Jana ulikuwa ni mkutano wa CCM uliovalishwa vazi la CHADEMA

Lakini kumsifia hasimu wako Mbele ya Mkeo na wanao Huko sio kuanza taratibu Mkuu.

Haikupaswa kivyovyote Chadema kuisifia CCM.
Tactic ya kumsifia mtu ni kubwa sana wengi wameangamizwa kwa ujanja huu. Hizo ndio busara za siasa za Tanzania na hata Samia mwenyewe anaelewa nini maana ya “kusifiwa” na Mbowe. Mbowe asingekuwa na busara za kisiasa kwa hakika Magufuli angelisha mmaliza siku nyingi! Ujue Magufuli alimchukia Lissu lakini alimwogopa Mbowe.
 
Hizo ndio busara za siasa za Tanzania na hata Samia mwenyewe anaelewa nini maana ya “kusifiwa” na Mbowe. Mbowe asingekuwa na busara za kisiasa kwa hakika Magufuli angelisha mmaliza siku nyingi!

Sasa hapo ndio ataiua Chadema mioyoni mwa Watu.
Wanachadema wa Chini wanaamini CCM ni adui Yao. Sasa unaposhirikiana na adui yao, lazima wakuone Msaliti. Rejea 2015 Wakati WA Lowasa.

CCM inachokifanya sasa ni kumpa mtoto mchawi. Watakuwa wamejipunguzia mzigo.

Chadema ambacho wangefanya Kwa sasa ni kubali na agenda Yao ileile ya kupigana na mafisadi, kisha kuwashawishi team magufuli wawe upande wao.

Sasa wakiungana na ccm, watapoteza uungwaji mkono na watu.
Alafu CCM wao kazi Yao itakuwa kuwabembeleza kirahisi wananchi
 
Sina hakika kama ndio aliyeimaliza, bali nina uhakika aliharibu sana haiba ya CDM. Lile lilikuwa ni kosa la karne.

Aliiharibu Kwa sababu Wananchi wengi walishaanza kuiamini Chadema.
2015 wangemuacha Slaa hata kama asingepata Kura nyingi lakini ingezidisha Imani ya Watu ndani ya chama.
 
Siasa za nchi hii ukihangaika kuzifuatilia utaumia kichwa, wanasiasa ni wafanya biashara kama wafanya biashara wengine. Masilahi ya tumbo yapo mbele.

Kama unasubiri wanasiasa wakutatulie shida zako, basi utasubiri sana... huu ni wakati wa mwenyekiti kurudisha biashara zake na utajiri wake. Umri alionao saizi anahitaji kupata assurance ya miaka 20 ijayo, akipiga hesabu vizuri huu ndio muda wa kuweka pride pembeni na kuumega mkate.
 
Aliyeidhuru CDM sio Lowassa ni Magufuli akitumia ukabila na dola.

Magufuli hakuidhuru Chadema Kwa kiasi kikubwa, labda katika umbo la nje.
Lakini Kwa umbo la ndani Chadema walijidhuru wenyewe pale walipoanza kutetereka kwenye msimamo. Hasa walipomkaribisha Lowasa
 

😂😂😂😂
Usiseme hivyo mkuu
 
Mbowe ni mwanasiasa makini. Hata CCM tutaanza kutumia ile hashtag ya #mwambatuvushe. Jana Mbowe alifanya kitu kikubwa sana kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi. Ninaomba Mbowe ataeuliwe hata kuwa mwenyekiti wa bodi ya parole kama itampendeza Mama Samia.
 
Mbowe ni mwanasiasa makini. Hata CCM tutaanza kutumia ile hashtag ya #mwambatuvushe. Jana Mbowe alifanya kitu kikubwa sana kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi. Ninaomba Mbowe ataeuliwe hata kuwa mwenyekiti wa bodi ya parole kama itampendeza Mama Samia.

Aiseeeh!
 
Ni kweli Ana data za kutosha namna wale Wana madini wawekezaji watakavyoipeleka mahakamani Serikali sababu ya makinikia..sure..!!
 
Sawa Robert kumbuka CDM imepitia magumu mengi mno hata mimi nashangaa kwamba CDM bado ipo. Pia kwanini watu wanai-judge CDM kwa mkutano mmoja tu wa jana ilhali ipo mikutano kibao inafuata? Mambo CDM wanataka kuyafanya ni process na sio tukio moja. Naogopa atakapokuja Lissu tutamwomba apoe kidogo kwani kama alimpa za uso Magufuli sijui itakuwaje kwa mama. Na Lissu ana machungu mengi, itabidi busara kubwa itumike. Ni hatari kweli kuwa mpinzani Africa especially of the kind of Lissu.
 

