Jaribio la kumuua Trump: Kwanini aliyetoa taarifa kwa Secret Service na polisi kuwa juu ya paa kulikuwa na mtu mwenye silaha alipuuzwa?

Jaribio la kumuua Trump: Kwanini aliyetoa taarifa kwa Secret Service na polisi kuwa juu ya paa kulikuwa na mtu mwenye silaha alipuuzwa?

Hivi (ukiondoa mtu anayetaka kujiua) kuna mtu anaweza ku stage tukio la kuhatatrisha uhai wake kwa kulengwa risasi maeneo hatari kama kichwani kweli?!

Hata tukio la Lissu ripoti za ccm (chama cha mambuzi) zilitanabahisha kuwa lilikuwa staged na Lissu mwenyewe!

Kwa ninavyoufahamu mtiti wa risasi sidhani kama kuna mtu wa kuiletea masikhara akiwa bado anautaka ugali. Kama inawezekana basi kuna watu duniani wana mioyo migumu sana!
Sasa mkuu kama tukio ni la kutengeneza bc n lazima watafute mtu sahihi kwa ajili ya hiyo kazi, sasa sio kwa sababu amekoswa risasi ya kichwa ndio useme sio igizo, labla target ilikuwa n sikio hvy wakatafuta mtu makini kwa ajili ya hilo
 
Najiuliza inakuwaje, mwananchi amuone sniper yule zaidi ya dakika mbili na kureport kwa wanausalama wampotezee wakati huyu sniper waliyemuua huyo dogo alikuwa juu ya bati kwenye view nzuri ya kumuona huyo dogo muda mrefu tu. Kuna wakati kazi zikifanyika kwa mazoea madhara yanaweza kuwa makubwa.​
Security lapse
 
Shuhuda huyo alitoa taarifa kwa polisi na Secret Service kuhusu shooter aliyekuwa amejificha juu ya paa akiwa na silaha.

View attachment 3042534
View attachment 3041839
Mahali ambapo shooter alikuwa juu ya paa na Trump alipokuwa akifanyia campaign ni mita 130 (google earth photo)

View attachment 3041840
Secret Service Agents baada ya kufanikiwa kumuua shooter juu ya paa lilelile ambalo shuhuda alishatoa taarifa mapema kwamba alimuona mtu huyo lakini taarifa yake ikapuuzwa.


Wamarekani wanasema ni wakati wa mkuu wa Secret Service ajiudhuru.

Akiongea na BBC shahidi huyo aliweka wazi kuwa taarifa yake ilipuuzwa na vyombo vya usalama (Secret Service)
View attachment 3041843
kuna watu wanaamini ilikuwa staged, hivi kweli unaweza kustage icho kitu mtu akakupiga risasi kifuani na kwasababu ulivaa bullet proof ikadunda, na ulipopindisha kichwa kidogo tu ikafyeka sikio, nani anaweza kufanya hayo maigizo? na hadi wamuue yule kijana kwa kustage? ninachoamini, ndani ya secret service, wanamchukia trump, na democrats pia wanamchukia, waliacha makusudi, walijua kinachoenda kutokea wakaacha itokee tu wakitegemea dogo angefanikiwa, na dogo alikua sniper mzuri sana manake risasi ya kwanza ilipiga kifuani kama mbili ivi na zilizofuata alipostuka ndio akawa amelenga kichwa, trump kutikisika ile mshangao ndio risasi ikapiga sikio ila alilengwa kichwani kabisa.
 
Nnachihisi,
Secret service walimuona ila wakawa hawana uhakika na lengo lake, that's why aliposhoot nae hawakumkawiza wakamshoot maana tyr alishakua kwny range yao
sema nilichojiuliza, pale karibu na trump kulikuwa na raia upande wa pili walistuka sana na kuhangaika, ila kuna jamaa hata kutikisika hakutikisika, tangu risasi ilipopigwa hadi trump alipoondoshwa, yeye alikodoa tu macho na hakuhangaika wakati risasi zilielekezewa eneo lao. nikaamini ile wanasema mle kwenye walinzi wa marekani kuna allien wengi tu, wanadam waliochangamana na mashetani, kwasababu marekani ni nchi inayotawaliwa na mashetani hivyo wale ni nusu mtu nusu shetani ndo maana utakuta hata yakigeuka yanageuka shingo kama mamidoli ila ni watu. yeye alijifanya kuchangamana na raia kule wala hakushtuka. alikuwa poa tu wakati wenzie wanahangaika.
 
Bila kukigeuza kichwa ile risasi ilikuwa imuue, kusema Trump mwenyewe alipanga ni ngumu kukubaliana nawe
Hakuna mtu anayeweza kumess up na risasi mkuu, nakubaliana na wewe.

