Tanzania kweli ni nchi ya kipekee sana kwa ujinga, wakati wapo waliotayari kupata chanjo ila serikali imewaambia wasubiri mpaka december, kama vile na Corona nayo itawasubiri, halafu wako wale wengine wasio na habari ya chanjo kabisa, hapo utaona watanzania wote tupo kwenye hatari ya kuugua Corona.
Wakati Corona inasumbua mataifa mengine, utashangaa wapo watakaoibuka kuipinga hii kauli ya Mbatia, ataambiwa anatafuta sifa za kisiasa, utadhani Tanzania haipo kwenye ramani ya dunia, wakati hata madaktari wakiongea kuhusu Corona, nao wanawapinga, sasa sijui wao wanataka nani wengine waongee kuhusu Corona, bado kama taifa tunazunguka mbuyu tu.