Japokuwa nimeoa lakini wanawake ndio chanzo cha wanaume kufa mapema kwenye ndoa/familia

Japokuwa nimeoa lakini wanawake ndio chanzo cha wanaume kufa mapema kwenye ndoa/familia

Uzi huu unapaswa kusomwa na wana ndoa za 10 and above. Hii ni ful experience na inatokea kila siku.

Hapa nina mda nakuwa na ubabe ila unatokana na ujuaji wa wife. Yaani tunagombana ndani kwa ndani.. naona kabsa umauti hauko mbali.
Mkuu chukua hatua mapema. Hao Huwa hawakubali washindwe hata siku Moja atajifanya tu kama ameshindwa kumbe ana lake jambo kalihifadhi mwisho wa siku likija lipuka ni hatari kwako
 
point to note : "wanawake hawapendi mwanaume dhaifu"

note hii point mtoa mada Nikifa MkeWangu Asiolewe
Hii factor ifatilie.....ndio huwa unaona watu wanshangaa mbona huyu Mwanamke anapewa kila kitu lakini anadharau mume wake? Au mbona anapewa huduma zote na mume wake ana pesa lakini anadanga? The reason is one.
 
Mabibi na mabwana Habari za uzima wenu!.

Wakuu sijaenda kanisani Leo mwaka wa6 sasa bila kukanyaga kanisani. (Haiwahusu)

Nina USHAHIDI na mifano mingini sana ya wanaume waliokufa na chanzo wakiwa wake zao!

Hapa nitajikita na mifano 2 ama mitatu kama nitaweza kuandika hapahapa maana sipendi kuandika inaendelea....

Mwezi ulio pita tulimzika jirani yangu baada ya kujinyonga sababu haikuwekwa wazi sana.
Mke alisema alikuwa na madeni mengi sana (jambo ambalo siyo kweli)

Baada ya mazishi na siku kupita ndo yakaibuka yakuibuka chanzo Hadi jamaa alifikia hatua hiyo ya kujimaliza.


Story ipo Hivi;-Jamaa alikuwa ana nunua mlima wenye mawe na kuanza shughuli za kulipua mawe na kuuza Kwa wenye gari (ujenzi na kokoto)

Hii ndo ilikuwa kazi yake kubwa sana. Na ndo ilikuwa inamlisha yeye na familia yake pamoja na kusomesha Watoto wake.

Mke wake alikuwa ni mama wa nyumbani tu. Ila nyuma yake alijiingiza kwenye mikopo hii ya kausha damu.

Kuna baadhi ya vitu vilienda kama bufa screen na masofa kufidia deni alikuwa anadaiwa.

Hii ni mwaka Jana. Mme wake akaenda kuvikomboa vitu vyake na vipigo akatembeza Kwa mke wake.

Siku zikaenda Mme wake akapata shida ya afya akaenda matibabu ya kienyeji kwao mwanamke akabaki na familia na kuendeleza mradi wa mawe.

Mwanamke akenda kukopa Hela wakisadiana na kaka yake. Kaka yake aka act kama Mme wa yule mama. Dhamana wakaweka shamba heka5 ambalo pia lilikuwa zuri Kwa uchimbaji wa mchanga na Mme wake alinunua Kwa malengo hayo Kuwa siku za usoni atapiga Hela za mchanga pale.

Hela ikakopwa na akashindwa kurejesha shamba likaenda.
Muda huo Mme wake ni mgonjwa yupo Kwa waganga wakienyeji akipiga simu kuomba Hela anatumiwa na kuambiwa kazi inaenda vzr tu kule kwenye mawe.

Baada ya Mme wake kurudi kuja kuona family yake huku Bado akiwa anaendelea na matibabu ndo akaambiwa na watu huko kwenye pombe.

Kwanini ameshindwa kulipa deni na shamba likaenda ?

Hapo Sasa ndo akapata taarifa kuwa kumbe Hela alizokuwa anatumiwa ni za shamba lake!

Akarudi Kwa mke wake na kumuuliza akasema ni kweli aliamua kuchukua Hela Ili zimsaidie kwenye matibabu.

Akauliza kwanini hakumshirikisha akasema hakuna haja ya kusumbua mgonjwa. Nakumbuka ilikuwa usiku wa 4 wife akaniambia mbona kama Kuna ugomvi Kwa mama X? Nikamjibu achana nao hayakuhusu.

Katika marubano hayo wife alikili kuwa kauza,shamba, na baadhi ya viwanja walivyokuwa wamenunua.

