Jamaa yangu ananitesa kisa alinitafutia kazi, ni haki?


Kimsingi ameekuunganishia kazi japo ulisha soma na unaujuzi wako tayari hivyo sio kwamba amekusaidia kila kitu.
Kosa ulilofanya ni kuongozana naye baa. Anza kupunguza mitoko ya kwenda baa; Jitahidi utoke naye vikao rasmi huku ukipunguza mazoea taratibu, lakini akiwa na shida msaidie kadri unavyoweza.

Kwa watu wenye Uroho kama hao; Ukipata mshahara (kama anaujua) unampa nusu yake kabisa unamwambia umempa kama shukrani ya kukusaidia kupata kazi. Wengine hutoa mshahara mzima (mmoja) ila baada ya hapo hamjuani tena. Ila nenda taratibu hasa kama ananafasi ya kukuharibia
 
Kwan lazima utoke naye?,lazima mfatane fatane?.
 
Jitengenezee CV nzuri kazini,kwa kufanya kazi kwa bidii,nidhamu&ubunifu.
Kisha weka mipaka kati yenu,akikukataa mkatae mazima.
 
Huyo hajaujua mji vzuri, anadhani wanaokesha kwa waganga au kwa mwomposa wanafanya hvo kwa kupenda.
Ye si atheist
Ss akae Kwa kutulia ndo atajua Kuna Mungu na miungu na huo u atheist utamuisha atachagua upande,🀣
 
mkate chap we endelea na mambo yako acha mzoea atakuja kukut…mbea hata mke huyo usipoangalia
 

chagua urudi msoto au Ulipe fadhila!!

Kama we mwanaume tafuta kazi nyingine hapo utakua umemuonesha kwamba naww yy si chochote ila kama huwezi bas kubali kulipa fadhila
 

Kwenye kutoka out unajitakia mwenyewe!!

Kwan lazima !!
Waweza kua unakwepa kwenda out
 
Pole sana
 
wewe achana na watu bhana kila mtu na maisha yake hata ukiacha kazi atasema nimemtaftia kazi kashindwa we mkatae kama anaweza akunyang'anye iyo kazi yeye sio Mungu rizki yako ipo tu
 
Paying the goodwill has known no end. Bila huyo jamaa usingekuwa na hii mada. Sisi wengine mbona tunaendelea kulipa fadhila kwa miaka sasa ingawa si kwa pesa ya kila mwezi. Ila siku ukijipata unamkumbuka mtu aliyekufanya uwe hapo ulipo.
Onesha ukomavu wa maisha.
 
Believe me... Hakuwahi kufanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…