Je, Allah alikuwepo kabla ya kushuka Quran?

Allah na God Sio sawa..
Ila Kiarabu neno Mungu ni ilahi au Ilah na sio Allah...

PakiJinja Tricky hizo Unaweza kuwafanyia hao waislamu na wakristo wasiojua Lugha..

KWa mfano Kwenye Kalima ya kwanza ya Uislam au Tayyab kalima..

Inasema "La Ilaha Ila Allah"
Yaani "Hapana Mungu Ila Allah"
Mkuu Leo umeongea vizuri sana ila ni watu wachache wa hiyo Imani wanajua unachokisema sema.
Tatizo ni Lugha.
Kila Mungu ana jina lake achana na sifa zake.
Sasa mi kila nikiwauliza Mungu wenu anaitwa nani wanabakia kunitajia sifa zake 99.
Mungu ana sifa zisizo hesabika wao wanasema ana sifa 99 tu.

Mfano Mungu wa Nabii Musa pamoja na kutajwa katika sifa tofauti lakini alimwambia Musa kuwa Jina lake ni NIKO AMBAYE NIKO.
Hilo ni Jina na sio Sifa.
Sasa Mungu wa Waislamu alijitambulisha kwa Jina gani kama jina na Allah wanalikataa?
Au hana jina ?
Mimi najua anaitwa Allah kama anavyo tajwa katika Shahada uliyosema hapo juu.
Yaani hata Shahada yao hawajui inasema nini .
Ila mimi najua ni kwanini baadhi yao wanalikanusha hilo jina ambalo katika sifa 99 halipo.
 
Kuna vitu vinafikirisha sana, hawa ndugu zetu katika Adam wanasema Allah alivyoona injili na torati vimechakachuliwa (japo kuwa katika quran kuna andiko linasema neno la Allah haliwezi chakachuliwa) Akashusha Quran.Sasa najiuliza inakuwaje katika quran humo humo Allah anasema mkiwa na shaka waulizeni watu wa kitabu? Je ni kitabu gani hiko..maana vitabu vilichakachuliwa ndio maana akashusha quran.
 
Wataalamu wa dini na wana historia wabobevu naomba mnisaidie hii mada maana imekuwa ikiniumiza kichwa kwa muda mrefu.Inasemekana uislamu ulikuja enzi za nabii Muhammad na ndio kipindi ambacho ilishushwa qurani.

Muhammad katika utoto wake wote mpaka anafikisha miaka 40 hakuwahi kuwa muislamu na historia haijawahi kugusia kwamba katika kipindi hiko chote kama kuliwahi kuwepo uislamu mpaka muhammad alipofikisha miaka 40 ndio akashushiwa qurani na yeye akasema atakuwa wa kwanza katika waliosilimu.

Kitendo cha kusema kuwa wa kwanza katika waliosilimu ina maanisha hakukuwepo na uislamu,japo kuwa wanazuoni wanadai uislamu ulikuwepo kabla hata ya kushushwa quran.

Maswali yangu ni je ,Kabla ya kushushwa quran Allah alikuwa wapi? maana quran pekee ndio imemzungumzia.
swali la pili kama Allah alikuwepo je ni vitabu gani alivishusha kwa waislamu kabla ya quran? na kama vipo hivyo vitabu ni vitabu vipi? Je vipo mpaka leo. Kama itakuwa ni Zaburi, torati na injili je ilikuwaje Allah ashindwe kuvilinda visibadirishwe kama waislamu wanavyodai kuwa vimechakachuliwa na pia wanasema vimetungwa na wanadamu? na kama sio zaburi, torati na injili ilikuwaje uislamu ukacopy zaidi ya asilimia 70 toka kwenye hivyo vitabu?

