Jasmine Razack: Yanga wana Roho mbaya, wamegoma kumuuza Mzize, wanataka dola Million moja

Wamuachie akatafute malisho sehemu nyingine kwa maslahi yake, wasimng'ang'anie
Mwambieni huyo dada yenu anayeleta udalali utulie,kisa anaten percent Almasry anadhani atatupelekesha Yanga? Tuna timu imeleta ya Qatar imeleta dollar 900,000/- angalau,sasa yeye Almasry wameleta dollar 600,000/- kiasa ana cha juu atapewa anataka tukubaliane naye,mpuuzi huyu
 
Huyu dada anahitaji darasa la uwakala na nimekuja kugundua why Tz nzima wakala ni mmoja anaye tambulika na FIFA. Au sijui na hapa anatafuta huruma kama kwa Fei. Yanga huyu mchezaji aliletewa na mashabiki huko alipotoka kwa mujibu wa Ricardo Momo, Yanga wamemtrain, wamebrand, wameinvest hela nyingi sasa kosa lipo wapi kutaka hela nyingi. Sasa kama Yanga walimfukuza mbona bado yupo, maanake yake walimpa nafasi.Hawa ndio wanaoleta mgogoro hasa kwenye mikataba,kesho anaweza akamwambia asuse hasije mazoezini.Nakumbuka Man Itd walikuwa wanatishia kutokufanya kazi na Mino Raiola sababu ya usumbufu kwa wachezaji wake, kama inawezekana Yanga isichukue mchezaji yoyote anaye milikiwa na huyu mwanasheria anaye jiita wakala.
 
Sasa wewe umesema hivyo unammiliki huyo mchezaji? Wamiliki wanaweza waksema ana value ya USD 100m. Uingereza wachezaji wakawaida wanauzwa kwa bei kubwa ,mpira biashara kila club ina target zake.
 
Sasa huyo Jasmine wakala? Wamevamia fani, Tanzania nzima wakala aliye fuzu mtihani wa FIFA ni mmoja tu. Huyo mganga njaa kama walivyo wengine, biashara ya mpira haijui.
 
Watu wengine bwana, sasa kama wenye mchezaji hawataki kumuuza tatizo liko wapi? Si asubiri mkataba uishe aondoke kama mchezaji huru?
Juzi hapa kuna timu ilimtaka Fei ya KKoo, ila kwa mujibu wa Zakazakazi amesema Fei kuondoka labda 2.5bil na Yanga ktk 2.5 ya kwao moja,naona wamekaa kimya kwa Fei.
 
Yanga wako sahihi kabisa. We unadhani mbadala wa mzize watampata kwa bei gani, sio mchezo. Mzize ameishaonesha ukomavu wa kutosha tu. Yanga washikilie hapo hapo tu. Kama wamesajili kiungo kwa dollar laki 6, vipi mshambuliaji wao tegemeo.
 
Wewe unadhani signing fee yake ilikuwa ngapi kama juzi tu hapa alikuwa analipwa mshahara milioni 2. Hizi roho mlizaliwa nazo au mmezipata ukubwani?
Mzize alitokea timu ya vijana ya Yanga, usingetemea kulipwa hela nyingi kwa mkataba wa mwanzo kwa sababu alikuwa bado hajawa na uhakika wa namba kwenye kikosi cha kwanza.
Baada ya kufanya vizuri ndo akaboreshewe mshahara hadi kufika hiyo milioni 15 mshahara.
Watu kama wewe na huyo dada yako ndo mnapoteza wachezaji wengi na hata wasanii kwa kuwajaza vichwa kwamba wanaonewa na kuwatengenezea migogoro na waajiri wao kwa maslahi yenu.

Huyo dada yako kajitokeza baada ya tetesi kwamba wamegomea dili la Qatar wakimshawishi aombe mshahara wa milioni 120 badala ya 75 alizopewa. Ameamua kuja kujiosha na nyie madalali wenzake mnamtetea
 
Tokea atakiwe kutoka dola laki 600 hadi 700 na hadi sasa hakuna aliyefikia hilo dau wanalolitaka nafikiri anavyoelelea atakua na diminishing decline na hapo ndio majuto huwa ni mjukuu kwa mchezaji.
Hahaha
 
Upo sahihi mkuu. Mtazamo wako upo vizuri. Wachezaji wa ndani sijui kwanini hawajifunzi kwa wa nje.
 
Atauzika
Ana umri mdogo
Kuna timu ya Tunisia imeleta dollar 900k
Yanga wanaweza kuona ila sio kuuza Kwa pressure ya management ya mchezaji
Kama kuna timu imetoa ofa ya $900k meneja wa mzize asingeelezea ofa ya 600k, angezungumzia ya 900k.
 
Yanga wasimamie msimamo wenye manufaa kwao sio kufanya kwa shinikizo la mtu ambaye amekuja katikati ya safari,anajifanya anauchungu na mchezaji kumbe anaajenda zake binafsi,anataka mchezaji aende sehemu atakayopiga pesa na Yanga wanataka wampeleke mchezaji ambapo wanatapiga pesa na ni sehemu ambayo huyo dalali ataambulia kichele,”Yanga walimfukuza ……” Lini Mzize alifukuzwa
 
Enheeeee, rudia tena hapo kwenye bei ya mayele. Hawa kurwa na dotto ni noma sana kwenye kuongeza sifuri. Ninamashaka na bei walizouzwa Chama na Miquissone
 
Wewe ndio kiongozi wa mambumbu kwa hii comment tu.
 