Umesema vizuri Kabisa.
Hofu yangu ni Ile ya kutaka kuibomoa katika umbo la ndani Kabisa.
Chadema isingekufa kivyovyote Kwa mbinu alizokuwa anatumia Magufuli, kwani yeye alijikita kupasua Kwa nje Kwa Kutumia nguvu kubwa.
Ilhali ukitaka kukiharibu kitu totally unatakiwa kukiangamiza Kwa ndani.

Watu wakishapoteza Imani na Chadema kurudi ni kipengele.
 

Siasa za Lisu ni zahatari lakini zinaeleweka zaidi kuliko Siasa za kina Mbowe na zitto.

Wakitokea kina Lisu kama 10 hivi ndani wanawawe kuleta matokeo yanayotarajiwa ndani ya muda mfupi.

Ila Kwa Afrika ni ngumu Sana
 
Lissu na yeye tunamsubiri akija atapita mle mle amsifie mama samia na hapo sjui ntamsubir nan tena , ukweli ni kuwa chadema ushawishi hamna
 
Kuandika hivi umeona fahari, lakini wakati Mbowe mali zake zinaharibiwa na yeye kuwekwa ndani kwa miezi mingi, je, hao Wana CHADEMA walifanya nini kupinga? Mikutano ilivyozuiwa Wana CHADEMA walifanya nini kupinga? Baada ya Rais Samia angalao kurudisha Uhuru wa kisiasa, ni hoja ya msingi kwa Mhe. Mbowe kushukuru kwa kilichofanyika Kama utangulizi. Hatupaswi kurusha lawama Kama hizi wakati wana Chadema hawakuweza hata Kutoka barabarani kupinga ukiwemo wewe mtoa mada. Je mapambano ya kudai haki ni ya mtu mmoja?
 
Magufuli hakuidhuru Chadema Kwa kiasi kikubwa, labda katika umbo la nje.
Lakini Kwa umbo la ndani Chadema walijidhuru wenyewe pale walipoanza kutetereka kwenye msimamo. Hasa walipomkaribisha Lowasa
Hakuna boost kubwa kwa CDM kama tukio la Lowassa kugombea kupitia CDM! Ukweli ni kwamba CCM walitetemeka kwa hofu kwani Lowassa alikuja na timu yake na kwa mara ya kwanza ushindani mkubwa kwenye kampeni ulionekana, watu hawakuona tofauti kubwa ya “mafuriko” ya watu kati ya vyama hivi. Ila CCM hawakuwa tayari kuachia madaraka. Unajua yote yaliyotokea wakati wa Magufuli vs Lissu, CCM ilikuwa idondoke ila Magufuli alifanya yote aliyofanya bila chembe ya aibu.
 
Basi sawa, lakini mleta hoja nadhani anayo hoja ya msingi.

Yesterday it was a "missed opportunity." Kila mmoja akikaa akatafakari moyoni analithibitisha hilo.

..mimi nadhani vyama vingine vya upinzani vifanyie kazi mapungufu yaliyoonyeshwa na Chadema.

..Mikutano ya hadhara imefunguliwa sasa ni muda wa kila chama kutumia fursa hiyo kujitambulisha kwa wananchi na kuelezea sera zao.

..Mwisho wa siku tuelewe kwamba hakuna chama ambacho hakina mapungufu. Na kila mwanasiasa ana mazuri yake, na mapungufu vilevile.
 
Robert Magufuli alifanya mauaji ya CDM nje na ndani. Nje: kwa kuuwa mfumo wa siasa za upinzani e.g. kuzuia mikutano na hata ruzuku za vyama. Ndani: alitargeti watu binafsi kama kina Mbowe kwa kuwafilisi na Pia wafanyabiashara waliodhaniwa kuisapoti CDM walikiona. Lililokusudiwa kwa Lissu lengo lake linajulikana ni kuwamaliza CDM kisaikolojia kwa hofu. Ni viongozi wangapi CDM walurubuniwa kwa fedha na vyeo? Alijitahidi kuua ndani na nje kwa nguvu zote.
 

..nadhani kauli yako ni ya kuwakandamiza wanaChadema.

..kuna wanachama na wafuasi zaidi ya 400 waliotiwa magerezani na mahabusu wakati wa Jpm kwasababu ya kuitetea Chadema na kusimamia haki.

..Ni kweli hakuna mwana Chadema aliyeingia barabarani, lakini wapo wengi waliotumia njia za AMANI kudai na kutetea haki na utawala wa sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…