Je, Allah alikuwepo kabla ya kushuka Quran?

Mkuu Leo umeongea vizuri sana ila ni watu wachache wa hiyo Imani wanajua unachokisema sema.
Tatizo ni Lugha.
Kila Mungu ana jina lake achana na sifa zake.
Sasa mi kila nikiwauliza Mungu wenu anaitwa nani wanabakia kunitajia sifa zake 99.
Mungu ana sifa zisizo hesabika wao wanasema ana sifa 99 tu.

Mfano Mungu wa Nabii Musa pamoja na kutajwa katika sifa tofauti lakini alimwambia Musa kuwa Jina lake ni NIKO AMBAYE NIKO.
Hilo ni Jina na sio Sifa.
Sasa Mungu wa Waislamu alijitambulisha kwa Jina gani kama jina na Allah wanalikataa?
Au hana jina ?
Mimi najua anaitwa Allah kama anavyo tajwa katika Shahada uliyosema hapo juu.
Yaani hata Shahada yao hawajui inasema nini .
Ila mimi najua ni kwanini baadhi yao wanalikanusha hilo jina ambalo katika sifa 99 halipo.
 
Kuna vitu vinafikirisha sana, hawa ndugu zetu katika Adam wanasema Allah alivyoona injili na torati vimechakachuliwa (japo kuwa katika quran kuna andiko linasema neno la Allah haliwezi chakachuliwa) Akashusha Quran.Sasa najiuliza inakuwaje katika quran humo humo Allah anasema mkiwa na shaka waulizeni watu wa kitabu? Je ni kitabu gani hiko..maana vitabu vilichakachuliwa ndio maana akashusha quran.
 

Ukipata naimba uniulizie swali la nyongeza kuwa Quran kama kitabu kiliandikwa takriban miaka 100 baada ya Mtume kufa.. yaan mtume alipokufa ilichukia miaka 100 Quran kuwekwa kwenye maandishi na kutambulika rasmi

Kabla ya hapo ilikuwa ikisambazwa na kufundishwa kwa kinywa kama ambavyo alishushiwa mtume sasa swali langu TUTAAMINI VIP CREDIBILITY YA HAO WALIOAMUA KUKUSANYA AYA ZA QURAN NA KUZIWEKA KWENYE KITABU KINA "ABU BAKR", na WENZIE JE KAMA WALICHAKACHUA WAKATOA AU KUONGEZA BAADHI YA AYA, MAANA KUNA AYA ZINA UTATA SANA
 
Mpagani ni anaye abudu miungu wengi yey Alikuwa Ana amini mafundisho ya Ibrahimu na kufuata tamaduni za Ibrahimu.
Lakini historia ya pale Maka inaonesha makoreshi walikuwa wana Mungu wao.
Na waliokuwa wanamuabudu Mungu wa Ibrahimu hapo Maka ni Mayahudi
 
Monotheistic religions zipo nyingi mno.
Je nao ni waislamu?
 
Mayahudi wanasali kama waislam?
 

Pia neno ALLAH, lilikuwa lilitumika na wapagan wa kiarabu kutambulisha Mungu wao wa kipagan, and Allah its a tittle ambao kwa lugha nyepesi maana yake ni supreme God, ironical hata staili Yao ya kuabudu ilikuwa kuzunguka jiwe ambalo waliamini ndio ndan kuna Mungu wao,
same Practise Mtume aliwaambia Waislam waifanye..
 
Porojo za Kusadikika
 

Allah ndio Mungu aliyeumba mbingu na aridhi pamoja na viumbe vyote

ALLAH ANAONGEA NA NABII MUSA
Kutoka 3:3
Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.
Kutoka 3:4
BWANA alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.
Kutoka 3:5
Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.

ALLAH ANAMUHADITHIA MTUME MUHAMMAD HABARI ZA NABII MUSA

Quran 20:9
Na je! Imekufikia hadithi ya Musa?
Quran 20:10
Alipo uona moto, akawaambia watu wake: Ngojeni! Mimi nimeuona moto, huenda nikakuleteeni kijinga kutoka huo moto, au nikapata uongofu kwenye moto.
Quran 20:11
Basi alipo ufikia akaitwa: Ewe Musa!
Quran 20:12
Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la T'uwa.
 
