Januari Makamba atapita njia ya Hayati Lowassa katika safari yake ya kisiasa

Januari Makamba atapita njia ya Hayati Lowassa katika safari yake ya kisiasa

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2009
Posts
4,175
Reaction score
2,294
Sio siri kuwa shauku ya mh Januari Makamba kuutaka urais ni kubwa sana pengine zaidi ya ile shauku ya mh Lowasa. Lakini kwa bahati mbaya mapito yake hayatatofautina na yale ya Mh Lowasa.

Atajitahidi sana, atakusanya watu, atakuwa kwenye makundi pendwa na hata nyakati nyingine atafika katika 5 bora, lakini kamwe hatachaguliwa kuwa mgombea Urais kupitia CCM.

Hata akifanya kama Lowassa, kuhamia upinzani nako atachaguliwa kuwa mgombea wa Urais lakini safari itaishia kama ile ya Mh Lowasa.
 
Sio siri kuwa shauku ya mh Januari Makamba kuutaka urais ni kubwa sana pengine zaidi ya ile shauku ya mh Lowasa. Lakini kwa bahati mbaya mapito yake hayatatofautina na yale ya Mh Lowasa...
Huyu jamaa hana chochote alichowahi kukifanya au hata kukisema tu cha kuonyesha kuwa anafaa kuwa rais. Kazi yake ni kupiga picha huku ameiga mapozi ya Obama. Hafai kabisa. Hata ubunge hafai. Hata uwaziri hafai.
 
Mwenyewe anfikiri, kama ukichagua bora 3 katika kugombea urais wa TZ na ukalikosa jina lake ujue umekosea.
 
Sio siri kuwa shauku ya mh Januari Makamba kuutaka urais ni kubwa sana pengine zaidi ya ile shauku ya mh Lowasa. Lakini kwa bahati mbaya mapito yake hayatatofautina na yale ya Mh Lowasa...
Sukuma gang mna gubu sana; Jaribio lenu katika uongozi wa nchi hii lilikufa na kuzikwa rasmi March 17, 2021. Acheni ujinga
 
Yupo too desperate, je ana uwezo wa kuwa raisi?
Kwa bahati mbaya mwenyewe hatambui kuwa hana uwezo wa kuvaa viatu hivyo. Mbaya zaidi alihakikishiwa na Mzee wake kuwa wao ndio waliokishika chama na Mzee huyo alijitahidi kumkuza mwanae kisiasa kwa malengo hayo.

Tatizo hakuna alichokionyesha mpaka sasa alichokifanya kikubwa sana ndani ya chama hata serikalini licha ya kupewa nafasi katika maeneo nyeti yanayowagusa wananchi moja kwa moja. Kama hakuweza huko ataweza wapi?
 
Tofauti kubwa ni kwamba Lowassa alikuwa na watu na alikuwa na uwezo. January hata hapo ndani ya chama akisimamishwa na mgeni Josephat Gwajima bado hawezi kumshinda Gwajima.
Ndio maana anajitahaidi kukusanya mali ili apanue wigo wake. Kwa bahati mbaya amekosa mbinu sahihi za kuwafikia watu. Pengine alifikiri jina la baba yake lingempaisha juu.

Na hili ndio pigo kwake, bado hajapata dawa yake, na sijui kama ataigundua.
 
Sukuma gang mna gubu sana; Jaribio lenu katika uongozi wa nchi hii lilikufa na kuzikwa rasmi March 17, 2021. Acheni ujinga
Jamani! Sukuma gang halipo. Na hata kama lingekuwepo sio tatizo kabisa katika nchi hii. Tatizo ni baadhi ya wanasiasa wanaofikiri kuwa toka wazaliwe tayari walishakuwa viongozi.

Na juhudi za kufikia malengo yao hazina kikomo. Na kwa yeyote aliyekuwa Rais kwao wanaona kama ni bahati mbaya tu mpaka pale wao wataposhika nafasi hiyo.

Hawa ndio tatizo kubwa la nchi hii.
 
Back
Top Bottom