Jamaa alieoa dada yangu mgumu kuwasiliana na sisi ndugu wa mkewe

huyu jamaa ni kweli tulimkabidhi dada yetu kifamilia, lakini baada ya miezi 6 kupita kuwasiliana adi tumpigie sisi, na sisi tumeamua hatutomtafuta akijisikia sawa tu, jengine bado hajamalizia mahari, kuhus maisha wanaishi vizuri na dada yetu ila sina uhakika 100%.nyie vijana acheni zadhau, tu nampigia tu dada yetu. yeye no.
Kwani lazima?
 
Huyo jamaa tangu mumkabidh dada yako mwaka wa hadi sasa?
 
huyu jamaa ni kweli tulimkabidhi dada yetu kifamilia, lakini baada ya miezi 6 kupita kuwasiliana adi tumpigie sisi, na sisi tumeamua hatutomtafuta akijisikia sawa tu, jengine bado hajamalizia mahari, kuhus maisha wanaishi vizuri na dada yetu ila sina uhakika 100%.nyie vijana acheni zadhau, tu nampigia tu dada yetu. yeye no.
Mahari inahalalisha biashara ya utumwa kwa dada yenu.
 
Akili za kimaskini hizi. Sema unadai mahari sasa gia ya kuingilia ndo tatizo.
Kwenye mahusiano mengi mashemeji wengi wanawaza kupiga hela tuu. issue za mahusiano ooh kupiga simu ni geresha tuu. kwani wao wanakatazwa kupiga simu? Mimi ndoa yangu ina zaidi ya miaka 15 kwa sasa ila nimeamua kuchinjia baharini mijinga jinga yote inayoitwa mashemeji. Nilioa, nikalipa mahari yote, nilihangaika baba yao alipoumwa hadi akafariki tukaenda tukazika. Miaka michache baadaye mama yao akaumwa nikahangaika naye hadi nikamchukua nikamleta kwangu kumuuguza kila kitu nikawa nagharimikia hadi bima nikamkatia. Hapo kuna mashemeji wakikwama kidogo wanampigia dada yao ananiambia kwa huruma nawasaidia.Baadaye mama akaforce kurudi kwao nikamrudisha. Tukaendelea kumuuguza hadi akafariki nilienda nikagharimikia almost nusu ya gharama zote za msiba. baada ya mwaka, mama yangu mzazi akafariki. Umbali wa mahali msiba wa mama yangu ulipotokea na kwa wakwe zangu nauli ni sh 5000. Lakini hakuna aliyekanyaga kwa kisingizio cha kukosa nauli, mashemeji zangu wana familia zao, mwingine anamiliki duka, mwingine mashine ya kusaga na mashamba kibao. Nikawapa taarifa kwamba sisi tumeandaa gari Costa kusafirisha mwili pamoja na abiria basi mwakilishi afike atasafiri na kurudi bure. Maana yake akisafiri hadi msiba ulipotokea gharama a kusafiri kwenda kwetu ni bure, takriban nauli ya kwenda na kurudi isingepungua 50k. bado hakuna aliyetokea. Yaani wao wameshindwa kuchangishana hata wamtume mmoja aje wawakilishe? Gari lililokodiwa lilienda na abiria pungufu, Nilienda msibani na mke wangu tuu. Wao haya kuja hawakuja, basi hata salamu za rambirambi hata wangechangishana wakatuma hata kwa M Pesa hata elf moja haikutumwa.

Baada ya miaka michache napigiwa na Bwashemeji ananiambia mbona sipigi simu wala siendi kuwatembelea? au kwa vile wazazi wamefariki wote sasa hata wao siwatembelei? Niliwaza cha kumjibu sikupata. Mimi ni wa muhimu kwao as far as nawapa chochote, ila kibao kikigeuka kwangu hawana muda.Basi kila mtu ashinde mechi zake
Wape makavu
 
Imeandikwa utawaacha wazazi na kuambatana na make/Mme wako
Hawa ndio waharibifu wa ndoa za watu,wameshasahu ile sendoff maana yake nini,walikula ubwabwa na soda sasa wanataka sijui irudiwe tena...?...
 
huyu jamaa ni kweli tulimkabidhi dada yetu kifamilia, lakini baada ya miezi 6 kupita kuwasiliana adi tumpigie sisi, na sisi tumeamua hatutomtafuta akijisikia sawa tu, jengine bado hajamalizia mahari, kuhus maisha wanaishi vizuri na dada yetu ila sina uhakika 100%.nyie vijana acheni zadhau, tu nampigia tu dada yetu. yeye no.
Ameoa dada yenu au familia nzima?
 
Niko kwenye mpango wa kuwapigia wakwe simu mara moja kila baada ya miaka mitatu na nitakuwa nikifanya hivyo kwa kutumia simu ya binti yao.

For emergency ni wakati wowote lkn eti blaablaa kama alalamikavyo mtoa mada nimeona ni kujitafutia matatizo tu kwa uzoefu niliopitia miaka kadhaa nyuma.
 
Sio huyo pekee me mwenyewe kuwasiliana nao huwa ngumu sana na mpaka sasa na miaka 15 kwenye ndoa
Suala la kumalizia mahari sio lazima kwa wakati huu
 
Sasa awatafute ili iweje? Mtakutana kwenye matukio mkuu. Mimi ndugu wa mke niwatafute ili iweje, watu pekee ninaowasamilia once a while ni WAKWE.

Ndugu tutawasiliana kukiwa na tukio, wife awasiliane na ndugu zake, mimi ndugu zangu. Wazazi tu ndo jambo la pamoja
Huyu NI Mimi mtupuuuu
 
huyu jamaa ni kweli tulimkabidhi dada yetu kifamilia, lakini baada ya miezi 6 kupita kuwasiliana adi tumpigie sisi, na sisi tumeamua hatutomtafuta akijisikia sawa tu, jengine bado hajamalizia mahari, kuhus maisha wanaishi vizuri na dada yetu ila sina uhakika 100%.nyie vijana acheni zadhau, tu nampigia tu dada yetu. yeye no.
Kwa nini unamtafuta?
 
Toa mwongozo. Mawasiliano yanapaswa yaweje?

Wewe unawasiliana vipi na wakwe zako?
 
Back
Top Bottom