Ong'wise
Nikifa MkeWangu Asiolewe ni kweli Wanaume huwa wanakutana na mambo magumu na yenye kuvunja moyo, akili hata kupelekea kuwa na mvurugo wa akili.
Kuna kisa fulani hicho ni kweli asilimia zote. Kuna Mwanamke ana watoto 3+ lakini imekuja kugundulika mtoto wa pili alizaa na Mwanaume mwingine, tena baada ya miaka 25+ kupita. Mume kasomesha, katunza mpaka mtoto kawa mkubwa na karibuni Baba wa mtoto anajitokeza. Tena sio choka mbaya au Kapuku ni mtu mwenye wadhifa wake.
Yule Mzee alichokifanya kaamua kuisusa na kuikimbia ile familia karudi Kijijini kuanzisha maisha mapya akiwa na miaka 60+ na huko Kijijini anaishi kwa depression na huzuni nyingi sana.
Inaumiza na kutia sana simanzi. Sijui kwanini Wanawake huwa wanakuwa na roho za kinyama na ukatili namna hii.