Je dini zitaeweza kuhimili maendeleo ya teknolojia?

[ Aisee!!

Hivi maendeleo ya teknolojia yanafanana kwa nyakati zote? Jee kabla ya kuvumbuliwa Kwa Spika Adhana misikitini zilikuwa zinapigwa kama siku hizi?

Kabla ya kutengenezwa Kwa kengele wakristo walikuwa wanajulishana muda wa ibada kama Sasa?

Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yamewezesha watu kuwasiliana kubadilishana maarifa kirahisi zaidi kuliko ilivyokuwa zamani.

Sasa historia inaonesha vitabu vya dini vilikuwa vipo kwa baadhi tu ya watu, lakini Sasa hakuna kitabu Cha dini yoyote kisichoko kwenye mitandao ya kijamii.

Sasa hizo teknolojia za zama hizo ambazo Bado dini ziliweza kizistahimili zinafanana na zilizopo sasa?
 
Bwashee sio mada hii tu,hili jukwaa kwa asilimia kubwa halina muangalizi,kuna nyuzi nyingi sana watu wanatukana lakini hioni hatua zozote zinachukuliwa,mbona sisi wengine hata tukitofautiana na watu kimtazamo huwa hatutukani


Uongozi umeshindwa kusimamia nidhamu ya jukwaa
 
Haya maelezo yako yanathibitisha ninachokisema. Wao wanasema kama kitu hakikuandikwa kwenye Quran basi hakipaswi kufuatwa.

Maana kwa mtizamo wao Quran ni timilifu aihitaji kuthibitishwa na Hadithi.
 
HAIWEZEKANI. Tena hizi dinimbili ndo kabisaa, Upande mmoja wanakwambia dogo Mudy alienda jelusalem na farasi anaepaa, upande wa pili blasa Ima alikufa akafufuka na akapaa mwenyewe mpaka mbinguni.
Sayansi inakataa vyote hivyo na haviwezi kuthibitishwa (ushahidi upo kwenye vitabu vyao na katuni tu).

Walivokua wanatunga dini zao hawakujua kua teknolojia itakua hivi.
 
Bahati mbaya sana ndio leo umenifahamisha kuwa huku kuna uongozi bwashee, binafsi mimi ndio kiongozi wa serikali yangu nikitaka kukwepa kuona takataka yoyote huyu na tia ignore tu.
 
ila inatokana na matumizi au mapokezi ya teknolojia, kuna watu wamekuwa waislamu na wengine imani imeongezeka kutokana na ugunduzi uliofanywa na nasa au maabara za kisayansi, mfano kuna aya inaelezea nyota inayogonga au inayongaa kama mapigo ya moyo na baadae nasa wakagundua puslar yenye sifa kama hizo, sasa hivi kuna app inayosoma quraan huku ukipewa na tafsiri na visa vya kwenye aya fulani hivyo inaonyesha faida ya teknolojia
 
Kwanza kabisa jiulize "essence(kiini)" ya Dini na Teknolojia ni nini!?

Dini ni nini!? Adhana, kengele n.k ni physical attributes za Dini na sio Dini.

Kwanini zimeishi pamoja kwa maelfu ya miaka!?

What makes it now 'special'!?

Je, tupo kwenye apex/ climax ya Maendeleo ya Teknolojia!?

Je, unaweza kutudhibitishia kwamba Maendeleo ya Teknolojia in the future hayawezi kuleta revelations zaidi ambazo hatuzifahamu kwa sasa na kuzaliwa kwa Dini mpya au kuimarika kwa Dini kongwe!?
 
😁

Haziwezi mkuu kabisa

Unakuta mtu mzima imefika mwaka 2026 ila anaaamini eti akienda mbiguni atapata thawabu ya mito ya pombe na wanawake wa kumfariji

Sasa najiuliza hio mbigu au coco beach
Kama mbinguni kuna mito ya pombe kwanini huku duniani wanakatazwa kuzitumia! Si waanze kutumia tokea huku ili wakifika kule ni muendelezo.
 
Kama mbinguni kuna mito ya pombe kwanini huku duniani wanakatazwa kuzitumia! Si waanze kutumia tokea huku ili wakifika kule ni muendelezo.
Ndio hapa unaona kuwa hizi dini ni mindgames na zinacheza katika vichwa vya wapumbavu kama ERTUGRUL BEY,

Atakupa vifungu vingi vilivyoandikwa na mwanaume mwenzake ila yeye anakuja kuviamini asilimia mia nne na vinaendssha mustakabali wa maisha yake hadi kusahau utashi wake

Akiambiwa hua huyu aanaua kweli, akiambiwa oa mtoto wa miak 10 anaoa kweli

UTAHIRA
 
Maendeleo ya technology ni MUNGU anasema: SI NILIWAAMBIA?

Wewe unaona yamekuja kupindua imani, sisi huku tunaona merging of prophecy on all fronts, yamekuja kuimarisha imani.

MUNGU WETU ALISEMA, JE HAYATOKEI KAMA ALIVYOSEMA? ? ?

TUMIA AKILI.

1)
"Basi, huyu mnyama wa pili akafanya miujiza mikubwa hata akasababisha moto kutoka mbinguni ushuke duniani mbele ya watu.

Aliwapotosha wakazi wa dunia kwa miujiza hiyo aliyojaliwa kutenda mbele ya mnyama wa kwanza. Aliwaambia wakazi wa dunia watengeneze sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi tena.

