Ni wanafki tu.
Wengine wanajifanya atheists kumbe ni wakatoliki.
Kazi kuuponda uislamu tu huku wakiutupia ukristo mara moja moja kuficha ajenda zao za siri.
Halafu walivyo wanafki muislamu akiamua kufuata misingi ya dini yake kikamilifu anaonekana hafai atasemwa na kubezwa akipotoka kama hao watoto pia uislamu utabagazwa.
Both ways uislamu unabagazwa.
Tunawachora tu ma atheist wa uongo kina
Yoda
Tushawazoea hawa. Shida yao ni Uislam na Waislam. Inasikitisha sana Muislam akilegeza msimamo katika Dini yake ili kuwafurahisha hawa na kutaka ku fit in na kufuata matamanio yao. Hajui kuwa hawa shida yao kubwa kabisa ni yeye kuwa Muislam. Na wanachukia yeye akiwa Muislam hata kama watafurahi kidogo kwa yeye kulegea katika Dini ila bado watamchukia na hawatoridhika mpaka wamtoe katika Uislam kabisa.
Hivyo hata kama Muislam ni dhaifu katika Dini yake na anazembea katika baadhi ya maamrisho na kuyafanya baadhi ya makatazo, bado hawako radhi naye mpaka afuate mila yao.
Ndio maana Muislam akisimama sawa katika Dini yake watamchukia na hata akistruggle au akawa kuna maasi atayafanya baadhi yao watatumia hiyo image kuutukana Uislam na Waislam, kwa sababu chuki yao hasa ni kwa Uislam na Waislam, wanamchukia mno bado.
Hivyo Waislam, tukae chini, tusome Dini yetu, tuifuate na tushikamane nayo barabara, tumche Mola wetu Mlezi, tumuabudu Allah Peke yake Bila ya kumshirikisha na chochote kile na tuwe na Subra katika kumuabudu na tuwe na msimamo, tuepuke shirki, tufuate Sunnah na kuepuka uzushi katika Dini na tujitahidi kufuata Maamrisho ya Allah na Mtume wake na tujitahidi kuacha Makatazo yao na tutubie kwa Allah pale tunapoteleza.
Tuishike Dini yetu na wala tusiogope lawama za wenye kulaumu, na wala tusifuate matamanio, bali tumtii Allah na Mtume wake.
Kuwa proud na Neema hii ya Uislam na wala usiwe mnyonge, usijali maneno ya watu ambao hawatokusaidia lolote lile, hawakupi Rizq, ni Allah Pekee Ndie Anatoa Rizq, wala hawakupi uhai wala pumzi, ni Allah Pekee Ndiye kakuumba na Ndiye Anayekulea na Kukuruzuku na Kukupa Uhai na Pumzi, na Akhera hao watu hawatokusaidia chochote kile. Usijali maneno yao ya kejeli wala kuvunja moyo, Uislam ndio Rasilimali yetu kubwa. Uislam ni NEEMA KUBWA kuliko zote alizokupa Allah, hivyo mshukuru Allah kwa wewe kuwa Muislam.
Ninamshukuru Allah kwa Neema ya Uislam na Sunnah.
Wallahi ninawapenda mno Ndugu zangu Waislam kwa ajili ya Allah.
Ninamuomba Allah kwa Majina yake Matukufu Atusamehe Waislam madhambi yetu na Atuongoze na Atuhifadhi na Atutibu Maradhi yetu na Atusaidie katika kumtii Yeye na Atusaidie kuepuka Makatazo yake na Atusaidie katika Jihaad tunayopigana na nafsi zetu (ni struggle kubwa mno) na Atupe Mwisho Mwema, Atufishe katika Uislam, Atufishe katika Tawheed na Sunnah, Allahumma Aamiin.