Jasmine Razack: Yanga wana Roho mbaya, wamegoma kumuuza Mzize, wanataka dola Million moja

Hakuna anaye Pinga kuwa hicho kipengele hakipo inapotokea ukatakq kufanya hivyo siinatakiwa uunue huo mkataba Au hujui Hilo !? Unachopaswa kufanya ni kuangalia kuwa ule mkataba uliutumikia Kwa miaka mingapi na Je Kwa hiyo miaka iliyobaki huo mkataba umebakisha thamani ipi , Kisha unalipia Ile thamani iliyopo Kisha club ndio inakuachia

So nyie mnataka watu wauzwe kiholela tu !?
 
Sasa wapi nimesema wauziwe kiholela? Sijamsapoti popote wakala, nitawapinga Yanga iwapo mchezaji atazuiwa kuvunja/kununua mkataba wake kwa value iliyopo kwenye mkataba. Kinyume na hapo Yanga ipo sahihi.
 
Unavyoongelea timu ya vijana ya Yanga utadhani unaongelea Barcelona U-17. Kuna uwekezaji gani ambao Yanga inafanya kwenye timu ya vijana? Mzize mwenyewe hajakaa hata mwaka kwenye hiyo timu ya vijana unayoitajataja hapa.
Kwahiyo mkuu shida nini hasa?

Yanga walimtoa mtaani na kumpa nafasi under 20 pale mpaka anapandishwa team ya wakubwa na kupewa nafasi kucheza walimvumilia kwenye up and down mpaka amekuwa huyu mzize wa sasa ambaye al masry wanamtaka unataka wauze tu kama mbuzi??
Umesema huyo Wakala wa Mzize hajasajiliwa, eti kuna wakala mmoja wa FIFA nchi nzima, halafu bado unataka tukuchukulie serious.
Ndiyo Tanzania mawakala wanaotambuliwa na FIFA ni mmoja tu wengine wote madalali kama wapo taja
 
Huyu mama sijui anawashwa nini na Yanga, issue ya Azam na Yanga kuweka kipengele cha Bil 1 alikipinga kwa nguvu kubwa mbona Zaka alivyoongea kakaa Kimya? Anatumika huyu sio bure
 
Leo nyie wote mu wageni ktk soka la bongo?
Hii ni tension tu ambayo inatengenezwa ionekane yanga ni klabu ya migogoro ili wachezaji wazuri wasiwe wanasaini yanga, lakini safari hii amekwama.
 
Huyu mama sijui anawashwa nini na Yanga, issue ya Azam na Yanga kuweka kipengele cha Bil 1 alikipinga kwa nguvu kubwa mbona Zaka alivyoongea kakaa Kimya? Anatumika huyu sio bure
Na yeye ndiyo chanzo cha kina Bangala na djuma kuwa hovyo yeye ndiyo kawaharibu sana

Shangaa hapo zaka ameongea yeye hajajibu kitu ila kwa yanga sasa sijui anatumwaga wapi?

Chamuhimu yanga waache kufanya naye kazi na wachezaji wake
 
Leo nyie wote mu wageni ktk soka la bongo?
Hii ni tension tu ambayo inatengenezwa ionekane yanga ni klabu ya migogoro ili wachezaji wazuri wasiwe wanasaini yanga, lakini safari hii amekwama.
Sababu viongozi hawajamjibu amekosa Kiki na zaidi anazunguka vituoni vy redio hajui anamuharibia pia mchezaji wake mzize?
 
Ndiyo Tanzania mawakala wanaotambuliwa na FIFA ni mmoja tu wengine wote madalali kama wapo taja
Ndiyo maana nimesema kwa kauli yako hii tu inatosha kupuuza maelezo yako yote maana inaonyesha ni mtu unayebwatuka tu bila kuwa na uelewa wowote wa unachokiongelea.
 
Huyu mama sijui anawashwa nini na Yanga, issue ya Azam na Yanga kuweka kipengele cha Bil 1 alikipinga kwa nguvu kubwa mbona Zaka alivyoongea kakaa Kimya? Anatumika huyu sio bure
Hahaha, Yanga bana huwa mna vitu vyenu ambavyo ukivua viatu vya ushabiki ukaviangalia unaona kuna vielement vya kukomoa.

Sasa kwa kipindi kile B1 kwa Fei kweli?, hapo ingetokea Fei angekuwa flop Azam, au asiingie kwenye mfumo wa kocha ina maana angekaa benchi mpaka mkataba uishe. Ni vile tu amepambana haswa.
 


Kwa kuwa nyie hapa mnaungana mkono kwa huu upuuzi, mnataka kutuambia Yanga ilitumia bilioni 2 kumuandaa Mzize alipokuwa U-20 alipokaa kwa chini ya mwaka mmoja? Maana huo ndiyo uwekezaji mnaosema mmeufanya kwa Mzize au kuna mwingine?

Bilioni 2 inawezekana ni bajeti ya miaka 10 ya kuendesha program nzima ya U-20 pale Yanga.
 
Reactions: Tsh
Wewe mwenyewe hujui chochote kuhusu uwakala na Biashara ya Soka kwa upabde wa Wachezaji.

Na kama Yanga imemkuza Mzize na wamemjengea Brand, si wamuuze huko Kuwait? Wanasubiri nini?
Wanasubiri makubaliano ya Mchezaji na Club anayotaka kwenda.

Sasa unataka wamuuze wakati mchezaji hajakubalina na club nayotaka kwenda.

Kiuhalisia Meneja huwa amaingia pale ambapo maslahi ya mchezaji yanazunguzmwa.

Kama mchezaji ana mkataba vilabu vinazungumza kwanza kabla ya meneja.
 
Uondokaji wake ulikuwa wa kishenzi, kwahiyo lazima ilihitaji kuweka restrictions ili walau kuwa na kaheshima
 
Mkuu naona upo nyuma sana
Kadri muda unasogea value ya bidhaa inaongezeka kutokana na ufanisi wake

Sasa tuambie mzize wa yanga B na wa sasa wanaendana?? Ulitaka auzwe bei gani??
 
Wape elimu hao
 
Mashabiki wa Yanga mtaacha ujinga lini? Huyo dada "hajajitokeza" na siyo dalali. Hiyo ni msimamizi rasmi wa Mzize anayetambulika na mamlaka zote za soka na hadi familia yake. Ni jukumu lake kulinda na kutetea maslahi ya mteja wake.
Msimamizi rasmi anajua hatua za kufuata siyo kubwabwaja kwenye vyombo vya habari na kutoa shutuma. Kama mawazo yangu ni ujinga basi anachokifanya huyo ndugu yako na dalali mwenzako ni upambavu.

Asante
 
Uondokaji wake ulikuwa wa kishenzi, kwahiyo lazima ilihitaji kuweka restrictions ili walau kuwa na kaheshima
Sema hakutaka kumlamba Engr miguu, hakuwa mnyonge kama tulivyozoea wachezaji wa ndani, alikuwa jeuri kama baadhi ya wachezaji wa nje na jeuri ikamlipa kwa kupata mkataba mzuri baina yake na Azam. Hiyo B1 ni suala la Azam na Yanga.
 
Kwa sasa Fei kwa mujibu wa Zakazakazi dau lake ni zaidi ya 2.5b,ina maana Azam wametumia 2bil kumuandaa Fei?

Mpira biashara ndio maana baadhi ya deal,club zinazivutwa sababu ya kupata dau kubwa. Mudrik alikuwa anakaribia kuja Arsenal, Chelsea na Liverpool wakapanda dau mchezaji akaenda Chelsea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…