Jasmine Razack: Yanga wana Roho mbaya, wamegoma kumuuza Mzize, wanataka dola Million moja

Mwambie apush basi.
 
Huyu wakala Yanga lazima wakatae kufanya nae kazi watamfanyia zengwe mpaka basi,, ila pia maneno ya wakala hayajakaa poa sip profeshino na ni mbaya kwa carrier ya mchezaji.
 
Mbona kwa fei mmeshindwa bei wanayotaka azam, ila sasa mnataka yanga wamwachie mzize kwa bei ya hasara.
 
Mpira ni biashara sio huruma
Mchezaji ndo bidhaa ya club
Timu ukija na offer ya million 1 wanayotaka Yanga watamuuza

Yanga inafanya kosa lile lile ililofanya kwa Feisal. Thamani ya mauzo ya mchezaji inabidi iendane na malipo unayofanya kwa mchezaji huyo. Mchezaji unayemlipa 15M kwa mwezi, haileti mantiki unagoma kumuuza kwa 1B. Hayo ni mahesabu gani? Hakuna biashara ya hivyo. Kama unadhani ana thamani ya 2B, basi hata mshahara wake wa sasa inabidi uendane na thamani hiyo.
 
Ninachoona Simba na Yanga zote zina kasumba mbaya dhidi ya wachezaji wazawa. Ni kama kuna agenda nyuma ya pazia. Haya mambo ya kubania wazawa hayajaanza leo, yapo toka enzi za kina Sunday Manara.
 
Mbona kwa fei mmeshindwa bei wanayotaka azam, ila sasa mnataka yanga wamwachie mzize kwa bei ya hasara.
Hujui biashara ya mpira kaa kimya. Mzize na fei wapi na wapi?
 
Mpira wetu una ma mbumbumbu wengi, kabla ya kuwa laumu Yanga nendeni mkajifunze Ulaya, mchezaji mchanga aliyetokea ndani ya klabu na ku sign mkataba wa kwanza kama professional player analipwaje?

Kama Jasmine ni wakala na ana mmiliki Mzize tangu awali Ali ruhusu vipi Mzize ku sign million 2 !!
 
Aache kulialia yeye ndio anataka malisho mazuri. Km vp aende yeye huko Al Masry
 
Hicho kimwanamke kinalazimisha biashara ili kipate 10%! Sijui hao Al Masry wamemuahidi kumlipa dola ngapi iwapo atafanikisha hilo dili la kumuuza Mzize kwa bei anayotaka yeye!

Halafu kuongea mambo ambayo hayana ushahidi, ni dalili ya mtu mwenye gubu.
 
Wabongo wengi linapokuja swala la mikataba wanaanza kuililia serikali. Mazoea ya longolongo yametuharibu sana. Dunia imebadilika, soma maandishi kwa makini kabla hujamwaga wino.
 
Ni kweli mpira ni biashara.
Swali la kujiuliza ni kweli Mazize ana thamani ya dola 1m?
Kama ndiyo basi sokoni atauzika kwa hiyo pesa na Yanga watakuwa sahihi.
Tokea atakiwe kutoka dola laki 600 hadi 700 na hadi sasa hakuna aliyefikia hilo dau wanalolitaka nafikiri anavyoelelea atakua na diminishing decline na hapo ndio majuto huwa ni mjukuu kwa mchezaji.
 
Reactions: Tsh
True. Wachezaji wa kibongo hawajifunzi kila siku wao wakiwekewa mkataba hapo wanaangalia pale kwenye mshahara tu wakiona upo vizuri umenonanona wanasaini haraka haraka. Huyo wakala wa Mzize ndio anapaswa alaumiwe kwanza alikubalije mteja wake akasaini mkataba ambao hauna kipengele cha kumruhusu mchezaji kuondoka muda wowote akipata timu yenye maslahi mazuri?

Wachezaji wa nje kila siku wanazinyoosha Simba na Yanga kwa sababu wapo makini na mikataba yao. Sasa hawa wa kwetu vilabu vinaweka vifungu vinavyowabana wakitoka kuondoka lazima walipe pesa nyingi lakini vilabu vikiwaacha vinawalipa fidia kiduchu.

Kipindi cha nyuma wakati SPUTANZA ilipokuwa "active" walau iliwasaidia kiasi fulani wachezaji sasa siku hizi sijui imefia wapi. Viongozi sijui walikuwa Kisoki na Kampira - naomba kusahihishwa kama nimekosea. Ni wakati muafaka sasa wa SPUTANZA kufufuliwa na wachezaji wetu nao wajiunge kwa wingi sio kusubiri tu wakati wameshapata shida ndio wakimbilie huko. Na hata ikifufuliwa walau basi ada ya kujiunga na mchango wa kila mwaka iwe rafiki ili iwezeshe wachezaji wote wa kibongo wajiunge ili huo umoja uwe na nguvu. Na iwe lazima kwa SPUTANZA kuajiri mwanasheria au kuipa kampuni ya wanasheria tenda ya kuwasaidia wachezaji kabla ya kuingia mkataba wakati wa usajili na kuwatetea wachezaji pale wanapodhulumiwa.

Hali ikiachwa hivi hivi wanaoumia ni wachezaji na mtafaruku kwenye soka hasa wanapotokea watu kama huyo mwansheria wa Mzize anapokuja kulalamika kwenye vyombo vya habari bila kutuwekea wazi mkataba wa Mzize unasemaje iwapo atapata timu nje. Na anaenda mbali zaidi kuilaumu Yanga badala ya kujilaumu yeye na mteja wake kwa kutoweka mazingira mazuri kwenye mkataba ili hali huwa anajigamba sana kwenye vyombo vya habari kuwa yeye ni mahiri kwenye kazi zake. Nina hakika kwa asilimia mia moja iwapo angekuwa ameweka mkataba wa Mzize vizuri walahi asingeenda kupiga kelele kwenye vyombo vya habari kwani kwa jinsi alivyojipambanua lazima Hersi na wasaidizi wake wangetafuta pa kutokea na Mzize sasa hivi angekuwa yupo anakipiga ligi ya Misri.

Ni mtiozamo tu.
 
Si
Signing fees yake alipewa milioni ngapi au unajiropokea Tu?
 
Si
Signing fees yake alipewa milioni ngapi au unajiropokea Tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…