Kama kuna tungo tata, hii ni mojawapo. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema (kwa fasili ya Kiingereza ambayo ndiyo fasili rasmi: Ibara ya 1(3): The Republic is a secular...state..." Ina maana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 'haina dini rasmi' (kama ilivyo kwa baadhi ya nchi kwa mfano, dini ya nchi ya Uingereza ni 'Anglicanism', Poland ni Roman 'Catholicism', Morocco ni Sunni Islam, Israel ni 'Judaism', Cambodia ni 'Buddhism' etc.
Kama nchi haina dini rasmi haina maana wananchi wake hawana dini rasmi. Ina maana kila mwananchi wa Tanzania anaamini au haamini katika dini fulani. Na kila mwanachi ni mwanasiasa, lakini siyo kila mwanasiasa ni muumini wa dini fulani. Kwa hiyo, muumini au kiongozi wa dini akisema kitu fulani kinachohusiana na siasa, kwa vile yeye pia ni mwananichi, mpiga kura na mlipa kodi, akiona kuna sehemu mambo hayaendi, akisema 'mambo hayaendi...' siyo kwamba amechanganya dini na siasa. Anayechanganya dini na siasa ni kwa mfano anayempigia debe mtia nia wa cheo fulani katika nchi au chama cha siasa. Siasa maana yake ni the art of governance of its country and people'. Na kila muumini ni mwanadamu (yaani mwanasiasa). Kwa hiyo, kila mwanadini ni mwanasiasa, ila siyo kila mwanasiasa ni mwanadini/muumini wa dini fulani. Mfano, huwa tunawasikia viongozi wetu wakisema "viongozi wa dini mna mchango mkubwa sana kwenye jamii. Mtusaidie kuwaasa vijana wawe waadilifu, kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukwimwi etc."Je, ni kuchanganya dini na siasa? Lakini kuna viongozi wa dini pia huwa wanasema: "wanasiasa wanapaswa kutenda haki ili tuwe na jamii inayojali utu, utawala wa sheria na uwajibikaji..." Je, kiongozi wa dini akisema hivi anachanganya dini na siasa? Kwa wa upande wangu, akisema hivyo ametimiza wajibu wake kama Mtanzania na pia kama kiongozi wa dini anayewaongoza waumi wake ambao kati yao ni wanasiasa pia kwa sababu kama hakuna siasa yenye tija nchini hata dini haifuatwi vizuri. Na kama wanasiasa wanaosali kama hawataambiwa hivyo, kiongozi wa dini anayewaongoza anakuwa hajatimiza wajibu wake.