Alipoulizwa Hela ziko wapi Sasa? Hana majibu. Ugomvi ulikuwa mkubwa sana Hadi mwenyekiti wa mtaa akaitwa hiyo sasa7 usiku.

Ikabidi awaambie kesho asbh ndo atakaa nao vzr hivyo mwanamke akaenda kulala Kwa mwenyekiti wa mtaa.

Jamaa hakulala siku hiyo Kwa maelezo ya mtoto mkubwa wa drs la5 alikesha akiongea mwenyewe "Nina faida Gani Sasa,viwanja vyangu vyote vimenda Hela kapeleka wapi? Nina faida Gani Sasa hapa?Nimekuja kufanyaje hapa"


Asbh ya saa12 akawambia Watoto wake nendeni mkamwambie mama yenu hataniona Tena nendeni Sasahivi mkamwambie hivyo

Yule binti akatoka mbio huku wadogo zake wakimfuata huku wanalia. Akajaribu kujinyongea mle ndani akashindwa.

Akaenda karibu na ule mlima wa mawe kulikuwa na mwembe karibu akajinyonga Hadi kufa mle hakuacha wosia wowote ule.

MyTake licha ya haya machache tuliyoyasikia nahisi yapo mengi zaidi ya haya. Kama mwanamke yeye alisema alikuwa anadaiwa na watu wengi Ili Hali aliyejitokeza na kukubali anamdai ni mmoja tu Tena ni rafiki yake na jamaa.

Kiasi alichokuwa ana mdai ni laki2 tu. Na anasema deni Lina wiki tu alimtumia ya matibabu akiwa kule na hakuwahi kumdai alikuwa anasubiri apone kwanza maana wametoka mbali sana na jamaa.

Kisa Cha pili. Ni sehemu niliko zaliwa Mimi(kijijini)

Jamaa alikuwa mpambanaji sana na amesomesha Watoto wote na Bahati mbaya au nzuri alizaa Watoto wanaume wote tu na baadhi Yao nimesoma nao. Hii imetokea wiki iliyopita tu.

Pia nahofia hata humu Watoto wake wamo naweza funguka nikawakumbusha maumivu makubwana pengine wenyewe
Haya ninayo yaongea humu walikuwa hawajui.(Sina Nia mbaya lengo tujifunze tu)

Tangu tukiwa shule ya msingi jamaa huyu wa makamo ya miaka55+ alikuwa mpambanaji kweli. Walikuja kutengana na mke wake hapo ndo jamaa akawa na presha kubwa sana akawa anatembea na vidonge vya kushusha presha yake.


Huyu mwanamke alikuwa na kisirani sana baada ya kuachana na Mme wake hakukubali kwenda kwao Wala kugawana Mali akabaki palepale ijapokuwa hawalali pamoja na Mme wake. Walio bahatika kuzaa nae Watoto zaidi 8.

Jamaa aliamua kuanzisha mahusiano ya hapa na pale lkn mwanamke alimfanyia Fujo sana. Siyo yeye pekee hata wanawake alienda kuwafanyia visa kadhaa licha ya kuwa wameshaachana na Mme wake.

Baada ya jamaa kuona hapa hapamstahili alienda sehemu ya mbali akanunua shamba na kuanza kilimo kule ukumbuke jamaa uwezo anao sana tu akanunua vitendea kazi vya kisasa.

Kifo chake:-Baada ya kwenda kuanza makazi mapya alienda kama anaenda kambini tu siyo kifamilia. Hivyo alikuwa yeye na mtoto wake mmoja wa kiume.

Baada ya kukaa Kwa muda kadhaa alimwagiza mtoto wake huyo wa kiume arudi nyumbani huku kuangalia maendeleo ya kilimo walichoacha huku kule.

Haijulikani ilikuwaje lakini dogo aliondoka jtano, alhamis ikapita free bila kutoka mtu ndani ijumaa wakaja wa mama wa vibarua wakaita Hadi wakachoka ikawalazimu kuondoka huku wakijua kabisa kuwa mlango umefungiwa ndani hivyo Kuna mtu ndani.

Jmos asubuhi wanaume wengine wakaenda hapo Kwa ajiri ya kazi kama walivyokuwa wamekubaliana nae. Wakaita bila mafanikio kipindi wanaita wakasikia simu inaita mle ndani. Simu ikaita bila kupokelewa Hadi ikakata. Ikaita Tena wakiwapo palepale na mara hii ilipokata tu basi ikawaladhimu wazunguke nyuma dirishani Ili wachungulie kujua mbona haamki?

