Januari Makamba adai uchaguzi wa 2020 ulitugawa, watu walifungwa, walinyang'anywa pesa, na waliharibiwa biashara zao

Januari Makamba adai uchaguzi wa 2020 ulitugawa, watu walifungwa, walinyang'anywa pesa, na waliharibiwa biashara zao

Utamdhibiti na katiba inamruhusu!? Utawezaje!?
Katiba inamruhusu kufanya nini?

Wewe unaelewa kuwa katiba hii hii inayolalamikiwa kuwa ni mbovu ina mchakato wa kumuondoa rais madarakani? Unajua ina impeachment process?

Katiba unaitaja na kuilalamikia tu? Au unaisoma?

Unajua hata impeachment ni nini?
 
Kajamaa ni kajanja kajanja kanmaneno , nadhan watu wa Pwani wanaujanja wa Maneno na majungu.

Wataisomba namba
 
..sasa kwanini Magufuli alichanganya mambo hayo mazuri na dhuluma za kufunga wanasiasa, kuiba uchaguzi, kunyang'anya pesa, kuharibu biashara za watu?
Weka na ushahidi mbona mnaongea tu

1) mwanasiasa gani aliyefungwa na JPM
2) Raisi gani aliyestahili kushinda kura zake zikaibiwa na JPM
3) Mfanya biashara gani biashara zake ziriharibiwa
 
Katiba inamruhusu kufanya nini?

Wewe unaelewa kuwa katiba hii hii inayolalamikiwa kuwa ni mbovu ina mchakato wa kumuondoa rais madarakani? Unajua ina impeachment process?

Katiba unaitaja na kuilalamikia tu? Au unaisoma?

Unajua hata impeachment ni nini?
Impeachment ni huko huko kwenu Marekani. Huyo Rais mjinga wa kuruhusu Hilo kutokea wakati mamlaka ya umungu mtu anayo hawezi kuwa hapa Afrika bali huko kwenu USA baby. By the way Ukijua wewe impeachment inatosha, Mimi nitajifunza toka kwako
 
Kwa hiyo unakubali kwamba hapo kwenye impeachment tatizo ni rais, watu, utamaduni, si katiba kama ulivyotaka kusema awali?

Rais ana mamlaka makubwa, lakini impeachment process ya kikatiba ipo.

In fact hata hayo mamlaka makubwa ya rais CCM wakitaka kuyaondoa wanaweza. Hawataki tu.

Kwa hivyo wote hao mpango wao mmoja.

Wanataka kuvuruga uchaguzi, wakishavuruga, wanatupiana lawama nani kavuruga uchaguzi.

Makamba kama kweli aliona uchaguzi umevurugwa angejiuzulu in protest.

Yeye mwenyewe kaingia bungeni kwa "kupita bila kupingwa". Kwenye katiba hakuna mbunge wa "kupita bila kupingwa".
 
Yeye na wengine wote ni zao la uchafuzi ule.
Hao wengine uwaitao zao la uchafuzi ndio hao hao uwaitao 'waheshimiwa' waliopo madaraka wanakula kwa urefu wa kamba zao.

Bi Kizimkazi na wateule wake wote ni zao la hao wachafuzi.

Acha kuwa mpumbavu kwa kumlaumu marehemu ilihali watenda mabaya walio hai wakikukausha damu.
 
Naomba nisimuwekee maneno Makamba.

Maneno aliyoyazungumza ni tuhuma nzito kwa utawala wa Rais Magufuli.
Kama waiiba kura alikuwa sehemu ya kuratibu kuiba kura, kitengo cha kubadilisha matokeo. Hakupewa nafasi kubwa baada ya wizi akawekwa pembeni ndio shida.

JPM angempa wizara ya nishati usingesikia hizi kelele. Angepiga pesa za kutosha.

Alikopa kwenye mifuko ya jamii na NGO yake ya Bumbuli mabilioni hajalipa hadi leo. Wewe Joka Kubwa , Kuu, unamwamini huyu muhuni, ndio role model wako?

Alipokuwa Nishati visingizik vilikuwa mara ukarabati, mara crane, mara mvua, mara uchepushaji wa maji. L

Amefanya nini cha maana kwa Tanzania?
 