Karibuni

Ukipata naimba uniulizie swali la nyongeza kuwa Quran kama kitabu kiliandikwa takriban miaka 100 baada ya Mtume kufa.. yaan mtume alipokufa ilichukia miaka 100 Quran kuwekwa kwenye maandishi na kutambulika rasmi

Kabla ya hapo ilikuwa ikisambazwa na kufundishwa kwa kinywa kama ambavyo alishushiwa mtume sasa swali langu TUTAAMINI VIP CREDIBILITY YA HAO WALIOAMUA KUKUSANYA AYA ZA QURAN NA KUZIWEKA KWENYE KITABU KINA "ABU BAKR", na WENZIE JE KAMA WALICHAKACHUA WAKATOA AU KUONGEZA BAADHI YA AYA, MAANA KUNA AYA ZINA UTATA SANA
 
Mpagani ni anaye abudu miungu wengi yey Alikuwa Ana amini mafundisho ya Ibrahimu na kufuata tamaduni za Ibrahimu.
Lakini historia ya pale Maka inaonesha makoreshi walikuwa wana Mungu wao.
Na waliokuwa wanamuabudu Mungu wa Ibrahimu hapo Maka ni Mayahudi
 
Tatizo siyo dini tatizo naloliona hapo ni elimu yetu duni inayofanya mtanzania kutojua kwamba duniani kuna lugha mbali mbali

Pili ungejua misingi au maana ya uislamu usingejiuliza hayo maswali yako,maa uislamu msingi wake ni kwamba mungu ni mmoja ,na alitumia mitume kugikisha ujumbe duniani kuanzia adam, musa hadi muhammad
Allah kwa kiarabu ni mungu, awe mkristo awe muislamu wote wanatumia neno allah kumaanisha mungu
Na mungu hajawahi kubadilika na ni mmoja tu hata ukiwauliza watu wa musa yani jews watakwambia mungu ni mmoja ambao kwao mungu ni yahweh,ikimaanisha mungu, na hakuna mungu watatu kama wazungu wanavyowadanganya
Na mungu alileta amri kumi ,na masharti ya chakula kama kula wanyama wanaocheua na wenye kwato zilizogawanyika ukienda kwa watu wa musa watakwambia waliambiwa hivyo, na ukiangalia quran utakuta hivyo hivyo
Swala haponi elimu tu hakuna kinachochanganya
Monotheistic religions zipo nyingi mno.
Je nao ni waislamu?
 
Kukujibu hili boss, kama wewe ni Mkristo, Hebu acha kufuata ulichozoea na badala yake Soma Biblia na mfuate Yesu.

1. Fuga ndevu kama yesu
2. Vaa kanzu fupi kama Yesu
3. Vaa makubazi kama Yesu
4. Swali kama Yesu kwa kufunga mikono na kusujudu

Wakati ukifanya yote hayo watu wakuangalie, je watasema wewe unafuata mafundisho ya nani? Wengi watasema wewe ni muisilamu.

Mitume wote walileta message moja tu, ukifuata mafundisho yao kwa asilimia kubwa utajikuta unafuata mafundisho ya Kiislamu. Leo hii wakristo na waisilamu wanatofautiana sababu kubwa ni wakristo kuacha mafundisho ya Biblia na kufuata maneno ambayo hayapo kwenye Biblia.

Huyu mchungaji akionesha namna wakristo wa zamani walivyo kuwa wakiswali, wayahudi na Waisilamu nao wanaswali almost hivyo hivyo.
View attachment 3140427

So mtume ama waisilamu kufuata mafundisho ya Ibrahim ni sawa na kufuata ya Yesu ni sawa na kufuata ya Musa etc mitume wote walikuja na msg moja ndio maana pia hizi dini zinaitwa Abrahamic.
Mayahudi wanasali kama waislam?
 
Mkuu Leo umeongea vizuri sana ila ni watu wachache wa hiyo Imani wanajua unachokisema sema.
Tatizo ni Lugha.
Kila Mungu ana jina lake achana na sifa zake.
Sasa mi kila nikiwauliza Mungu wenu anaitwa nani wanabakia kunitajia sifa zake 99.
Mungu ana sifa zisizo hesabika wao wanasema ana sifa 99 tu.

Mfano Mungu wa Nabii Musa pamoja na kutajwa katika sifa tofauti lakini alimwambia Musa kuwa Jina lake ni NIKO AMBAYE NIKO.
Hilo ni Jina na sio Sifa.
Sasa Mungu wa Waislamu alijitambulisha kwa Jina gani kama jina na Allah wanalikataa?
Au hana jina ?
Mimi najua anaitwa Allah kama anavyo tajwa katika Shahada uliyosema hapo juu.
Yaani hata Shahada yao hawajui inasema nini .
Ila mimi najua ni kwanini baadhi yao wanalikanusha hilo jina ambalo katika sifa 99 halipo.

