa sasa amejawa tu na roho ya ubinafsi. Yeye mwenyewe anaishi kama yuko peponi. Ila anapenda wengine waishi kama vile wapo Jehanamu.

Sitokuja nimsahau huyu mzee! Yaani tangu 2015, hakuna kupanda daraja wala nini! Wakati enzi za JK, kila baada ya miaka 3 unatoka daraja moja, kwenda lingine! Huyu wa sasa, amalize tu muda wake aondoke. Anatuchosha tu wafanyakazi.

Mkuu naona kama hili la kuomba muda wake yule Chakubanga uishe aondoke ulisahau. Mimi naamini ndio kafika pale.
Kwanza anakipenda kile cheo, ile kuzungukwa zungukwa, kunyenyekewa na wazalendo kwake anaona fahari sana. Halafu haamini kama akitoka yeye ataekuja kama ataweza kufanya aliyoyafanya yeye. Halafu ukumbuke kuna Binaadam wanataka kutia Mbao Barabarani kuomba aongezewe muda.
Yule bado yupo sana.
 
Kwenye nyuzi za kutoa huruma kama hizi, zijui life ngumu, uwezi kutana na comment ya done kiduku lilo.
 
Wasaalam ndugu wana jamvi!!

Nimefikiri kwa marefu na mapana bila kupata majibu ya baadhi ya maswali yahusuyo utawala wa Dr Jakaya Kikwete enzi za utawala wake. Ni miaka kadhaa imepita sasa toka mzee wetu arudi kijijini kwao Msoga kuendelea na maisha yake ya kawaida baada ya kumaliza muda wake wa kuongoza.

Kuna vitu vingi na vikubwa mno vilifanyika enzi za Jakaya Kikwete lakini havikuzuia mambo mengine kwenda sawa bin sawia.
Kuna nyakati mambo yalikuwa yanakwama lakini yanatatulika ndani ya muda mfupi mambo yalikuwa yanakaa sawa.

Mfano wa vitu ambavyo alivimudu Jk pasi na kuteteleka ni pamoja na:

- Nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma kila ufikapo mwaka mpya wa bajeti

- Ajira za uhakika pasi na urasimu

- Miundo mbinu ya barabara

- Ujenzi wa madarasa na shule za kata

- Ujenzi wa zahanati na hospitali

- Mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu

- Uwekezaji wa pesa kwenye tafiti mbali mbali zihusuzo mambo ya Uchumi kwa ujumla

- Vikao na semanars kwa maafisa wa idara mbalimbali(hawa wote walipata posho zao bila bughuza?)

*NA MENGINE MENGI.

Lakini nchi ilienda na Mzunguko wa pesa mtaani ulikuwa mkubwa biashara zilikuwa zinakua kila uchao kukaongeza wimbi la wafanyabiashara na wawekezaji wa nje na ndani ya mipaka ya nchi yetu. Mashirika na makampuni yalinawiri kwa utajiri na yalitoa ajira kwa ukubwa usio kifani.

Sasa swali langu kwa awamu hii pamoja na kubana matumizi na uzibaji wa mianya ya Rushwa kwa ukali wa hali ya juu ni nini kinachofanya tusione matunda ya huo mfumo? kama mishahara ya watumishi imebaki constant bila kuongezwa tokea JK aondoke???_Suala la ajira lipo wazi sitaki hata kuligusia kwa kifupi hakuna ajira za uhakika awamu hii lakini bado kunaonekana kuna uhaba na umasikini mkubwa kwa taifa na mtu mmoja mmoja??

Nawakaribisha mezani tutete!!
Umesahau wapinzani aliwaachia pia waongee wanavyotaka
 
Pata gharama zinatumika;
kujenga Chato
Kununua ndege
Sgr n.k.

Angalia jinsi tenda na miradi ya ujenzi inavyoendeshwa awamu hii;
Tanroads
Suma jkt
Tba

Utaona tofauti ya uongozi unaotawanya rasilimali za taifa kwa wote na ule unaoelekeza rasilimali za taifa eneo moja.
Utaona uongozi unaothamini mchango wa sekta binafsi na hivyo wengi kufaidika na tenda/miradi, na ule unaopendelea taasisi fulani, na sekta binafsi kusahauliwa.
 
Mnaolalamika maisha magumu mlikuwa wapigaji tu kipindi cha JK. Eti "naweza toka mishe ghafla nakuta pochi imejaa minoti". Hivi pesa inaweza kuwa rahisi kiasi hicho mahali gani pengine wapi duniani? Siyo kipindi cha JK watu walikuwa wanajilia rushwa wanavyotaka.
Kati ya mambo ambayo hayaleti tofauti kati ya awamu ya 4 na ya 5, ni rushwa. Ipo pale pale.
 
Katika kipindi cha huyu mzee aisee niliokota sana pesa kwangu elfu 5, 10, 20, 50 hata laki,... hazikunipiga chenga.

Naweza toka mishe gafla nakutana na pochi au waleti zimejaa minoti hatari.

Kipindi kile pesa zilikuwa nje nje na mzunguko ulikuwa mzuri sana. Ila toka huyu mkulu aingie madarakani pesa kubwa niliyookota ni mia tano huwezi amini.

Hiyo inaleta tafsiri kuwa hali ni ngumu sana sasa hivi, hata mzunguko wa hela umekuwa finyu sana kiasi kwamba hata mia tano ukiwa nayo unailinda kama mboni ya jicho.

Abarikiwe sana huko alipo huyu mzee kikwete japo na yeye hakuwa perfect ila itoshe kusema alikuwa bora sana.

Kwangu mimi huyu alikuwa bora sana kuliko huyu mpenda sifa na mapambio.

Ni mtazamo tu.
Kwa tafsiri rahisi inaonesha wewe jamaa ni choko mitaa flani,haiwezekani uwe unaokota elfu 5,10,20,50 hata laki yani wewr tu ndio uokote hizo ela....kuna watu kwa makusudi kabisa walikuwa wanakutegeshea hizo ela ukiinama kuziokota wanakupa nao hapo hapo juu kwa juu
 
Nikiri hata mimi kweli alikuwa bomba sana, kila mtu alimwacha afanye anavyotaka, majambazi yaliba mchana kweupe, banki zilivamiwa hadharani na wazi, mafisadi yaligawana pesa kwa magunia, rushwa ilikuwa waziwazi na watumishi ilikuwa ni halali kuingia kazini akiwa kachelewa au haingii kabisa kazini
You are the captivity of your own negativities!Hukuona jema hata robo!?Mungu akurehemu.
 
Mnaolalamika maisha magumu mlikuwa wapigaji tu kipindi cha JK. Eti "naweza toka mishe ghafla nakuta pochi imejaa minoti". Hivi pesa inaweza kuwa rahisi kiasi hicho mahali gani pengine wapi duniani? Siyo kipindi cha JK watu walikuwa wanajilia rushwa wanavyotaka.
Machoko ao na wauza nyapu.

Kuna watu mjini hapa kazi yao kusifia watu ili wapate shibe yao na ndio hao hao wamekamata social networks.
 
Back
Top Bottom