James Rugemalira aachiwa huru, DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka


Ushahidi tosha ya udhalimu wa Mwendakuzimu na udhaifu wa mfumo wa kusimamia haki nchini ni huu hapa.

Yaani ng’ombe mmoja aliyetokea Chato aliweza kuvifanya vyombo vyetu vitende kila alichokitaka yeye bila kujali wapo sahihi au la!

Popote alipo huyo ng’ombe afe tena.
 
Hii Tz ina matabaka, wanasiasa hawakufungwa kabisa lkn luge na mwenzake wamesota balaa
 
Mkuu hi kesi wapinzan wakina Lissu nawenzie si ndio waliitolea macho na kushikilia kidete pale bungeni mpka kutoa maamuzi hayo Sasa Magu kosa lake ni lipi maana yet alitekeleza vile bunge lilivyotaka
Kina Lissu walitaka kesi iendeshwe na uamuzi wa mahakama upatikane kwa wote waliohusika. Sio kukamata watu wawili, watatu na kuwaweka ndani indefinitely. Kosa la Magufuli ni kutoruhusu mahakama ifanye kazi yake na, badala yake, kumtuma DPP kujadiliana plea bargain ili kujipatia mgao wa ufisadi jambo ambalo limeacha mafisadi kutochukuliwa hatua stahiki za kisheria.

Usifikiri akina Lissu walikuwa wanawaonea huruma kina Ruge na Singa. La. Walitaka ukweli ujulikane kupitia mahakama na wote waliohusika wachukuliwe hatua. Serikali za JK na Magu hazikuwa tayari kutokana na "unyeti" wa suala hilo kwao.
 
Haki imeshinda. Mara baada ya kuachiliwa huru, ameenda kanisani kusali na kumshukuru Mungu. Alimwachia kila kitu Mungu, akabaki na rozari yake shingoni and he would say it daily. Hata sasa Mungu amemsaidia.
 
Reactions: Qwy
Kweli nchi ilikuwa inaendeshwa mjinga wa mihemko ya kijingajinga...
Yule mfu hata angekuwa anapumulia machine angelazimisha kesi iendelee na mahakama yake ya kipuuzi ya miaka ya 80 ya uhujumu uchumi
Karudisha nchi nyuma sana mpaka dunia imesahau kuna nchi inaitwa Tanzania....
 
Reactions: Qwy
Wewe inaonekana ni mtoto wa fisadi, ndio maana una chuki na Magufuri.Magufuri amewaenyesha Mpaka kiburi kikawaisha,zile zama za unanijua me nani alizikomesha, kipindi cha Magufuri Mafisadi wameionja joto ya jiwe,huyo Lugemarila wenu hawezi kurudia mchezo wake wa kuchora madili ya kuibia serikali tena.
 
Ndio sisi mafisadi tumeshirikiana mabeberu kumchapa na covid...
Ameshakufa huyo hafufuki....
Kwisha habari yake.....
 
Ndio sisi mafisadi tumeshirikiana mabeberu kumchapa na covid...
Ameshakufa huyo hafufuki....
Kwisha habari yake.....
Hata Wewe nawe siku yako ya kufa itafika,tena utakufa kifo kibaya, akuna mtu atakeyetamani kuona maiti yako
 
Mafisadi wanazidi kujikusanya na kufufua team yao chini ya mama samia the killer one
Tafuta pesa, wivu wa kimasikini utakufanya uishi maisha ya kifukara huku ukilialia na kumuita kila aliyefanikiwa fisadi. Upumbavu na wivu wa kishamba wa Jiwe umfuate huko huko kaburini kwake. Narudia tena, tafuta pesa.
 
Mafisadi wanazidi kujikusanya na kufufua team yao chini ya mama samia the killer one
Huwezi kumfunga Lugemalila ukamuacha Kikwete , ile ilikuwa uonevu , yeye alikuwa mwakilishi wa VIP , nani aliyeleta IPTL , kwanini aliachwa ?
 
Kipindi cha Jiwe 'unajua mie nani' ndipo ilikithiri kutoka kwa 'wasiojulikana', sasa raia at least wanapumua na Rugemalira yuko huru na biashara zake zitaendelea kama ilivyokuwa awali. Wenye vijiba vya roho shauri zao.
 
Kuna watu walikufa kwa kukosa madawa hospital,wamama walikosa vitanda vya kujifungulia wakati mke wake akijifungulia Marekani, watoto walikosa madawati,wakati wakwakwe akipeleka Ulaya,acha akomeshwe, sasahivi awezi rudia dili zake za kuibia serikali
Wale wanasiasa walioshirikiana nae kupiga Mbona hawajakomeshwa Sasa
Ukiambiwa katiba mpya ccm hamtaki. Mnataka hii ya kimagumashi inayoruhusu dpp kumfunga ama kumuachia mtu vile anavyojisikia
 
Reactions: Qwy
Imagine, angefanya alivofanya Harbinder watu wangesema haki imetendeka ila sasa wanajua kuwa nchi hii unaweza kaa gerezani muda wwt visivo halali. Maana hata ile ya ku.kamata na kumfunglia shitaka upya, wamegwaya. Ndo ujue DPP anaposema wanatenda "Haki", wanachomaanisha ndo hicho! Miaka 4 "Upelelezi Haujakamilika", lakini lipa utoke, halafu yanaishia hapo - bila kujali ikiwa atadai fidia italipwa na nani, Za kodi au za mfukoni! Wanachezea maisha ya watu kutokana na madaraka yao, hawajali. Kila kitu kina mwisho
Jambo la kheri, yeye aligoma kabisa kukiri kosa na kulipa fidia?
 
JK alituambia zile hela ni mali ya IPTL tukamuoma mjinga na kumnanga kila kona...

Ni ngumu sana kuwaelewa watanzania na Tanzania juu ya haya yanayotokea, nafikiri hata dunia kuna mahala inatuona ni species tofauti..

tulipiga sana kelele JK alipoacha kuchukua hatua juu ya Ruge na Singasinga, tukamuita dhaifu na zihaka nyingi sana...Wanasiasa wetu tunaowashabikia wakashupaza shingo bungeni,, Hatimaye JPM akasikia kilio na kuwatia mkononi Singa na Ruge, Watanzania walewale wakamuita JPM dikteta na leo wanashangilia Ruge kuachiwa na kumdhiki marehemu JPM...

Kwa akili hizi ni bora CCM ikaendelea kutawala miaka mingine 300 labda kitakuja kizazi kinachojielewa...
 
Mama akileta Tozo tuache kulialia..maana hawa wote wanaotoka wanaweza kuishitaki serikali na kudai mabilioni ya fidia...Serikali itabidi itukamue kufidia hizo fidia....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…