Iron SMTZ
Member
- May 10, 2019
- 77
- 232
Narudia kusema, mwanamke akitaka kukufanya chochote ndani ya mahusiano anaweza atafanikiwa kwa namna yoyte, haijalishi mwanaume una strengths gani in terms of wealth, intelligence or physical. Wanawake wenye akili na wanaotambua nafasi yao ktk ndoa au mahusiano huwafanya wanaume zao kuwa Bora zaidi na hata kufikiri mwanaume huyo ni Bora kuliko wanaume wengine. Lakini pia mwanamke anaweza kubadilika wakati wowote na akakufanyia tukio ambalo halitakuacha salama ili tu afanikishe kusudio lake hata kama nilakipuuzi machoni pa wengine. Tatizo ni wepesi wa shetani kumwingia mwanamke na kutawala hisia zake. Familia nyingi zimetawanyika na watoto kukosa maadili na ustawi kwa sababu tu mwanamke alitanguliza maslahi yake kwa kuingiwa na shetani na kisha kusababisha familia ku collapse. Sheria nyingi zinazomtetea mwanamke na kujiona ana haki sawa kama mwanaune ktk mahusiano na ndani ya jamii ni chanzo kikubwa sana cha wanawake kuharibu ustawi wa mwanaume. Kwa mjibu wa Dr Doroth Gwajima (W) takwimu za mwaka 2024 za taraka, zaidi ya 80% zimefunguliwa na wanawake wenyewe, hii ni tofauti sana na miaka ya kabla ya azimio la Beijing la 50:50. Tunakoelekea ni kumfanya mwanaume awe chini ya mwanamke tofauti hata na maandiko ktk vitabu vitakatifu, let's be very careful.