Pia neno ALLAH, lilikuwa lilitumika na wapagan wa kiarabu kutambulisha Mungu wao wa kipagan, and Allah its a tittle ambao kwa lugha nyepesi maana yake ni supreme God, ironical hata staili Yao ya kuabudu ilikuwa kuzunguka jiwe ambalo waliamini ndio ndan kuna Mungu wao,
same Practise Mtume aliwaambia Waislam waifanye..
 
Mimi nitakujibu kwa uchache kuhusu Uislamu, japo mimi ni mkristo.

1. Uislamu Kabla ya Nabii Muhammad

Katika mtazamo wa Kiislamu, Uislamu si dini iliyoanzishwa na Nabii Muhammad (s.a.w.) pekee, bali ni dini ya kimapokeo inayojulikana kama Dini ya Tauhidi—imani katika Mungu Mmoja. Katika Qur’an, inaelezwa kuwa manabii waliotangulia kama Ibrahim (Abraham), Musa (Moses), na Isa (Yesu) wote walikuwa "Waislamu" kwa maana ya wale waliojitoa kwa Mungu Mmoja. Hii inamaanisha kuwa dhana ya Uislamu kwa msingi wa kiimani, yaani kumwamini Mungu Mmoja (Allah) na kumtii kwa maelekezo yake, imekuwepo hata kabla ya Nabii Muhammad (s.a.w.). Kwa hiyo, Uislamu kwa maana pana ya "kujisalimisha kwa Mungu Mmoja" unachukuliwa kuwa uliwepo tangu zamani.

2. Kitendo cha Nabii Muhammad Kusema "Mimi ni wa Kwanza Kusilimu"

Nabii Muhammad alipotamka kuwa yeye ni wa kwanza kusilimu, alimaanisha kuwa yeye ndiye wa kwanza kupokea na kutii wahyi wa Qur’an, ambayo ni ujumbe mpya ulioshushwa kwake ili kukamilisha na kusahihisha mafunzo ya vitabu na mafundisho ya manabii wa zamani. Hii haimaanishi kwamba hakukuwa na watu waliomwamini Mungu Mmoja kabla yake, lakini kwa mujibu wa Uislamu, mafundisho yao yalipotoshwa na wanadamu kwa vipindi tofauti vya kihistoria.

3. Uwepo wa Allah Kabla ya Qur’an na Vitabu Vingine

Kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, Allah ni Mungu ambaye ameumba kila kitu na yupo daima. Vitabu kama vile Taurati (Torah), Zaburi (Psalms), na Injili (Gospels) vinatajwa katika Qur’an kuwa vilitumwa na Mungu kwa watu wa wakati huo kupitia manabii kama Musa (Moses), Daudi (David), na Isa (Yesu) kwa ajili ya kuwaongoza kwenye imani na matendo mema. Hata hivyo, waislamu wanaamini kwamba baadhi ya mafundisho ya vitabu hivi yalibadilishwa na wanadamu kwa muda na matukio tofauti ya kihistoria, na hii ndiyo sababu Qur’an ilishushwa kama mwongozo wa mwisho na ambao haubadiliki, kwa kuwa Mungu ameahidi kuulinda.

4. Kwa Nini Vitabu vya Zamani Kama Taurati, Zaburi, na Injili Havikulindwa?

Kwa mujibu wa tafsiri ya wanazuoni wa Kiislamu, Allah aliruhusu vitabu vya awali kuvunjika au kubadilishwa kwa kuwa vilikuwa kwa ajili ya makundi maalum ya watu, na vilikuwa na kipindi maalum cha muda. Qur’an inaelezwa kuwa ni ujumbe wa mwisho kwa wanadamu wote, na kwa mujibu wa imani ya Kiislamu, Allah ameahidi kuulinda ujumbe huu dhidi ya mabadiliko ya wanadamu. Hii ndiyo sababu Qur’an inachukuliwa na waislamu kama mwongozo wa kipekee na wa mwisho.