Lakini historia ya pale Maka inaonesha makoreshi walikuwa wana Mungu wao.
Na waliokuwa wanamuabudu Mungu wa Ibrahimu hapo Maka ni Mayahudi
Kulikua na Hanafi, historicaly wapo documented kupinga hili ni kuendekeza ubishi tu, kuanzia source za west hadi east scholars wanakubali, kinachokua debated ni kama Walikua kama Organized Cult ama Individual tu.
 
Kwa hiyo ndio umeprove nini hapa? huwa mnasema Allah aliishuha quran kwa sababu injili na torati vimechakachuliwa ,mbona Allah katika hiyo hiyo quran anasema mkiwa na shaka nendeni mkatafute msaada kwa watu wa kitabu.Sasa ni kitabu gani Allah anachozungumzia ikiwa Alishusha quran baada ya kuona Kitabu kimechakachuliwa.Kwa nini aendelee kutumia reference kwa kitabu kilichochakachuliwa.Halafu kama ukisoma kwa Umakini ni kama Allah anajitenga na watu wa kitabu na anaonesha kabisa kwamba kushuka kwa qurani sio substitute ya vitabu vilivyotangulia bali kaamua kushusha kitabu chake tu huku vingine vikiendelea kuwepo.
 

Nimeprove kisomi Ili kukuonyesha kuwa Allah ndio aliyemtuma nabii Musa pia Allah huyohuyo ndio aliyemtuma nabii Muhammad


Kuhusu kuchakachuliwa Taurati na Injili sio Quran tu ndio imesema hata Taurati yenyewe na Injili zinakubali kuwa zimechakachuliwa

Nabii Yeremia anasema Taurati imechakachuliwa
Yeremia 8:8
Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya BWANA tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.

Luka anasema Injili imechakachuliwa

Luka 1:1
Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu,
Luka 1:2
kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo,
Luka 1:3
nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu,

Acha kuishutumu Quran Bibilia lenyewe linakubali kuwa limechakachuliwa

Pia tambua kuwa ndani ya Bibilia hakuna Taurati ila Kuna kumbukumbu la Taurati mlipo lipata hilo kumbukumbu la Taurati mnajua wenyewe

Pia ndani ya Bibilia hakuna Injili ila Kuna Injili kama ilivyoandikwa na hao wandishi
 
Umejibu vizuri sana kwa kuthibitisha hivi vitabu vimechakachuliwa,enhee ilikuwaje Allah wenu akasema kama mnashaka watafuteni watu wa kitabu vilivyochakachuliwa wawasaidie.? yaani Quran haijitoshelezi inaomba msaada kwa vitabu ilivyochakachuliwa..hahahaaa.
 
Kumbe nyie ni ndugu,mbona mnachukiana
Torah inakataza hata wayahudi kuwa na Taifa hadi Messiah aje, kuna wayahudi kibao na wao wanapigwa na kutolewa maneno machafu na huo utawala wa Israel. Kinachoendesha ile nchi sio uyahudi kama dini bali ni uyahudi kama asili ila wengi wao mule ni Atheist wasio na dini.

Wayahudi wengi wenye dini Wapo upande wa Palestine.
 

Quran 10:94
- Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka.

Hivi mnadhani Quran inaposema watu wa kitabu na nyinyi wagalatia mpo?

Kitabu gani wakolitho, wagalatia Tito na Rumi ? Hivyo vyenu vilivyokuleteeni ukristo Mungu Wala havitambui

Na ndio maana nyinyi wagalatia ndani ya Quran Kuna spana zenu za kutosha kama
Yesu sio Mungu
Mungu hawezi kuwa na mwana Kwa sababu hana MKE
Yesu sio mtoto wa Mungu
Mungu ni Moja na sio 3
 
Ukishasema Mungu hawezi kuwa kitu fulani basi huyo hana sifa ya uungu..Mungu anaweza kujifanya vyovyote atakavyo..Kama anavyotumia wingi kwenye quran
 
Waislamu Bado mnasubiriwa mseme.
Mungu wenu anaitwa nani ?
Na ni kwanini hamko huru kumtaja jina lake ?
Je mnapo apa Shahada yenu mnasema Hakuna Mungu ila Mungu?
Huku ni kukosa kujiamini ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…