Kisha alijaliwa kuipulizia uhai hiyo sanamu ya yule mnyama wa kwanza, hata ikaweza kuongea na kuwaua watu wote ambao hawakuiabudu.

Aliwalazimisha wote, wadogo na wakubwa, matajiri na maskini, watu huru na watumwa, watiwe alama juu ya mikono yao ya kulia au juu ya paji za nyuso zao.

Akapiga marufuku mtu yeyote kununua au kuuza kitu isipokuwa tu mtu aliyetiwa alama hiyo, yaani jina la yule mnyama au tarakimu ya jina hilo.

Hapa panatakiwa hekima! Mwenye akili anaweza kufafanua maana ya tarakimu ya mnyama huyo, maana ni tarakimu yenye maana ya mtu fulani. Tarakimu hiyo ni 666."

Ufunuo13.13-18.BHN


2) "
Ila sasa, Danieli, weka siri mambo hayo; kifunge kitabu na kukitia mhuri mpaka wakati wa mwisho utakapofika. Wengi watakimbilia huko na huko, na maarifa yataongezeka."
Danieli.12.4.BHN

3) Hata nyie mlioiacha imani na kujiona mna akili sana na kukumbatia dini yenu mpya ya scientism inayoamini sayansi ndo itawapa majibu ya kila kitu maishani, na kukumbatia kutafuta utajiri kama lengo la maisha yenu, hata nyie ni utimizo wa unabii. Sisi tuaminio tukiwaona tunafarijika kwani SI MUNGU WETU ALISEMA? ? JE HAYAWI?

"Kumbuka kwamba, katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu.

Watu watakuwa na ubinafsi, wenye tamaa ya fedha, wenye majivuno, wenye kujiona, wenye kumtukana Mungu.... na waovu..."

2Timothy.3.1-2.BHN


"Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana."
Mathayo.24.10.BHN



BTW hizo nchi mnazozihusudu zimeendelea sana zimejengwa na kina nani? ?


Wangekuwa washika mauzauza tangu mwanzo mnafikiri wangefika hapo? ?

Ukitaka kujua faida za mauzauza ona hali zilivyo sasa hivi huko. We have a mentally disturbed, drug consuming generation who dont even know what gender they are! ! !

Are these the people who could have built those nations? ? ?

Most seem to only get meaning in life from fighting people with meaning in life: peole with faith.

The paradox. You dont believe in something then spend your whole life consumed by it. Speaking of being mentally disturbed.


Let's hear from the founding fathers of America:

i) George Washington, Rais wa kwanza wa Marekani, alisema:

“Unafanya vyema kutamani kujifunza sanaa zetu na njia zetu za maisha, na zaidi ya yote, dini ya Yesu Kristo. Mambo haya yatakufanya muwe taifa kubwa zaidi na lenye furaha kuliko mlivyo sasa.”

ii) John Adams, Rais wa pili wa Marekani, alisema:

“Kanuni za jumla ambazo mababa wa taifa walitumia kufikia uhuru zilikuwa kanuni za jumla za Ukristo Ninakiri kwamba niliamini wakati huo, na ninaamini hata sasa, kwamba kanuni hizo za jumla za Ukristo ni za milele na zisizobadilika kama vile uwepo na sifa za Mungu.”

iii) John Quincy Adams, Rais wa sita wa Marekani, alisema:

“Katika mfululizo wa matukio ya kibinadamu, siku ya kuzaliwa kwa taifa letu imefungamanishwa bila kutenganishwa na siku ya kuzaliwa kwa Mwokozi. Azimio la Uhuru liliweka jiwe la msingi la serikali ya wanadamu juu ya kanuni za kwanza za Ukristo.”

iv) Maneno kutoka Azimio la Uhuru wa Marekani (Declaration of Independence):

“Tunashikilia ukweli huu kuwa ni wa wazi wenyewe, kwamba watu wote wameumbwa wakiwa sawa, kwamba wamepewa na Muumba wao haki fulani zisizoweza kunyang’anywa, na miongoni mwa haki hizo ni Uhai, Uhuru, na utafutaji wa Furaha... Na kwa ajili ya kuunga mkono Azimio hili, kwa kutegemea kwa uthabiti ulinzi wa Maongozi ya Kimungu (divine Providence), tunaahidiana sisi kwa sisi kutoa Maisha yetu, Mali zetu, na Heshima yetu takatifu.”

v) Na maneno kutoka rais wa mwisho wa Marekani, Donald Trump (I don't believe I'm quoting this guy):

"I believe people can't be happy without religion, without that belief. Let's bring religion back. Let's bring God back into our lives".
 
Tayari distortions zipo. Kutumia tu hii kalenda ya Gregorian ni kosa. Lakini kwa nini mnaitumia? Huoni tayari maendeleo ya teknolojia yameondoa uhalisia wenu?
Mnasheherekea maulid! birthday ha kuzaliwa mtume), hii nayo ishaondoa uhalisia
 
Wanabisha vitu ambavyo vipo wazi. Anasema hawawezi kubadilishwa na teknolojia wakati bado wanatumia madawa ambayo yana uwezo wa kubadilisha hadi DNA.
 
Teknolojia ni upanga wenye pande mbili, upande mmoja imesaidia kuonyesha illogical , ujinga, uongo na utata wa dini, upande mwingine teknolojia hiyo hiyo imesaidia kuziremba(romanticize) dini na kuzipa muonekano mzuri wa kuvutia katika jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…