HOJA Janga la Mashoga Mitaani na kwenye Familia... Kwanini Serikali na Jamii wanafumbia Macho?

HOJA Janga la Mashoga Mitaani na kwenye Familia... Kwanini Serikali na Jamii wanafumbia Macho?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Huwezi kuona shida ya ushoga mpaka siku wamfanyie mtoto wako au ndugu yako yeyote awe shoga.
Ni uongo, hakuna mtu anayefanywa kuwa shoga na mwenzake, watu wanakuwa mashoga wao binafsi. Mtoto wako au ndugu yako kama ni shoga atakuwa shoga tu hata kwa kuwatafuta mwenyewe mashoga wenzake kama hawapo karibu.

Huwa sikubaliani hata na suala la kusema wanawake ndio wanawatamanisha wanaume na kusababisha ubakaji kwa hiyo wanawake wajifunike gubigubi.
 
Ni uongo, hakuna mtu anayefanywa kuwa shoga na mwenzake, watu wanakuwa mashoga wao binafsi. Ni sawa na kusema wanawake

Huwa sikubaliani hata na suala la kusema wanawake ndio wanawatamanisha wanaume na kusababisha ubakaji kwa hiyo wanawake wajifunike gubigubi.
Huonagi kesi za wababa kuwaingilia watoto wa kiume chini ya miaka 18?
Ushoga ni sawa kama mtu atafanya hilo jambo kwa siri chumbani kwake ila wanaoharibu ni wale wanaofanya hadharani na kuwaingiza hadi watoto wadogo.
 
Ni kosa kisheria mtu mzima kufanya mapenzi na watoto wadogo au wanafunzi hata wa kike.

Huu mjadala unahusu watu wazima walioridhiana wenyewe kuwa mashoga kwa nini iwe jinai/ criminal kwao.
 
"Huwezi kuona shida ya ushoga mpaka siku wamfanyie mtoto wako au ndugu yako yeyote awe shoga"

Kwa Hiyo wanao ona shida tayari watoto wao wamefanyiwa hivyo vitendo?

Nimejaribu kuwaza tu hii sentensi🤔
Kwa yanayoendelea mitandaoni mashoga kupigia debe ushoga waziwazi kabla hata mtoto wako hajafanyiwa lazima roho ikuume na kuchukia ushoga
 
"Huwezi kuona shida ya ushoga mpaka siku wamfanyie mtoto wako au ndugu yako yeyote awe shoga"

Kwa Hiyo wanao ona shida tayari watoto wao wamefanyiwa hivyo vitendo?

Nimejaribu kuwaza tu hii sentensi🤔
Nina uhakika wanotokwa na povu wengi hapa kuhusu ushoga zaidi ya 90% hawajawahi hata kukutana na shoga mmoja hata wa mbali tu zaidi ni kusikia tu habari za mtandaoni.
 
Kwa yanayoendelea mitandaoni mashoga kupigia debe ushoga waziwazi kabla hata mtoto wako hajafanyiwa lazima roho ikuume na kuchukia ushoga
Mzuie mtoto wako asiingie mtandaoni na kwenye porn sites.

Usinunue kisumbuzi cha DSTV, nunua cha Azam tu.
 
Kwa yanayoendelea mitandaoni mashoga kupigia debe ushoga waziwazi kabla hata mtoto wako hajafanyiwa lazima roho ikuume na kuchukia ushoga
Mimi sitaki kuwajadil hao watu , hawana faida yoyote wala hasara kwangu , najadili muundo wa sentensi yako tu , just kiswahili tu
 
"Huwezi kuona shida ya ushoga mpaka siku wamfanyie mtoto wako au ndugu yako yeyote awe shoga"

Kwa Hiyo wanao ona shida tayari watoto wao wamefanyiwa hivyo vitendo?

Nimejaribu kuwaza tu hii sentensi🤔
Kwa nini watu wanachanganya hoja ya ushoga na mambo ya watoto?

Kwenye watoto, hawaoni kuwa mambo yoyote ya kuwa sexualize watoto ni tatizo, bila kujali mambo hayo ni ushoga au si ushoga?

Hao wanaolalamikia ushoga kwa watoto, ina maana tatizo lao ni ushoga kwa watoto, watoto wao wakibakwa na mtu wa jinsia tofautina mtoto, bila ushoga, watakuwa hawana tatizo kwa sababu huo si ushoga?

