Uko sahihi. Lakini ukumbuke kuwa muumini wa dini anafungwa pia na sheria za nchi (au utaratibu wa utawala wa nchi na watu wake - ambao kwangu ndiyo siasa au tuseme ambao ni sehemu ya siasa). Kuna mwanasheria mmoja na mwalimu wa mambo ya jamii Paulo Freire anatoa mfano mzuri wa kuishi imani na siasa (in a cross-fertised way) kwa kulinganisha pande mbili za ngazi (ladder) - mhimili wa kushoto na kulia - moja kama imani na mwingine kama siasa). Kwamba ukitaka kupanda ngazi vizuri lazima ushike mihimili hii miwili kwa pamoja - i.e ukitaka uwe 'well-integrated' ni lazima imani yako ishirikiane na siasa kukufanya wewe uwe mtu mwema. Yaani, ni kwamba imani yako inachangamana na siasa na siasa inachangamana na imani (in a cross-fertised way). Maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba mtu wa namna hiyo anaishi imani yake vizuri na wakati huohuo anaishi siasa yake vizuri tofauti na wale wakiwa nje ya nyumba ya ibada wanavua koti la imani na kuvaa koti la siasa na kinyume chake.
Watu wa namna hii kwa upande wangu ni 'opportunists' na katika maisha yao kuna 'dualism'. Mfano, kuna watu wanashiriki kuchoma moto vibaka mtaani kwa kuiba kuku, bata, TV set etc, lakini watu walewale wakiwa kwenye nyumba za ibada ndiyo wanaohubiri 'Mungu ni upendo na mwenye huruma na anataka na sisi tupendane na kusameheana'. Lakini 'well-integrated person' hawezi kumwua mtu mwenzake kwa kuiba bata, kuku, TV set etc kwa sababu anajua wazi kwamba licha ya kwamba Amri za Mungu zinakataza kuua, hata sheria za nchi pia zinakataza kujichukulia sheria mkononi maana kuna utaratibu wa kisheria wa kumpeleka mtuhumiwa wa wizi kwenye vyombo vya sheria na kuacha sheria ichukue mkondo wake. Hivyo, inategemea na uelewa wa mtu namna gani ana'practise' imani na siasa bila shida, ingawa wengine shida inaonekana waziwazi, mfano, mtumishi wa Mungu kuanza kuwanadi wagombea nafasi fulani za kisiasa madhahabuni au mwanasiasa kutumia madhahabu kunadi sera zake au kuwatumia waumini wake wamchague yeye kwa vile ni mwenzao na siyo kwa vile wanaona ana sifa za kuwa kiongozi bora etc.