Pili, mpaka sasa Trump amekuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda Urais kuliko mpinzani wake yeyote yule hasa Biden ambae anaonekana umri umemtupa.
 
Hivi (ukiondoa mtu anayetaka kujiua) kuna mtu anaweza ku stage tukio la kuhatatrisha uhai wake kwa kulengwa risasi maeneo hatari kama kichwani kweli?!

Hata tukio la Lissu ripoti za ccm (chama cha mambuzi) zilitanabahisha kuwa lilikuwa staged na Lissu mwenyewe!

Kwa ninavyoufahamu mtiti wa risasi sidhani kama kuna mtu wa kuiletea masikhara akiwa bado anautaka ugali. Kama inawezekana basi kuna watu duniani wana mioyo migumu sana!
Kwa mtu kama Trump endapo angekuwa alipanga hili tukio ni lazima angewasiliana na watu professional juu ya alichotaka kufanya.

Hakuna mtu professional angemkubalia Trump afanye mzaha na kitu kinachoitwa Risasi ya kichwa.
 
Hapa ndiyo nimeelewa kwanini alivyokuja Obama Secret Service walikuwa wamekaa kwenye majengo juu kumbe sniper akiwa hata zaidi ya 100m anaweza kuleta madhara.

Nimesikiliza wachambuzi wa BBC wanasema kweli kuna uzembe wa Secret service ulifanyika.
Mita 100 ni karibu sana, hata mita 400 au 500 Sniper anakutoa kwa one shoot.
 
Suala si Trump kubadili msimamo wa nchi, bali suala ni kwamba Democrats ni lazima waendeleze vita ya Ukraine.

Wafahamu fika kwamba Trump akishinda hakutakuwa na vita ya Ukraine.

Huo ndo ukweli.
Trump alishasema haungi mkono juhudi za Putin kutaka kuimeza Ukraine.
 
Unafikiri ni kwa nini kulikuwa na delay?

Je, kama ingekuwa ni Rais Biden angekuwa kwenye campaign hiyo wangesema wasikilizie waone kwanza lengo la mtu huyo ni nini?

Kwanini mpaka risasi ipigwe ndio waanze kumshambulia?

Kwanini hawakutaka kufuatilia mapema kuhusu shooter huyo mahali alipojificha na kama ana silaha walipopewa taarifa?
Hawa washikaji ni waongo na wanafiki kishenzi. Ni mabingwa wa kutngeneza au kubadili jambo. Kennedy alipokufa walikuja na hadithi na michoro ya kuzuga tu. Ushahidi hadi leo haukamiliki. Wamebaki kuita lile tukio kama 'unsolved issue'.
 
Mita 100 ni karibu sana, hata mita 400 au 500 Sniper anakutoa kwa one shoot.
JF Kennedy alipigwa risasi tatu ndani ya sekunde 8.

Ya kwanza ilimkosa, akabaki anashangaa yaani amepigwa na butwaa.

Ya pili ikampiga begani.

Ya tatu ikapiga kichwani ikafumua kabisa ubongo.

Hivyo kusema Sniper anakuondoa kwa mpigo mmoja tu huwa inatokea lakini si mara zote.

Donald Trump sekunde ya pili baada ya kwanza kupigwa risasi, sekunde ya pili risasi imepiga kwenye sikio lake.

Sekunde ya 4 mlinzi wake kutokea ubavuni mwa kuliani kwake anamwambia lala chini na Trump anatii.

Sekunde ya 5 walinzi wake wanafika na kum cover.

Hivyo kijana aliyetaka kumuua Trump ametumia sekunde 3 tu.

Hiyo si accuracy ndogo kijana.
 
CIA wanahusikaje na usalama wa ndani ya nchi?
Huwa wanahusika inapokuwa necessary.

Unachotakiwa kukielewa ni kwamba licha ya kwamba US wana mashirika ya kijasusi zaidi ya 17 na CIA ni la nje ya nchi haimaanishi kwamba ndani hawahusiki kabisa, sio kweli.

CIA wana resources nyingi na zenye uwezo zaidi ya FBI. Kuna wakati huwa wanawatumia CIA hata operation za ndani na sometime hata agents kutoka CIA huwa wanatumwa kushirikiana na FBI and kuna baadhi ya vitu FBI huwa wanafeli kwenye access kutokana na resources hivyo huwatumia CIA.

THOSE DUDES are everywhere mkuu.

Ila ukiangalia structure yao basi lazima utaona kwamba ndani wanahusika FBI ila kiutendaji wote wanashirikiana kuhakikisha usalama wa taifa lao
 
Back
Top Bottom