Mbona hapo mimi naona tatizo ni sexualization kwa watoto tu, si ushoga, na mtu akileta hoja ya ushoga kwa watoto hapo namuona ana tatizo na ushoga tu anatumia watoto kuwaandama mashoga tu.
 
Si kila mtu anaamini katika mila, desturi na dini yako.

Jifunze kuishi kwa kuelewa kuwa kuna watu tofauti na wewe, na wao wana haki kuishi wanavyotaka wao.

Fikiria kwamba upo katika dunia ambayo mashoga ni wengi halafu wasio mashoga ni wachache.

Halafu wale mashoga wengi wanawaandama, wanawaua, wanawalazimisha muwe mashoga.

Ungejisikiaje?
Kwa sasa haipo hivyo twende na lililopo
 
Hapana, mimi si shoga, na wala sihitaji kuwa shoga kutambua haki za binadamu.

Wewe kufikiri mtu kutetea haki za binadamu za mashoga ni lazima awe shoga, ni ukosefu wa uelewa tu.

Yani umeshindwa kufanya fikra dhahania (abstract thinking).

Umeshindwa kujua kuwa, hata mzungu anayethamini haki za binadamu, asiyependa ubaguzi, anaweza kuchukia ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi bila ya yeye kuwa mweusi.

Katika mawazo yako umeona ili mtu apinge ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi, ni lazima awe mweusi.

Hii ni hoja potofu. Inaonesha udogo wa fikra.

Inaonesha huijui dunia tu.
Mkuu shoga sio binadamu binadamu wana jinsia mbili kwahio ukiongelea binadamu shoga hayumo
 
Kwa sasa haipo hivyo twende na lililopo
Lakini hujajibu hoja.

Kwa sasa ipo hivyo kwa mashoga. Haipo hivyo kwako tu.

Ukisema kwa sasa haipo hivyo unaonesha ubinafsi wako, unawaona mashoga hawana haki wewe tu ndiye una haki.

Na hili ni tatizo kubwa sana Tanzania.

Watu wengi wanasema wanataka nchi yenye haki, lakini kiukweli hawataki nchi yenye haki.

Wanataka nchi yenye haki pale haki hizo zitakapo wafaidisha hao tu.

Ikiwa haki zitamfaidisha mtu mwingine, na oengine wao hawaoni umuhimu wa haki hizo, wanazipotezea tu.

Nyie ni watu wabinafsi sana hamuwezi kumfikiria mtu mwingine.

Na hii ni moja ya sababu umasikini hauwezi kuisha.

Jamii ya watu wasioweza kuwafikiria watu wengine ni jamii itakayoshindwa kumaliza umasikini. Viongozi hawataweza kuwajali wananchi, kwa sababu itawaona hawa ni watu baki tu.

Watu wenye uwezo hawatawajali masikini wenye mawazo mazuri, kwa sababu watawaona hawa ni watu baki wajinga tu. Masikini nao hawatawajali matajiri na kuwaibiaibia tu. Hiki ndicho kinachotokea Tanzania kwa kiasi kikubwa.

Ndiyo maana mnauawa ovyo na viongozi wenu, kwa utamaduni huu huu wa kutojali haki za wengine.

Na mnaweza kuwalaumu sana viongozi, kwa sababu wao wana nafasi ya kuua watu, lakini hata nyie wananchi mna utamaduni huo huo wa ubaguzi na kuwanyima watu wengine haki zao tu.

Kwa hiyo hapo utaona viongozi wanaoua watu na wananchi wanaobagua wenzao, wote ni Watanzania walewale tu.

Kuna mstari wa moja kwa moja kutoka Watanzania kuwabagua mashoga na viongozi wa Tanzania kuua wananchi October 29 2025.

Yote mawili ni matokeo ya Watanzania kunyima wenzao haki, kuanzia wananchi kuwanyima wananchi wenzao haki za sexual orientation mpaka viongozi kuwanyima wananchi haki ya kuishi.

Wabongo karibu wote mnawindana tu.
 
Mkuu shoga sio binadamu binadamu wana jinsia mbili kwahio ukiongelea binadamu shoga hayumo
Jinsia ni nini? Ushoga ni nini?

Nani kakwambia ushoga ni jinsia?

Inaonekana unaandika mambo ambayo huyaelewi kabisa.
 
Back
Top Bottom