5. Uislamu na Ufanano wa Qur’an na Vitabu vya Zamani

Uislamu unaamini kuwa mafundisho ya msingi kuhusu Mungu, uadilifu, na maadili ni ya kudumu na yamekuwepo kwa vizazi vyote. Qur’an inasema kuwa kuna mambo ya msingi yaliyoshirikishwa katika vitabu vyote vya mbinguni, kwa sababu ya ujumbe wa pamoja kuhusu Mungu Mmoja. Hata hivyo, Qur’an inajitofautisha kwa namna nyingi, ikiwemo jinsi ilivyoshushwa, mfumo wake wa lugha, na mwelekeo wa jumla wa kisheria na kijamii ambao unakidhi mahitaji ya wakati wote.
Porojo za Kusadikika
 
Wataalamu wa dini na wana historia wabobevu naomba mnisaidie hii mada maana imekuwa ikiniumiza kichwa kwa muda mrefu.Inasemekana uislamu ulikuja enzi za nabii Muhammad na ndio kipindi ambacho ilishushwa qurani.

Muhammad katika utoto wake wote mpaka anafikisha miaka 40 hakuwahi kuwa muislamu na historia haijawahi kugusia kwamba katika kipindi hiko chote kama kuliwahi kuwepo uislamu mpaka muhammad alipofikisha miaka 40 ndio akashushiwa qurani na yeye akasema atakuwa wa kwanza katika waliosilimu.

Kitendo cha kusema kuwa wa kwanza katika waliosilimu ina maanisha hakukuwepo na uislamu,japo kuwa wanazuoni wanadai uislamu ulikuwepo kabla hata ya kushushwa quran.

Maswali yangu ni je ,Kabla ya kushushwa quran Allah alikuwa wapi? maana quran pekee ndio imemzungumzia.
swali la pili kama Allah alikuwepo je ni vitabu gani alivishusha kwa waislamu kabla ya quran? na kama vipo hivyo vitabu ni vitabu vipi? Je vipo mpaka leo. Kama itakuwa ni Zaburi, torati na injili je ilikuwaje Allah ashindwe kuvilinda visibadirishwe kama waislamu wanavyodai kuwa vimechakachuliwa na pia wanasema vimetungwa na wanadamu? na kama sio zaburi, torati na injili ilikuwaje uislamu ukacopy zaidi ya asilimia 70 toka kwenye hivyo vitabu?

Karibuni

Allah ndio Mungu aliyeumba mbingu na aridhi pamoja na viumbe vyote

ALLAH ANAONGEA NA NABII MUSA
Kutoka 3:3
Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.
Kutoka 3:4
BWANA alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.
Kutoka 3:5
Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.

ALLAH ANAMUHADITHIA MTUME MUHAMMAD HABARI ZA NABII MUSA

Quran 20:9
Na je! Imekufikia hadithi ya Musa?
Quran 20:10
Alipo uona moto, akawaambia watu wake: Ngojeni! Mimi nimeuona moto, huenda nikakuleteeni kijinga kutoka huo moto, au nikapata uongofu kwenye moto.
Quran 20:11
Basi alipo ufikia akaitwa: Ewe Musa!
Quran 20:12
Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la T'uwa.
 
Lakini historia ya pale Maka inaonesha makoreshi walikuwa wana Mungu wao.
Na waliokuwa wanamuabudu Mungu wa Ibrahimu hapo Maka ni Mayahudi
Kulikua na Hanafi, historicaly wapo documented kupinga hili ni kuendekeza ubishi tu, kuanzia source za west hadi east scholars wanakubali, kinachokua debated ni kama Walikua kama Organized Cult ama Individual tu.
 
Allah ndio Mungu aliyeumba mbingu na aridhi pamoja na viumbe vyote

ALLAH ANAONGEA NA NABII MUSA
Kutoka 3:3
Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.
Kutoka 3:4
BWANA alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.
Kutoka 3:5
Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.

