Japokuwa nimeoa lakini wanawake ndio chanzo cha wanaume kufa mapema kwenye ndoa/familia

Uzi huu unapaswa kusomwa na wana ndoa za 10 and above. Hii ni ful experience na inatokea kila siku.

Hapa nina mda nakuwa na ubabe ila unatokana na ujuaji wa wife. Yaani tunagombana ndani kwa ndani.. naona kabsa umauti hauko mbali.
Mkuu chukua hatua mapema. Hao Huwa hawakubali washindwe hata siku Moja atajifanya tu kama ameshindwa kumbe ana lake jambo kalihifadhi mwisho wa siku likija lipuka ni hatari kwako
 
point to note : "wanawake hawapendi mwanaume dhaifu"

note hii point mtoa mada Nikifa MkeWangu Asiolewe
Hii factor ifatilie.....ndio huwa unaona watu wanshangaa mbona huyu Mwanamke anapewa kila kitu lakini anadharau mume wake? Au mbona anapewa huduma zote na mume wake ana pesa lakini anadanga? The reason is one.
 
MPK KUFUNGUA UZI HUU KUNA VITU NA WEWE USHAANZA KUPITIA HAPO NDOANI KWAKO SEMA UNASHINDWA KUFUNGUKA,FUNGUKA TUKUSHAURI MZEE
 
Tatizo mahusiano huwa tuna ya overate Sana..ndo chanzo Cha kufa mapema...
Mkuu kisa Cha pili umekisoma?

Jamaa kashaachana na mke wake miaka zaidi5 kashamwambia aseme anataka Nini apewe hataki kitu Wala kwenda kwao hataki. Ukianzisha mahusiano pembeni anaenda kufanya matukio. Na hapo umezaa naye akikamatwa police inakubidi ukamtoe Kwa sababu ya Watoto wako nao ni wakubwa tu hayupo wa chini ya miaka10 maana wa mwisho yupo chuo kikuu Kwa Sasa!

Hivi mwanamke wa namna huyo asipokupa ugonjwa wa moyo atakapa Nini? Kuna matukio mengi akama kubonda simu zako Kila ukijisahau tu ama kuteuliwa chooni nk.
 
Au kwasababu mleta mada si mhusika inawezekana kuna info hana. Unaweza ukajua habari kwa 70% ila hiyo 30% usiyoijua ikawa ya muhimu sana kwenye kuleta uhalisia wa habari.
Ndio mkuu na ndivyo ilivyo Mimi ni jirani hata Sasa hapo pamefungwa hizi habar zimetoka Kwa mwenyekiti aliyesuruhisha ungomvi maana angemuua mke wake au na yeye kujiua ndio maana aliondoka na yule mwanamke usiku ule.

Kwenye shamba alimtumia GIA ya Mme wangu ni mgonjwa anaumwa maana alichukua mkopo kwanza Kwa dhamana ya shamba Hilo. Kwa GIA hiyohiyo na vile hati zipo anazo yule mama ana julikana ndo mke wa jamaa husika yakafanyika hayo.


Mengine siyajui yote huenda ninavyojua ni 60% maana Kwa sababu hizi sijaona ya kuifanya Hadi nijiue.Ahsante sana
 
Reactions: Tsh
Umeeleweka mkuu.
 
MPK KUFUNGUA UZI HUU KUNA VITU NA WEWE USHAANZA KUPITIA HAPO NDOANI KWAKO SEMA UNASHINDWA KUFUNGUKA,FUNGUKA TUKUSHAURI MZEE
Mimi Sina shida tofauti na sababu tu za kawaida kabisa ambazo Kila mtu anapitia.

Nimeleta haya kutoka kwenye jamii zetu yanayotokea ndio maana kukawa na jukwaa hili!

Kama unataka kunisaidia nisaidie Hela tu Leo weekend mkuu nitashukuru sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…