Jana ulikuwa ni mkutano wa CCM uliovalishwa vazi la CHADEMA

Kosa la CHADEMA ni kutofuata katiba ya chama chao. Mwenyekiti Mbowe huwa akiamua ndo tayari inakuwa bila kupitia vikao halali vya chama. CCM wataendelea kuutumia huo udhaifu wao wa kutoheshimu katiba yao wenyewe.
 
Aliiharibu Kwa sababu Wananchi wengi walishaanza kuiamini Chadema.
2015 wangemuacha Slaa hata kama asingepata Kura nyingi lakini ingezidisha Imani ya Watu ndani ya chama.

Hilo ni sahihi, Slaa alikuwa na uwezo na ushawishi kuliko Lowassa, na CDM ingepata kura nyingi kuliko ilizopata kwa kuwa na Lowassa, na hata kama wasingepata urais, bado haiba ya CDM ingebaki palepale.
 

Kama ulikuwa mkutano wa CCM unapiga kelele za Nini?. Mbowe kakiri wanachadema wanampinga halafu unakuja kudai ulikuwa mkutano wa CCM . Endeleeni kujifariji.
 
Umeandika mambo mengi Lin pointless tuu. Mbowe Ni mwanasiasa nguli anajua anachokifanya, na anajua anataka nn kutoka kwa watawala, na amejifunza nn toka kwa watawala. Hakuna siasa nchi ambazo mbowe hajafanya. Inawezekana kajifunza namna gani ya kwenda sawa na watawala Kama una ajenda yako mkononi inayoitaji nguvu ya watawala kuifanikisha.
 
Mwenyekiti alihutubia akiwa vyombo tusubiri tamko la kuomba radhi
 
Haikuwa Kete nzuri Kwa kweli, Lowasa ndiye aliyeimaliza chadema,

Lowassa aliimalizaje CHADEMA?. CHADEMA iliopata kura asilimia arobaini. Kitendo Cha kuzuia mikutano na kuwashambulia Viongozi wa CHADEMA ndicho kilichoharibu siasa za CHADEMA. CHADEMA haijamalizwa bado ipo intact.
 


Hiyo Ni imagination yako. Pamoja na kauli ya Mbowe bado Bunda na Lamadi watu wamejitokeza kwa wingi na Musoma Pia. Usiichukulie CHADEMA kikawaida.
 

Kuielewa Chadema au Mbowe hakujawahi kuwa rahisi hivyo mjomba. Hii ni kwenye nutshell ndugu:



Ninakazia chenga ya mwili ya Mbowe imewachuuza wote waliomo na hata wasiokuwamo.

Zingatia adui yako akikusifia ujue fika umeuvaa mkenge!
 
Amlipaye mpiga zumari ndiye huchagua wimbo.
 
Magufuli hakuidhuru Chadema Kwa kiasi kikubwa, labda katika umbo la nje.
Lakini Kwa umbo la ndani Chadema walijidhuru wenyewe pale walipoanza kutetereka kwenye msimamo. Hasa walipomkaribisha Lowasa

Acha uongo eti Magufuli hakuidhuru CHADEMA. Usiwe mnafiki. Kama Magufuli asingezuia mikutano baada ya ule uchaguzi na kuwarubuni Viongozi wa CHADEMA wasiojielewa unadhani Hali ingekuwaje. Nakumbuka Lowassa alikamatwa Mpanda akienda kufanya mkutano wa kuwashukuru wananchi.

CHADEMA iliungwa mkono Sana pamoja na Lowassa kuwepo. Uchaguzi ambao utabiri ulikuwa mgumu Sana kujua Mshindi Nani, mpaka Tume ilipoleta ujinga.
 

Nadhani amejifunza siku nyingine ataleta porojo Kama za Jana. Watu tumefunga Safari mpaka Mwanza halafu mambo Kama. Ilitakiwa iwe Kama Musoma leo.
 
Kuna wajinga wapo chadema wanaamini wapo kwenye harakati kumbe ni kumsindikiza mbowe kulamba asali

Wajinga gani?. Wakati Mbowe kakiri ana upinzani ndani ya chama. Unapoongea jaribu kuwa mkweli
 
Siku za nyuma nilikuwa naheshimu sana michango yako.Lakini siku hizi umekuwa mweupe sana .....nadhani huna principles!
 
Kwani yeye ndio wa kwanza kukaa jela?
Walikaa akina mandela et al, na bado walibaki na msimamo wao. Siasa za nchi hii ni against a person and not a system! Wao walimchukia mtu, hawakuchukia mfumo

Huyo mtu ndiye aliyeanza kuwachukia CHADEMA, na CHADEMA wakamchukia pia. Usiongee kwa upande mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…