Japokuwa nimeoa lakini wanawake ndio chanzo cha wanaume kufa mapema kwenye ndoa/familia

Narudia kusema, mwanamke akitaka kukufanya chochote ndani ya mahusiano anaweza atafanikiwa kwa namna yoyte, haijalishi mwanaume una strengths gani in terms of wealth, intelligence or physical. Wanawake wenye akili na wanaotambua nafasi yao ktk ndoa au mahusiano huwafanya wanaume zao kuwa Bora zaidi na hata kufikiri mwanaume huyo ni Bora kuliko wanaume wengine. Lakini pia mwanamke anaweza kubadilika wakati wowote na akakufanyia tukio ambalo halitakuacha salama ili tu afanikishe kusudio lake hata kama nilakipuuzi machoni pa wengine. Tatizo ni wepesi wa shetani kumwingia mwanamke na kutawala hisia zake. Familia nyingi zimetawanyika na watoto kukosa maadili na ustawi kwa sababu tu mwanamke alitanguliza maslahi yake kwa kuingiwa na shetani na kisha kusababisha familia ku collapse. Sheria nyingi zinazomtetea mwanamke na kujiona ana haki sawa kama mwanaune ktk mahusiano na ndani ya jamii ni chanzo kikubwa sana cha wanawake kuharibu ustawi wa mwanaume. Kwa mjibu wa Dr Doroth Gwajima (W) takwimu za mwaka 2024 za taraka, zaidi ya 80% zimefunguliwa na wanawake wenyewe, hii ni tofauti sana na miaka ya kabla ya azimio la Beijing la 50:50. Tunakoelekea ni kumfanya mwanaume awe chini ya mwanamke tofauti hata na maandiko ktk vitabu vitakatifu, let's be very careful.
 
Natamani kila mtu asome huu ujumbe asee. umenene vyema sana mkuu
 
upo sahihi mkuu.
Nilikuja kuona hata wanawake ambao ni marafiki, ukimpa attention mmoja, mwenzake anawe ku-mind hiki kitendo chako. Urafiki wao si wa kuaminiana.
 
Jamaa waga unajua sana kutetea upande wa kikeni
 
Jamaa waga unajua sana kutetea upande wa kikeni
Wanaume tumekuwa rojo rojo mno, wanawake ndo wanapaswa kulalamila na kulindwa, sio wanaume. Sasa hali inakuwa mbaya mpaka wanaume tunataka tulindwe na kutetewa mwanamke asituumize.
 
Wanaume tumekuwa rojo rojo mno, wanawake ndo wanapaswa kulalamila na kulindwa, sio wanaume. Sasa hali inakuwa mbaya mpaka wanaume tunataka tulindwe na kutetewa mwanamke asituumize.
Umewahi kuipa akili yako muda wa kutafakari chanzo Cha ya malalamiko ya wanaume miaka hii?? Kwani wanaume wa Sasa hivi ndio wanaongoza kwa kujiua sana kulinganisha na miaka ya nyuma??
 
Umewahi kuipa akili yako muda wa kutafakari chanzo Cha ya malalamiko ya wanaume miaka hii??
Mkuu, wewe ndo uipe muda akili yako utafakari asili ya jina mwanaume. Mwanaume unalalamikaje sababu ya mwanamke, aah. Wanawake ndo wa kukalamika, mimba wanabeba wao, nyumbani wanaondolewa kwao, pesa unazitafuta wewe, Ukitaka mwingine unampata saa unataka, sasa nani wa kulindwa hapo?
Kwani wanaume wa Sasa hivi ndio wanaongoza kwa kujiua sana kulinganisha na miaka ya nyuma??
Wa sasa hivi wakishasikiliza bongoflavor za kina mario na wenzake wanakuwa nyoro nyoro tu.
 
Uhalisia upi? Yaani uamke saa10 asbh ukatafute mali ufanikiwe halafu aje aseme kuwa mali mlichuma wote?
Kama hutaki hilo, beba mimba na ulee watoto ili yeye akatafute hizo mali.

Jukum la kubeba mimba na kulea watoto, linathamani kubwa kuliko hata hizo mali unazozipa thamani kuliko utu.
 
Kama hutaki hilo, beba mimba na ulee watoto ili yeye akatafute hizo mali.

Jukum la kubeba mimba na kulea watoto, linathamani kubwa kuliko hata hizo mali unazozipa thamani kuliko utu.
Akili yako ndo imefikia kikomo? nilijua tu mara ulipoanza kujifananisha na wanawake.

Hujui kuna wana wake wapo kwenye ndoa mwaka 5 na hawana mtoto? unawaweka kwenye kundi gani?
 
Hujui kuna wana wake wapo kwenye ndoa mwaka 5 na hawana mtoto? unawaweka kwenye kundi gani?
Hizo kesi chache wala haziondoi uhalisia wa nilichokisema.

Mkuu tuishie hapa, tofauti zetu kimtizamo wala zisiwe sababu ya kukoseana adabu, kila la kheri mkuu.
 
Hoja ulizoandika ni dhaifu sana yaani na ziko nje kabisa wa chanzo husika Cha tatizo, unaonekana Bado uko usingizini na hujui kabisa ni jinsi gani the whole atmosphere ya intersexual dynamics ilivyochange na kuwa unfavorable kwa mwanaume.

