Je, Cheti cha ndoa kimetajwa popote kwenye biblia au Quran?

Je, Cheti cha ndoa kimetajwa popote kwenye biblia au Quran?

Hivi unajuwa athari ya mwanandoa kukukana?
Wakati umesha invest pamoja vitu kadhaa?

Watoto
Mali nk.

Upo radhi kuvipoteza?
Hao watoto wanakuwa wako au sio wako? Kama ni wako shida nini na wanatunzwa?

Hizo mali ni zako au sio zako? Shida nini na kitu ni chako na kimeandikwa jina lako?
 
Kwani Ndoa ni nini ?
Ndoa ni ile inayofungwa kanisani / Msikitini/ Kimila na jadi au ndoa inahitaj kipi hd kuitwa ndoa
 
2.) Ni kwanini sasa wanaofunga ndoa ili kutimiza miongozo ya kidini, wanalazimishwa kutimiza takwa lisilo la kidini?
Mamlaka zote za duniani zimewekwa na Mungu. Serikali ikishauri suala ambalo halikinzani na utukufu wa Mungu bali linaongeza commitment, dini hazina haja ya kulikataa.

Besides, biblia imeelekeza kuzitii mamlaka ya kidunia kwenye mambo ambayo hayaondoi utukufu wa Mungu.
 
Naomba muongozo
Hakuna sehemu yoyote ndani ya Bible au Quran kumeonesha utaratibu wa utoaji wa cheti cha ndoa baada ya ndoa kufungwa! Isipokuwa yako madai ya watafiti wa mambo ya kale yanayodai kuwa Misri ilikuwa na huu utaratibu wa kusajili na kutoa vyeti vya ndoa miaka 3000 Kabla ya Kristo (3000 KK).
 
Sio wa dini, ni wa serikali. Vyeti vyote vya ndoa vinatolewa na serikali. Dini zinatii mamlaka ya kiserikali.

Ukifunga ndoa ya kikristo, kiislam au kiserikali wote mnapata vyeti vinavyofanana.
Kipo cheti cha Bakwata mkuu kwa waislamu ambacho ni cha kidini na sio cha serikali
 
Endapo umefunga ndoa kanisani au msikitini bila cheti, KIDINI hiyo ndoa ni halali?
Uislam unafindisha kua,ili ndoa ikamilike inahitaji mambo manne (4)

1 anaeoa
2 anaeolewa
3 anaefungisha ndoa
4 wazazi au ndugu wa muoaji/anaeolewa

Hayo mambo manne hapo yakisha kamilika basi hiyo ndoa ni halali kwa MWENYEZIMUNGU

Ila serikali wao ili wawatambue kua ni wanandoa ni mpaka pale mtakapokua mna cheti cha ndoa
 
Ukifunga kanisani ndoa ni lazima upewe cheti. There's no way hutapewa, maana gharama zake unazitoa mapema kabisa kabla siku ya ndoa.

Halafu kuhusu uhalali wa ndoa hiyo kidini, ni kwamba tukio la kutoa cheti cha ndoa ni sehemu ya taratibu za kufungisha ndoa. So kama wewe na mkeo hamtasaini vyeti vyenu, nachelea kusema kuwa tukio la kufunga ndoa hapo litakuwa halijakamilika.
Ndoa sio posho hadi msaini document. Ndoa ni maelewano ya me na ke , hizo zingine ni biashara na slave of mind.
 
Cheti cha ndoa ni kwa ajili ya serikali na mambo ya mirathi.
 
cheti cha ndoa ni uthibitisho wa kiserikali ili ikitokea tatizo kati ya wanandoa muwe mnatambulika.
ila katika dini siyo lazima bila hata cheti ndoa bado ni halali kama vigezo vya ndoa vimetimia (kiislam)
Kiserikali ndoa ni mkataba; na mkataba wowote lazima uwe na documents za kuuthibitisha iwe mahakamani or elsewhere just in case. Kiimani, ndoa ni ibada; na hakimu mkuu kiimani ni yeye aliye Muumba. Hahitaji docs zozote maana yeye ni mjuzi wa yote.
 
Ukifunga ndoa Kanisani au msikitini bila cheti, hiyo ndoa ni halali kidini?

Serikali ikiamuru makanisa na misikiti yaweke sanamu la shetani kwenye nyumba za ibada, watatii?
swali zuri sana hili, ngoja nikujibu: unaambiwa hata ukifunga huko na kupewa cheti, kama aliyewafungisha hajasajiliwa kufungisha ndoa, hiyo ndoa itakuwa batili. Kuhusu kuwekwa sanamu hapa ni papana zaidi sijui kiwango chako cha kiroho ningekujibu ni sanamu zipi unazizungumzia, ni midoli au ni kitu gani?
 
Back
Top Bottom