James Rugemalira aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka

James Rugemalira aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka

"China Mafisadi wanadhibiwa, huku Mafisadi wamekuwa kama Inspiration....."

Maneno ya mlevi mmoja alisikika akisema, baada ya hapo akamalizia "Mtanikumbuka...............".

Hapo ndipo nami nikagundua tuna safari ndefu sana kukijenga kuzazi chenye uchungu, uzalendo na uaminifu kwa taifa hili kwa manufaa ya kizazi kijacho, yaani unashangaa mpaka wale waliomponda kwa miaka mitano mfululizo kwenye majukwaa na kwenye magazeti yao ya kwamba mwizi, leo wanadai alionewa. Kweli yule mlevi alikuwa sawa "MTANIKUMBUKA "
Na sisi tumekataa kumkumbuka huyo mlevi mbwa
 
Unajua remote ya nchi nayo ilihusika katika mchongo huo hivyo ni lazima aachiwe huru kwa maamuzi ya remote ya nchi yetu ya Tanzania.
Aisee nyie mabeberu mna maneno.....
Remote ya nchi ndio Nini 😂😂
 
Ndio nimejifunza kuacha mafisadi wafisadi mpaka kiwango cha 5G, kumbe tunapenda kupigwa kiasi hiki! Aliyenacho ataongezewa mara dufu hata kwa kuiba.
Mahakama imemuachia alafu wewe unamwita fisadi, je una ushahidi wa huo ufisadi?
 
Salaam Wakuu,

Leo nimepita maeneo ya Mahakama ya Kisutu, Nikakuta Mkurugenzi wa kampuni ya VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira anatabasamu akiwa na ndugu zake wakipeana hugs na kuchumiana. Inaashilia kuna dalili nzuri leo Mzee wa Henken akaliona jua. Langu Dua.

_MG_0435.JPG
James Rugemalila(Kulia) na mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Harbinder Seth Sigh(Kushoto), wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi kabla ya kupanda kizimbani Mahakamani Kisutu Jijini Dar.

Tarehe 19 Jun, 2017 TAKUKURU wawafikisha mahakamani Seth Na Rugemalila kwa uhujumi uchumi. walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu wakishtakiwa kwa makosa sita ya uhujumu uchumi, likiwamo la kuisababisha Serikali hasara ya jumla ya takriban Sh358 bilioni.

Wakili wa Serikali, Paul Kadushi aliyataja mashtaka mengine yanayowakabili wawili hao kuwa ni kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na kuisababishia hasara Serikali.

Zaidi Soma:

1). TAKUKURU yawafikisha mahakamani Harbinder Sethi na James Rugemalira kwa kosa la Uhujumu uchumi

UPDATE:

Rugemalila yupo huru!

Mashtaka yake yameondolewa chini ya kifungu cha 91(1) cha Mwanendo wa Makosa ya Jinai

Jamaa amesimamia alichokiamini hadi mwisho,kwamba ikibidi afe kwa sababu hakuna atakaedumu.. hongera zake
 
Naamini hata Sabaya atakutwa hana hatia na wabongo tutashangilia.
 
Kamuombe akugawie! Nyinyi vichwa panzi kazi kutetea wezi wakati wewe huna hata baiskeli!
Mbona alishanigawia na sasa tunasheherekea kutoka kwake jela

Nyie vichwa sisimizi wenye roho ya kwanini endeleeni kuona wivu
 
Be serious. Wizi huo unahusisha serikali na mkubwa ana mkono mzito kwenye misheni hiyo. Unategemea nini? Kwa serikali ya CCM kusema inapambana na ufisadi ni UNAFIKI wa hali ya juu. Hakuna ufisadi mkubwa wa kiwango hicho unaoweza kufanikiwa bila "signecha" ya mkuu mwenyewe.

Baada ya kushindwa kushughulika na mkuu wa awamu ya iliyopita, mwendazake kavamia kina Ruge akitarajia wamgawie pasenti ya mshiko wa "wizi". Where is the moral high ground with these people? Ndio maana wanaishia kudhalilika kwa roho zao mbaya. Mkuu wa sasa kaondoa "nadhiri" ndio unasikia DPP akidai eti "sina nia"! kirahisi rahisi tu! Sijui wanapata wapi amani ya roho watu hawa?
Mkuu hi kesi wapinzan wakina Lissu nawenzie si ndio waliitolea macho na kushikilia kidete pale bungeni mpka kutoa maamuzi hayo Sasa Magu kosa lake ni lipi maana yet alitekeleza vile bunge lilivyotaka
 
Wandugu

Huyu mzee Rugemalira leo hataweza kulala kwenye godoro. Kila akijaribu kulala atakuwa anaona kama anazama ndani ya godoro.

Hii hali ni kutokana kashazoea kulala kwenye kitu kigumu/sakafu kwa miaka minne. Hivyo basi mke na wanafamilia wasije huzunika kuona mzee wao anakataa kulala kwenye godoro, wajue hio ni hali ya kawaida.

Itachukua mda akili yake kujiadjust kupokea mazingira mapya.

Sijajua ukweli nachoweza kusema huyu mzee Rugemalira amekuwa mfano mzuri katika philosophy za Ustoic.

Misingi mikuu hii philosophy inafundisha ni juu ya kutambua mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu na mambo yalio njee.

Mzee alitambua mapema kukubali au kukataa mashtaka yapo ndani ya uwezo wake na kufungwa, kuabishwa kupo nje ya uwezo wake, hali kadhalika watesi wake waliweza kumweka ndani na kushindwa kupata tubu yake.

Yapo mengi ya kujifunza na hakuna wa kulaumu katika hizi pande mbili kinzani kwani ubora wa Rugemalira unatokana pia na ubora katika kutenda hayo kinyume na haki kwa watesi wake.

Alamsiki
 
Bro unajidanganya sana.

Jela pia kuna VIP. Yeye alikuwa akilala sehemu safi, zisizo na msongamano.

Usiku wake ni wa kawaida tu.
 
Bro unajidanganya sana.

Jela pia kuna VIP. Yeye alikuwa akilala sehemu safi, zisizo na msongamano.

Usiku wake ni wa kawaida tu.
Naskia kuna wakati alikuwa akipewa uhuru wa kuwa na mkewe faragha hapohapo gerezani
 
Back
Top Bottom