Yaani Bado unaamini eti mwanaume ndani ya nyumba akiwa na uwezo wa kutimiza majukumu yake ya kiume ana hold all the power dhidi ya mwanamke, pole sana.

Usichokijua ni kwamba mwanaume tayari ameshanyang'anywa ile Strong gender privilege so licha ya kutimiza hayo majukumu yake lakini Bado Hana mamlaka kwa mkewe, kitu ambacho kimepelekea wanawake wa kisasa kuwa nagging, narcissistic na rebellious na tabia zingine zote za ajabu... Na leo ikitokea mgogoro wowote au tofauti kati ya mume na mke, hapo Mwanaume anakuwa hapambani na mkeweTena Bali anakuwa anapambana na system ambayo ndio imempa nguvu mwanamke na kumnyang'anya mamlaka mwanaume.... Yaani now in any marital crisis it is Man vs Government and not a Man vs woman weka hii akilini mwako.

This unheard massive outcry from men boils down to the overhauling of our ways of living in which we have decided to embrace the western gynocentric culture that has been socially marginalizing men and preferentially favoring women.....

Halafu wewe hapo unaniambia eti sababu ni kusikiliza nyimbo za akina Mario??? Serious?...No wonder Bado uko kwenye Utopia na mara nyingi humu unatoaga comments zenye vinasaba vya mfumo jike.

Lakini nikuluuze swali kwani huyo mwanamke kwenye hii story aliamua kuuza shamba la mmewe licha ya kukatazwa na mmewe asifanye hivyo maana tayari alikuwa amefanya kosa kama hili mwanzo? Wewe unafikiri huo ujasiri wa kurudia kosa aliupata wapi?

Na pia kwa ufahamu wako unafikiri ni kwanini vilio kama hivi hatuviskii kwenye jamii ambazo Bado ziko conservative kama vile huko middle east??? Ni kwanini huko kwa warabu na nchi nyingi za Asia wao taasisi ya ndoa iko imara na wanaume wao hawapitii mateso kwenye mahusiano/ndoa kama wanayopitia wanaume wa magharibi ambao mpaka wanafikia hatua ya kujiua??
 
Mkuu mwanamke sio tatizo hili jambo nimekuja kulijua hivi karibuni ngoja nikufahamishe

Ukiacha dunia ya sasa toka tulivyoumbwa mwanamke anatakiwa awe chini ya jinsia ME Wala hatakiwi kufanya CHOCHOTE bila kupata ruhusa ya mume na AKIENDA kinyume itakuwa kaenda kinyume na matakwa ya mji anaokaa na mume anaye mtunza hivyo kufukuzwa katika ndoa NI Jambo la kawaida na NI aibu kwa mwanamke itoshe kusema kwa historia hiyo alokuwa nayo hawezi pata mume mwingine wa kumuoa


Lakini hivi imekuwa kinyume mwanaume haezi fanya kitu au kuamua kitu bila kupata ridhaa ya mke na ukifanya maamuzi peke yako hilo nI kosa na unaweza kuyumbisha ndoa yako

NB MWANAMKE UKIMPA UHURU UKASAHAU MWANAUME NDO FINAL SAY JUA USHAFELI NA HUWEZI UKAMWAMBIA CHOCHOTE MKEO AKAKUTII ASILIMIA 100 TUJITAHIDO WANAUME TUJUE NAFASI YETU KATIKA FAMILIA
 
Kisa # Kijijini kwetu Mzee mmoja around 75-85 hivi alikuwa na mke mmoja na watoto 6 .
Huyu Mzee ndiye ngariba maarufu pale kijijini.
Siku moja yeye na mke wake walikuwa wamepiga pombe za kienyeji ndipo mke akaamua atoe ya moyoni.
"Baba fulani, hivi unajua kati ya hawa watoto 6 wa kwako ni wawili tu"?
Nasikia alienda mbali zaidi mpaka alimtajia baba wa kila mtoto.
Fear women, mkapime DNA msiwe wajinga eti katoto kamechukua macho yangu.
 
Akili yako ndo imefikia kikomo? nilijua tu mara ulipoanza kujifananisha na wanawake.

Hujui kuna wana wake wapo kwenye ndoa mwaka 5 na hawana mtoto? unawaweka kwenye kundi gani?
Kaka siku hizi Kuna wanaume wengi sana wapuuzi wapuuzi, yaani Wana akili za kishenzy ukiwasoma hoja zao mpaka unajiuliza hivi huyu kweli mama yake naye anajivunia amezaa mtoto wa kiume??

Cheki kama huyo yaani anajiona ni mwanamke kuliko hata wanawake wenyewe.... Anavyoongelea suala la watoto utafikiri kwamba hao watoto ni wa mwanaume pekee yake na Wala mwanamke Hana umiliki kwenye hao watoto, na sula la kubeba mimba sijui kwanini huwa wanataka tulione liko so special na wakati Hilo ni jukumu lao la asili na kibailojia na mwanaume Hana uwezo nalo.

Wajinga sana Hawa vijana wa kileo.... Ndio maana wanatawaliwa ovyo na wanawake
 
Sisi wanaume ndo tunaongoza kuwapiga matukio wanawake huko ndoani bt wao huvumilia ama wakishindwa huondoka bila kuua/kujiua.
Wanaume kama wewe ni hatari sana kwa wanaume wenzako hasa mkiwa kwenye position of power
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…