Pasipoti yako imegongwa muhuri tarehe ngapi ulipoingia Tanzania ukitokea Pluto?
Nilijua kabisa hakuna atakayeweka huo ushahidi

1) Kuna mwanasiasa mmoja Mbeya alitukana watu na matusi ni kosa la jinai akafungwa Leo hii mnamsingizia JPM

2) Uchaguzi kama ungekuwa sio Halali tungekuwa na kesi nyingi sana Mahakamani za Uchaguzi kutoka Kwa wabunge na madiwani

Sasa iweje madiwani washinde kihalali na wabunge washinde kihalali alafu Raisi asishinde kihalali hayo ni mahesabu ya wapi?

Kama mdee aliibiwa kura mbona hajaenda Mahakamani? Tena mwanasheria ni yeye mwenyewe

3) Mfanya biashara aliharibiwa biashara zake nani Manji?

Manji alikuwa anachezesha system za bandari Ili watu wasiotoe mizigo Yao Kwa wakati Ili bandari zake kavu zipige pesa

Manji aliinunua coco beach Kwa magumashi

Manji aliinunua kiwanja Cha waislam pale Changombe Kwa magumashi

Alafu wewe jinsi unavyomjua JPM anaweza kuwachekea wafanyabiashara wa namna hii labda huyu bi mkubwa ila sio JPM

R.I.P Jembe langu
 
Weka na ushahidi mbona mnaongea tu

1) mwanasiasa gani aliyefungwa na JPM
2) Raisi gani aliyestahili kushinda kura zake zikaibiwa na JPM
3) Mfanya biashara gani biashara zake ziriharibiwa
We ni Mtz kweli!
 
Jiwe alikuwa mshenzi sana. Asante mhe. January Makamba kwa kulisema hili ili dunia ijue. Na January ndiyo mwanaccm pekee uliyebakia kuwa na akili.

Mhe. January Makamba naomba uende mbali zaidi, kwa kuitaka serikali kifuta kumbukumbu zote za serikali zinazomtambua jiwe kama mmoja wa watu waliowahi kuwa marais nchi hii.
Ushauri wa kijinga kabisa,kisa vyeti feki,mishahara hewa kwani MUNGU anaruhusu vyeti feki? Ukifuta unaondoa makao makuu idodomya,jnhpp,sgr afutwe kisa uliingia 18 zake lzm kichwa kiliwe.eti junuari ndiye ccm aliyebaki mwenye akili jinga sana wewe, huyo januari muulize dili la mahindra ndo akili hizo
 
1. Je, wanasiasa walifungwa?

2.Je, kuna walionyang'anywa fedha?

3. Je, kuna walioharibiwa biashara zao?

4. Je, shughuli za vyama vya siasa zilizuiliwa?

5. Je, uchaguzi haukuwa na makandokando?
Jibu ni ndiyo. Mbowe mfanyabiashara alifungiw bilcanas, manji alifukuzwa nchi, mo alitekwa nk. Account za wafanya biashara zilivamiwa na kuporwa mfano Nimrodi mkono mpaka akafa kwa mshtuko. Siasa zilizimwa zikabaki siasa za ccm tu ukikutwa we ni chadema unaweza kunyingwa hadharani. Uchaguzi hakukuwa uchaguzi Bali uchaguzi. Wanasiasa walifungwa mfano mbowe, mdude, sugu nk
 
Kama waiiba kura alikuwa sehemu ya kuratibu kuiba kura, kitengo cha kubadilisha matokeo. Hakupewa nafasi kubwa baada ya wizi akawekwa pembeni ndio shida.

JPM angempa wizara ya nishati usingesikia hizi kelele. Angepiga pesa za kutosha.

Alikopa kwenye mifuko ya jamii na NGO yake ya Bumbuli mabilioni hajalipa hadi leo. Wewe Joka Kubwa , Kuu, unamwamini huyu muhuni, ndio role model wako?

Alipokuwa Nishati visingizik vilikuwa mara ukarabati, mara crane, mara mvua, mara uchepushaji wa maji. L

Amefanya nini cha maana kwa Tanzania?

..Januari Makamba ana makandokando mengi ambayo yameshatajwa ktk mijadala mingine.

..Tunachopaswa kujadili hapa ni kama Januari amesema ukweli kuhusu uchaguzi wa mwaka 2020, na matendo ya kidhalimu ktk awamu ya 5.
 
Back
Top Bottom