ALLAH ANAMUHADITHIA MTUME MUHAMMAD HABARI ZA NABII MUSA

Quran 20:9
Na je! Imekufikia hadithi ya Musa?
Quran 20:10
Alipo uona moto, akawaambia watu wake: Ngojeni! Mimi nimeuona moto, huenda nikakuleteeni kijinga kutoka huo moto, au nikapata uongofu kwenye moto.
Quran 20:11
Basi alipo ufikia akaitwa: Ewe Musa!
Quran 20:12
Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la T'uwa.
Kwa hiyo ndio umeprove nini hapa? huwa mnasema Allah aliishuha quran kwa sababu injili na torati vimechakachuliwa ,mbona Allah katika hiyo hiyo quran anasema mkiwa na shaka nendeni mkatafute msaada kwa watu wa kitabu.Sasa ni kitabu gani Allah anachozungumzia ikiwa Alishusha quran baada ya kuona Kitabu kimechakachuliwa.Kwa nini aendelee kutumia reference kwa kitabu kilichochakachuliwa.Halafu kama ukisoma kwa Umakini ni kama Allah anajitenga na watu wa kitabu na anaonesha kabisa kwamba kushuka kwa qurani sio substitute ya vitabu vilivyotangulia bali kaamua kushusha kitabu chake tu huku vingine vikiendelea kuwepo.
 
Nimeprove kisomi Ili kukuonyesha kuwa Allah ndio aliyemtuma nabii Musa pia Allah huyohuyo ndio aliyemtuma nabii Muhammad

Kuhusu kuchakachuliwa Taurati na Injili sio Quran tu ndio imesema hata Taurati yenyewe na Injili zinakubali kuwa zimechakachuliwa

Nabii Yeremia anasema Taurati imechakachuliwa
Yeremia 8:8
Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya BWANA tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.

Luka anasema Injili imechakachuliwa

Luka 1:1
Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu,
Luka 1:2
kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo,
Luka 1:3
nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu,

Acha kuishutumu Quran Bibilia lenyewe linakubali kuwa limechakachuliwa

Pia tambua kuwa ndani ya Bibilia hakuna Taurati ila Kuna kumbukumbu la Taurati mlipo lipata hilo kumbukumbu la Taurati mnajua wenyewe

Pia ndani ya Bibilia hakuna Injili ila Kuna Injili kama ilivyoandikwa na hao wandishi
 
Umejibu vizuri sana kwa kuthibitisha hivi vitabu vimechakachuliwa,enhee ilikuwaje Allah wenu akasema kama mnashaka watafuteni watu wa kitabu vilivyochakachuliwa wawasaidie.? yaani Quran haijitoshelezi inaomba msaada kwa vitabu ilivyochakachuliwa..hahahaaa.
 
Kumbe nyie ni ndugu,mbona mnachukiana
Torah inakataza hata wayahudi kuwa na Taifa hadi Messiah aje, kuna wayahudi kibao na wao wanapigwa na kutolewa maneno machafu na huo utawala wa Israel. Kinachoendesha ile nchi sio uyahudi kama dini bali ni uyahudi kama asili ila wengi wao mule ni Atheist wasio na dini.

Wayahudi wengi wenye dini Wapo upande wa Palestine.
 
Umejibu vizuri sana kwa kuthibitisha hivi vitabu vimechakachuliwa,enhee ilikuwaje Allah wenu akasema kama mnashaka watafuteni watu wa kitabu vilivyochakachuliwa wawasaidie.? yaani Quran haijitoshelezi inaomba msaada kwa vitabu ilivyochakachuliwa..hahahaaa.

Quran 10:94
- Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka.

Hivi mnadhani Quran inaposema watu wa kitabu na nyinyi wagalatia mpo?

Kitabu gani wakolitho, wagalatia Tito na Rumi ? Hivyo vyenu vilivyokuleteeni ukristo Mungu Wala havitambui

Na ndio maana nyinyi wagalatia ndani ya Quran Kuna spana zenu za kutosha kama
Yesu sio Mungu
Mungu hawezi kuwa na mwana Kwa sababu hana MKE
Yesu sio mtoto wa Mungu
Mungu ni Moja na sio 3
 
Ukishasema Mungu hawezi kuwa kitu fulani basi huyo hana sifa ya uungu..Mungu anaweza kujifanya vyovyote atakavyo..Kama anavyotumia wingi kwenye quran
 
Waislamu Bado mnasubiriwa mseme.
Mungu wenu anaitwa nani ?
Na ni kwanini hamko huru kumtaja jina lake ?
Je mnapo apa Shahada yenu mnasema Hakuna Mungu ila Mungu?
Huku ni kukosa kujiamini ?
 
Back
Top Bottom