Fei si walikua wanampa 3.2m hapo bdo 1m anakula dalali😀😀😀😀😀😀😀
 
I salute you kinsmen.

Huyu mama wakala naona amekuwa akipotosha sana na mchonganishi sana sasa nawapa za ndani na ukweli mtupu

1: Jasmine anasema eti alimtoa mzize under 20 huko na kumtengeneza alivyo leo!

Huu ni uongo mkubwa sana na upotoshaji❌️

Ukweli ni kuwa mzize aliletwa yanga na mwenyekiti wa zamani Dr mshindo msola wakati alipoenda iringa na akawa na mkutano na tawi la wanachama wa iringa ndipo wakamshauri kuna kijana mzize kama anafaa ampeleke yanga na si vinginevyo ..!❎️

Jasmine ameanza kumsimamia mzie hivi majuzi tu hapa kabla hajasaini mkataba mpya❎️

2:madai kwamba yeye ndio alibembelezwa na baba wa mzize na Zahera eti mzize abaki yanga ni uzushi❌️

Ukweli ni kuwa mzize alikuwa ni project ya yanga na zahera mwenyewe akiamua kusema hayo atasema ukweli mtupu yeye ndio alishauri mzize abaki yanga ya vijana akitengenezwa❎️

Mzize amejengwa na yanga unayoiona leo, mzize wa sasa amejengwa na brand ya yanga, kama Anadai hayo kwanini asingemtoa hapo na kumpelea huko Al.masry? Bila yanga angejulikana vipi? Biashara ni mutual benefit wote yanga na mzize wanufaike❎️

3:kudai kuwa yanga wana roho mbaya na mzize alikuwa akilipiwa mwanzo milion 2 na sasa analipwa milioni 15..

Kwanza anatakiwa ajue kuwa mkataba unasainiwa kwa mutual benefit mzize yule wa mwanzo aliyekuwa akilipwa milioni 2, sio wa sasa anayelipwa milioni 15 kwa kiwango kile cha kipindi kile klabu gani ingemlipa milioni 15?? Jasmine anataka apate asilimia yake basi bila kujali mchezaji wake anaennda wapi?

Al masry ni klabu ndogo sasa anaenda kufanyaje hapo?

Pili wakati mzize anasaini mkataba wa milion mbili yeye si anadai alikuwa anamsimamia? Alikuwa wapi kukataa na kupinga mkataba huo? Si angemchukuaga na kumpeleka al masry wakati huo? Na hata mwaka jana mzize anasaini mkataba mpya wa shilling milion 15 kwa mwezi yeye alikuwa wapi? Aache tamaa na ujanja ujanja klabu imemvumilia sana mzize na sasa ni muda wa kuvuna faida yake hakuna shortcut

🆕️ Hakuna biashara inayoweza kufanyika kwa huruma, nawashangaa sana wanaosema Yanga inabidi wakubali kumuuza Mzize utadhani wao Yanga sio timu inayomuhitaji Mzize, Yanga walionyesha kumuhitaji Clement Mzize pale tu walipompa mkataba wa miaka 3 mwaka jana, mpaka sasa Clement ametumikia mwaka 1 wa mkataba wake amebakisha miaka 2, sasa unajiuliza wakati mwaka jana Clement anasaini na Yanga Bibie wakala alikuwa wapi? Hakumshauri Clement asisaini miaka 3? Au hakuambiwa kwamba Clement anasaini?

Nadhani Yanga ukimya wao unamuumiza sana Bibie Wakala na ndio maana kila siku anafanya mahojiano, anataka sana Yanga wajibu ili mambo yawe kama yalivyokuwa ya Feisal,

Yanga wameamua kumfungia vioo. Lakini swali la Msingi pia linabaki, BIBIE NI WAKALA WA WAPI? MBONA HATAMBULIKI NA FIFA? maana FIFA wanasheria ya kuwatahini na kuwapa Vyeti tambuzi mawakala wote kabla ya kufanya kazi!


Mwisho ni kuwa al masry wametuma ofa ya Dola Qatar ya dola 700,000

Na yanga wanataka kwanzia 1000000

Huku klabu moja kutoka uarabuni Kuwait imetuma ofa ya 900000 dollar na yanga wanataka kumuuza mzize Qatar kwa maslahi mapana ya mzize mwenyewe na yanga mwenyewe!

Biashara inafanyika lakini huyu mama anataka kumuuza mzize haraka haraka ili apate percent yake kiufupi sio wakala ni dalali tu mjanja mjanja ❎️

Kila mara amekuwa mtu wa kuzua migogoro yanga pale hata isipotakiwa na anataka kumgombanisha mzize na yanga!

Safari hii yanga nawashauri waache kufanya kazi na wachezaji wanaosimamiwa na huyu mama hajui biashara ya soka na ana tamaa..


Its Pancho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…