I salute you kinsmen.
Huyu mama wakala naona amekuwa akipotosha sana na mchonganishi sana sasa nawapa za ndani na ukweli mtupu
1: Jasmine anasema eti alimtoa mzize under 20 huko na kumtengeneza alivyo leo!
Huu ni uongo mkubwa sana na upotoshaji❌️
Ukweli ni kuwa mzize aliletwa yanga na mwenyekiti wa zamani Dr mshindo msola wakati alipoenda iringa na akawa na mkutano na tawi la wanachama wa iringa ndipo wakamshauri kuna kijana mzize kama anafaa ampeleke yanga na si vinginevyo ..!❎️
Jasmine ameanza kumsimamia mzie hivi majuzi tu hapa kabla hajasaini mkataba mpya❎️
2:madai kwamba yeye ndio alibembelezwa na baba wa mzize na Zahera eti mzize abaki yanga ni uzushi❌️
Ukweli ni kuwa mzize alikuwa ni project ya yanga na zahera mwenyewe akiamua kusema hayo atasema ukweli mtupu yeye ndio alishauri mzize abaki yanga ya vijana akitengenezwa❎️
Mzize amejengwa na yanga unayoiona leo, mzize wa sasa amejengwa na brand ya yanga, kama Anadai hayo kwanini asingemtoa hapo na kumpelea huko Al.masry? Bila yanga angejulikana vipi? Biashara ni mutual benefit wote yanga na mzize wanufaike❎️
3:kudai kuwa yanga wana roho mbaya na mzize alikuwa akilipiwa mwanzo milion 2 na sasa analipwa milioni 15..
Kwanza anatakiwa ajue kuwa mkataba unasainiwa kwa mutual benefit mzize yule wa mwanzo aliyekuwa akilipwa milioni 2, sio wa sasa anayelipwa milioni 15 kwa kiwango kile cha kipindi kile klabu gani ingemlipa milioni 15?? Jasmine anataka apate asilimia yake basi bila kujali mchezaji wake anaennda wapi?
Al masry ni klabu ndogo sasa anaenda kufanyaje hapo?
Pili wakati mzize anasaini mkataba wa milion mbili yeye si anadai alikuwa anamsimamia? Alikuwa wapi kukataa na kupinga mkataba huo? Si angemchukuaga na kumpeleka al masry wakati huo? Na hata mwaka jana mzize anasaini mkataba mpya wa shilling milion 15 kwa mwezi yeye alikuwa wapi? Aache tamaa na ujanja ujanja klabu imemvumilia sana mzize na sasa ni muda wa kuvuna faida yake hakuna shortcut
🆕️ Hakuna biashara inayoweza kufanyika kwa huruma, nawashangaa sana wanaosema Yanga inabidi wakubali kumuuza Mzize utadhani wao Yanga sio timu inayomuhitaji Mzize, Yanga walionyesha kumuhitaji Clement Mzize pale tu walipompa mkataba wa miaka 3 mwaka jana, mpaka sasa Clement ametumikia mwaka 1 wa mkataba wake amebakisha miaka 2, sasa unajiuliza wakati mwaka jana Clement anasaini na Yanga Bibie wakala alikuwa wapi? Hakumshauri Clement asisaini miaka 3? Au hakuambiwa kwamba Clement anasaini?
Nadhani Yanga ukimya wao unamuumiza sana Bibie Wakala na ndio maana kila siku anafanya mahojiano, anataka sana Yanga wajibu ili mambo yawe kama yalivyokuwa ya Feisal,
Yanga wameamua kumfungia vioo. Lakini swali la Msingi pia linabaki, BIBIE NI WAKALA WA WAPI? MBONA HATAMBULIKI NA FIFA? maana FIFA wanasheria ya kuwatahini na kuwapa Vyeti tambuzi mawakala wote kabla ya kufanya kazi!
Mwisho ni kuwa al masry wametuma ofa ya Dola Qatar ya dola 700,000
Na yanga wanataka kwanzia 1000000
Huku klabu moja kutoka uarabuni Kuwait imetuma ofa ya 900000 dollar na yanga wanataka kumuuza mzize Qatar kwa maslahi mapana ya mzize mwenyewe na yanga mwenyewe!
Biashara inafanyika lakini huyu mama anataka kumuuza mzize haraka haraka ili apate percent yake kiufupi sio wakala ni dalali tu mjanja mjanja ❎️
Kila mara amekuwa mtu wa kuzua migogoro yanga pale hata isipotakiwa na anataka kumgombanisha mzize na yanga!
Safari hii yanga nawashauri waache kufanya kazi na wachezaji wanaosimamiwa na huyu mama hajui biashara ya soka na ana tamaa..
Its Pancho