DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Kwa hiyo mchezaji aliyekaa U-20 yako kwa chini ya mwaka mmoja, tena program yako ya vijana isiyo na mbele wala nyuma na haujatoa mchezaji yoyote wa maana kutoka katika program hiyo kwa miaka 10, leo unamlipa milioni 15, na juzi juzi tu ulikuwa unamlipa milioni 2. Umesimama mbele ya majaji wa CAS, embu jitetee hiyo value ya Mzize ya bilioni 2 inatokea wapi? Kwa gharama zipi ulizoingia kwa mchezaji huyo?Sasa mkuu wangu shida unataka kuforce mambo yaende unavyotaka
Haya wakala anataka kumpeleka mchezaji anapotaka yeye tena ofa ambayo klabu inaona ndogo je wamuuze tu??
Leo hii umemtunzq tangu team za vijana halafu unauza tu hovyo bila kuangalia value uliyotengeneza?
Yanga ni wamiliki wa mzize na wana haki ya kubargqin bei ya kumuuza sio kuuza tu kisa wakala ametaka! Hope unanielewa?
Kwahiyo wauze tu kwa bei ya hasara kisa wakala anataka? Mambo hayaendi hivyo hata kidogo mkuu lazima tukae mezani tukubaliane sio wakala afaidike kupitia mgongo wa nyuma
Kama wakala anammiliki mchezaji pekee basi amuuze saivi bila kuongea na yanga tuone..
Haya ya utumwa unaongelea wewe hapo sijui yametoka wapi??
Mzize yupo kazini na yanga taasisi ipo kazini pia
Mkataba usio wa kitumwa ni ule mkataba ambao mfanyakazi ana haki ya kuuvunja akifata masharti yaliyoainishwa kwenye huo mkataba.
Imagine una shida ya kazi, unasaini kwa mhindi mkataba miaka mi3 halafu huwezi uvunja huo mkataba hata umpe nini mhindi, hiyo miaka mi3 itakuwa ni miaka ya kitumwa.
Klabu yenu ina miaka 100 na haijawahi kununua mchezaji kwa hata 800M, mnatajataja tu 2B mnadhani pesa ya madafu hiyo.Mkuu naona upo nyuma sana
Kadri muda unasogea value ya bidhaa inaongezeka kutokana na ufanisi wake
Sasa tuambie mzize wa yanga B na wa sasa wanaendana?? Ulitaka auzwe bei gani??
Mnatoa mifano ya mizigo sijui kutoa shambani hadi sokoni. Basi peleka sokoni nyanya zako halafu sema unauza kilo 100K, si mali yako bwana na una haki ya kujipangia bei? Hapo ndiyo maana ya mchezaji siyo mtumwa inapoingia.
Unaweza kusaini mkataba lakini baadae ukienda kulalamika mbele ya vyombo vya sheria na haki, mkataba ukaonekana siyo halali, sijui kama unajua hilo.