Kweli wakafika Ile kusukuma dirisha hawakuamini macho Yao.
Kwanza walikutana na harufu Kali na Nzi. Wakajua tiyari huyu mtu ni marehemu tiyari hawakuvunja hata mlango mja Kwa Moja wakampigia mwenyekiti wa kitongoji akaja na process za kutafutwa ndg zikaanza.

Hiki kisa sijafunguka sana ila nimejaribu kutoa taswila tu ya juu.

MyTake:- Kwa visa hizi chanzo kikubwa Cha wanaume wenzetu kufa kabla ya wakti ni wanawake wao(wake zao)

Mimi/wewe unaweza ona hakuna point ya kufikia Hadi kujiua unaweza ukawa sawa. Lakini yakikufika hakika utakuta zaidi ya Hawa au unaweza kuua.

Imagine mwanamke auze shamba lako temewa Hela haijulikani ilipo na muda huo Kuna mradi mkubwa tu umewamchia.bado haitoshi anauza na viwanja vingine huyo kama sio kumpiga na kumuumiza vibaya au hata kuua unadhani ni Nini?


Tuwe makini sana
MPK KUFUNGUA UZI HUU KUNA VITU NA WEWE USHAANZA KUPITIA HAPO NDOANI KWAKO SEMA UNASHINDWA KUFUNGUKA,FUNGUKA TUKUSHAURI MZEE
 
Tatizo mahusiano huwa tuna ya overate Sana..ndo chanzo Cha kufa mapema...
Mkuu kisa Cha pili umekisoma?

Jamaa kashaachana na mke wake miaka zaidi5 kashamwambia aseme anataka Nini apewe hataki kitu Wala kwenda kwao hataki. Ukianzisha mahusiano pembeni anaenda kufanya matukio. Na hapo umezaa naye akikamatwa police inakubidi ukamtoe Kwa sababu ya Watoto wako nao ni wakubwa tu hayupo wa chini ya miaka10 maana wa mwisho yupo chuo kikuu Kwa Sasa!

Hivi mwanamke wa namna huyo asipokupa ugonjwa wa moyo atakapa Nini? Kuna matukio mengi akama kubonda simu zako Kila ukijisahau tu ama kuteuliwa chooni nk.
 
Au kwasababu mleta mada si mhusika inawezekana kuna info hana. Unaweza ukajua habari kwa 70% ila hiyo 30% usiyoijua ikawa ya muhimu sana kwenye kuleta uhalisia wa habari.
Ndio mkuu na ndivyo ilivyo Mimi ni jirani hata Sasa hapo pamefungwa hizi habar zimetoka Kwa mwenyekiti aliyesuruhisha ungomvi maana angemuua mke wake au na yeye kujiua ndio maana aliondoka na yule mwanamke usiku ule.

Kwenye shamba alimtumia GIA ya Mme wangu ni mgonjwa anaumwa maana alichukua mkopo kwanza Kwa dhamana ya shamba Hilo. Kwa GIA hiyohiyo na vile hati zipo anazo yule mama ana julikana ndo mke wa jamaa husika yakafanyika hayo.


Mengine siyajui yote huenda ninavyojua ni 60% maana Kwa sababu hizi sijaona ya kuifanya Hadi nijiue.Ahsante sana
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Ndio mkuu na ndivyo ilivyo Mimi ni jirani hata Sasa hapo pamefungwa hizi habar zimetoka Kwa mwenyekiti aliyesuruhisha ungomvi maana angemuua mke wake au na yeye kujiua ndio maana aliondoka na yule mwanamke usiku ule.

Kwenye shamba alimtumia GIA ya Mme wangu ni mgonjwa anaumwa maana alichukua mkopo kwanza Kwa dhamana ya shamba Hilo. Kwa GIA hiyohiyo na vile hati zipo anazo yule mama ana julikana ndo mke wa jamaa husika yakafanyika hayo.


Mengine siyajui yote huenda ninavyojua ni 60% maana Kwa sababu hizi sijaona ya kuifanya Hadi nijiue.Ahsante sana
Umeeleweka mkuu.
 
MPK KUFUNGUA UZI HUU KUNA VITU NA WEWE USHAANZA KUPITIA HAPO NDOANI KWAKO SEMA UNASHINDWA KUFUNGUKA,FUNGUKA TUKUSHAURI MZEE
Mimi Sina shida tofauti na sababu tu za kawaida kabisa ambazo Kila mtu anapitia.

Nimeleta haya kutoka kwenye jamii zetu yanayotokea ndio maana kukawa na jukwaa hili!

Kama unataka kunisaidia nisaidie Hela tu Leo weekend mkuu nitashukuru sana
 
Back
Top Bottom